Tafuta

Ziara ya Papa Francisko nchini Lithuania, Latvia na Estonia Ziara ya Papa Francisko nchini Lithuania, Latvia na Estonia 

Salam za Papa kwa wanahabari na telegram kwa marais wa nchi !

Wakati za kusalimia waandishi wa habari katika ndege iliyokuwa inawapeleke Jiji la Vilnus Lithuania, Papa Francisko amesema hizi ni nchi tatu ambazo zinafanana lakini zenye utofauti, hivyo itakuwa kazi nzuri hasa ya kuwa na umakini kama waandishi kutazama ufananisho na utofauti huo pamoja na kwamba wanayo historia inayowashirikisha pamoja

 

Ni ziara ya kitume ya 25 kimataifa ambayo  Baba Mtakatifu Francisko, tarehe 22 Septemba mapema, amewasiri nchini Lithuania na kupokelewa katika uwanja wa kimataifa mjini Vilnius.

Greg Burke: Ni wakati wa kusalimia Papa

Wakati wa safari ya kuelekea Vilnius Papa Francisko amepata fursa ya kuwasalimia waandishi wa habari waliokuwa naye katika ndege. Kwanza Bwana Greg Burke Msemaji Mkuu wa Vatican ametangulia kumsalimia Baba Mtakatifu Francisko,  kwamba amefikia kwa mara nyingine tena ziara ya 25 ya kimataifa. Na kuendelea kumtambulisha juu ya waandishi waliokuwa nao kwamba, "wandishi wa habari walio wengi anaamini au tofauti wamefanya safari nyingi, wengine ni safari yao mpya ya kwanza, wakiwemo hata waandishi tisa wa chi za Kibaltiki". Kutokana na hilo Bwana Burke anasema “ ninachukua fursa hii kuwakumbusha wote kwamba, ni kipindi sasa cha kusalimia kwa haraka bila video, mahojiano, selfie au kadha wa kadha, lakini kusalimia kwa haraka. Bwana Burke akimgeukia Baba Mtakatifu amesema, “ labda wewe unataka kusema neno kwanza….

Papa Francesco: Wao wana historia wanayoshirikishana pamoja

Naye Papa Francisko akijibu ametamka :” habarini za asubhui. Ninawashukuru sana kwa usindikizaji wenu na shauku zenu. Ni nchi tatu ambazo zinafanana lakini zenye utofauti, na itakuwa kazi nzuri kwa ajili ya umakini wenu, kutazama ufananisho na utofauti huo. Wao wanayo historia ya pamoja, lakini tofauti na hivyo itakuwa ni vizuri!  Asante sana! Baba Mtakatifu amehitimisha.

Telegram kwa marais wa nchi alizopitia akiwa wangani

Baba Mtakatifu akiwa angani katika ndege iliyokuwa inampeleka Lithuania, zaidi ya Italia ametuma hata telegram kwa marais wa Croazia Kolinda Grabar-Kitarovic, Rais wa Hungary Janos Ader, rais wa  Slovacchia Andrej Kiska na Rais wa Poland Andrzej Duda. Na kwa kila moja ya nchi hizi Papa Francisko amewabariki kwa Baraka ya Mungu ili awapatie zawadi ya amani, furaha na matarajio mema!

22 September 2018, 10:12