Katekesi ya Papa tarehe 26 Septemba 2018 Katekesi ya Papa tarehe 26 Septemba 2018 

Papa:Katekesi imejikita juu ya ziara yake ya kitume nchi za kibaltiki!

Nchini Lithuania, Latvia na Estonia, utume wangu ulikuwa ni kutangaza kwa upya “furaha ya Injili na mapinduzi ya huruma na upendo; hiyo kwa sababu haitoshi tu kuwa na uhuru, pia ukamilifu wa maisha bila upendo utokanao na Mungu. Ni kwa mujibu wa Maneno ya Papa Francisko wakati wa katekesi yake mjini Vatican akisimulia juu ya ziara yake ya kitume nchi za Kibaltiki

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Katika katekesi ya Baba Mtakatifu Francisko Jmato tarehe 26 Septemba, imejikita katika hatua zake za ziara ya Kitume nchini Lithuania, Latvia na Estonia, iliyotimilizika jioni ya tarehe 25 Septemba kwa kuwaachia wito wa kutangaza kwa upya furaha ya Injili na mapinduzi ya huruma, upendo katika nyakati za huruma ambao ndiyo safari ya kila siku inayotoa radha ya maisha...

Nchini Lithuania, Latvia na Estonia, utume wangu ulikuwa ni kutangaza kwa upya “furaha ya Injili na mapinduzi ya huruma, upendo, kwa sababu haitoshi tu kuwa na uhuru, pia ukamilifu wa maisha bila upendo utokanao na Mungu. Ndiyo kiini  maelezo ya Baba Mtakatifu Francisko akifafanua kwa mahujaji na waumini zaidi 20.000 waliounganika katika uwanja wa Mtakatifu Petro,ambapo amewaeleza juu ya thamani ya ziara yake ya kitume katika nchi za kibaltiki, iliyomalizika tarehe 25 Septemba 2018.

Baba Mtakatifu amejikita kuelezea hatua zake zote za nchi kwa siku  nne alizotembelea kuanzia Mji Mkuu Vilnius hadi Tallin, kupitia Kaunas, Riga, na Aglona, ziara iliyo andaliwa katika fursa ya kuadhimisha miaka 100 ya uhuru dhidi ya  majeshi ya Urusi wa Zar.  Papa amekumbuka kuwa nchi tatu wameishi miaka miamoja  na karibu nusu yake wameishi  chini ya mzigo mzito  wa kutawaliwa na  majeshi ya  kidikteta ya vita ya Pili vya Dunia,  kwanza wa kisovieti na baadaye wengine. Ni watu ambao waliteseka sana, kwa maana hiyo anasema, Mungu aliwatazama kwa hali ya upendeleo.  

Lakini mantiki hiyo ilibadilika sana, tangu safari ya Mtakatifu Yohana Paulo II, miaka 25 iliyopita, katika nchi zilizo kuwa zimetoka chini utawala mzito wa mzigo wa ukomunisti.  Na ndio maana utume wa Papa ulikuwa ni kutangaza kwa upya furaha ya Injili na mapinduzi ya huruma. Injili ambayo wakati wa majaribu hutoa nguvu na kutoa mwamko wa mapambano kwa ajili ya uhuru, katika kipindi cha uhuru hutoa mwanga kwa ajili ya safari ya kila siku ya watu, familia na jamii na chumvi inayotoa radha  ya maisha ya kila siku  na kulinda dhidi ya ufisadi, ubinafsi. Amethibitisha Papa.

Akiendelea kufafanua zaidi, Baba Mtakatifu amekumbusha kuwa, nchini Lithuania wakatoliki ndiyo wengi wakati Latvia na Estonia wapo walutheri na waorthodox, lakini ambao wamekwenda mbali na maisha ya dini. Kwa maana hiyo changamoto ni ile ya kuongeza nguvu ya umoja kati ya wakristo ambao ulikuwa umeendelezwa, wakati wa kipindi kibaya cha mateso.

Kwa wote hao, Baba Mtakatifu amesisitiza juu ya kipindi cha sala ya kiekuemene katika Kanisa Kuu la Riga na kukutana na vijana huko Tallin. Kadhalika katika mkutano na viongozi wote wa nchi tatu, ameonesha umuhimu wa mchango mkubwa ambao wanautoa katika umoja wa Mataifa hasa kwa Ulaya. Mchango ambao ni thamani ya kibinadamu na kijamii kwa nyakati zilizopita za majaribu. Kwa viongozi hao amesema alitoa ushauri wa kuunganisha daima uhuru, mshikamano na mapokezi.

Papa amekumbusha pia mkutano na vijana wa Vilnius, mahali ambapo walishuhudia, na kuonesha furaha ya katika maombi na nyimbo, zaidi hata kuonesha huduma kwa wengine ambayo ni njia ya kuondokana na wigo la umimi, ili kutembea kwa pamoja, kuwa na uwezo wa kuamka mara tu baada ya kuanguka. Na kwa wazee huko Riga, Papa amesisitizia juu ya mahusiano, na  kati ya uvumilivu na matumaini.

Kadhalika amekumbusha juu ya mkutano wa Lithuania kwa na mapadre, watawa na waseminari ambao amewahimiza juu ya matumaini na ukuu wa msimamo, na ili wapate kumweka Mungu awe kitovu cha maisha yao, katika misingi y a upendo wake. Katika hali hiyo, anathibitisha juu ya ushuhuda ambao unatolewa na mapadre wengi, watawa kike na kiume wazee. Wengine wameteseka sana, kufungwa kuchukuliwa… lakini wamebaki kidete katika imani. Baba Mtakatifu amewashauri wasisahau, kuhifadhi kumbukumbu ya mashahidi, kwa kufuata mifano yao hasa watawa, mapadre na waseminari vijana.

Katika mji wa Vilnius, ametoa heshima katika mnara wa waathirika wa mauaji ya kimbari  kwa wayahudi wa Lithuania,  kwa dhati miaka 75 iliyopita  ya kufungwa mtaa wa kibaguzi, uliokuwa na vyumba ambamo waliua maelfu na maelfu ya wayahudi. Pia Papa alitembelea Jumba la Makumbusho na mnara wa Mapambano ya kudai uhuru, mahali ambapo alisimama kitambo kwa sala, sehemu ambazo waliteswa na kuwauwa waliokuwa wakipinga utawala wa mabavu wa udikteta.

Hata hivyo ishara hai daima ipo Injili ya upendo. Baba Mtakatifu amethibitisha. Mahali ambapo kuna kumezwa kwa malimwengu, Mungu anazungumza na lugha ya upendo, analinda, anatotoa huduma ya bure kwa wale wanaohitaji. Na kwa maana hiyo mioyo inafunguka na miujiza inatokea na  katika jangwa vichipukizi vipya vinatokea.

Mwisho Papa amekumbuka Misa tatu huko Kaunas, nchini Lithuania ,  Aglona nchini Latvia na Tallin, nchini Estonia mahali ambapo Papa amesema,” waamini wa Mungu katika safari kwenye  ardhi zile, wameweza kupyaisha “ndiyo” yao kwa Kristo tumanini letu; wamepyaisha na Mama Maria ambaye daima ni Mama wa mwana wake hasa kwa wale wanaoteseka.

 

26 September 2018, 14:42