Tafuta

Vatican News
Ziara ya Papa nchini za  Lithuania, Latvia na Estonia Ziara ya Papa nchini za Lithuania, Latvia na Estonia  (AFP)

Papa yuko kwenye ndege angani kuelekea Lithuania!

Ziara ya Papa Francisko, imeanza asubuhi ya siku ya Jumamosi tarehe 22 Septemba 2018, saa 1.37 masaa ya Ulaya, ikiwa ni ziara ya 25 ya kitume katika nchi za kibaltiki, Lithuania, Latvia na Estonia. Anatarajiwa kufika huko Vilnius majira ya saa 5.30 masaa ya huko na italia ikiwa ni saa 4.30 masaa ya Italia

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Jumamosi ya tarehe 22 Septemba 2018, Papa Francisko amefika uwanja wa ndege wa Leonardi da Vinci Fiumicino  majira ya saa 1.15 asubuhi masaa ya Ulaya, katika gari la Kipapa na kuegeshwa katika uwanja wa faragha ndege ya Alitalia  A320  iitwayo “Aldo Palazzeschi” ambayo ndiyo sasa inampeleka huko Lithunia ikiwa ni hatua ya kwanza ya ziara ya kitume ya 25 katika nchi za Kibaltiki.

 Salam za Papa kwa walio msindikiza uwanjani

Aliye toa salam akiwa katika mstari wa mbele kabla ya kupanda ndege ni viongozi wa serikali ya raia na kidini. Kama kawaida kwa tabasamu na akiwa  kashika mkono wa kushoto mfuko wake mweusi amekwenda moja kwa moja hadi ngazi na kuzipanda. Baada ya kufika juu amewasalimiana na mahostess na marubani wa ndege waliokuwa wanamsubiri. Baadaye amegeuka na kuwapungia mkono wa kwaheri wote walikuwa wanamsindikiza.

Ratiba ya siku nchini Lithuania

Ndege inatarajiwa kufika mji Mkuu Vilnius nchini Lithuania saa 11.30 masaa ya huko. Na baadaye kutakuwa na sherehe fupi ya kumkaribisha rasmi katika uwanja wa kimataifa. Saaa 6.10 Papa Francisko anatembelea Rais wa nchi Bi Dalia Grybauskaite katika Ikulu yake, mahali ambapo saa 6.40 atakutana na viongozi wa serikali ya Lithuania, raia na viongozi wa kidiplomasia. Saaa 10.30 za alasiri, anatarajia kutembelea Madhabahu ya (Mater Misercordiae) Mama wa huruma na saa 11.30 atakutana na vijana katika uwanja karibu na Kanisa Kuu; saa 12.40 za jioni atatambelea Kanisa Kuu. Na mara baada ya hapo atakwenda katika Ubalozi wa Vatican ulioko mjini Vilnius ,mahalia   Papa Francisko atakuwa anapata malazi kwa kipindi chote cha ziara yake katika nchi za Kibaltiki

Papa watakia matashi mema na utulivu kwa nchi ya Italia

Kama ilivyo desturi yake, wakati wa kuanza safari yake kuelekea Jamhuri za Kibaltiki, Papa Francisko ametuma salam kwa Rais wa Jamhuri ya Italia Bwana Sergio Matarella katika salam hizo Papa anaandika: “ Katika kipndi ambacho ninaondoka kuelekea katika ziara ya kitume nchini Lithuania, Latvia na Estonia, ninapendelea kukupatia wewe Bwana Rais na watalia wote salam za matashi mema, ambazo zisindikize kila heri ya amani na utulivu”.

 

22 September 2018, 08:55