Tafuta

Vatican News
Papa Francisko na Rais wa Lithuania Bi Dalia Grybauskaite  Papa Francisko na Rais wa Lithuania Bi Dalia Grybauskaite   (AFP or licensors)

Papa: Lithuania inatufundisha namna ya kupokea wageni!

Katika hotuba yake ya kwanza nchini Lithuania, akihutubia raia wa Jamhuri na viongozi , Papa Francisko amesisitizia juu ya mazungumzo na heshima na makaribisho, kama ishara msingi ya watu wa Lithuania

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Tarehe 22 Septemba 2018, wakati wa mkutano na Viongozi wa Serikali, jamii ya raia na kidiplomasia mjini Vilinus, ameanza kuonesha sababu ya furaha yake na matumaini ya kuanza hija yake katika nchi za kibaltiki,  hasa katika nchi ya Lithuania. Hiyo ni kama jinsi alivyopenda kusema Mtakatatifu Yohane Paulo II kwamba ni “ushuhuda wa kimya kwa upendo na shauku kwa ajili ya uhuru wa dini, ( rej Hotuba ya makaribisho Vilnius, 4 Septemba 1993).

"Wana wako wanaweza kupata nguvu kutokana na  nyakati zilizopita", ndiyo pia maneno aliyo sema Baba Mtakatifu Francisko akiendelea na hotuba yake  na  kuutaja wimbo wa Taifa la Lithuania. Mbele ya Rais wa nchi,  Bi Dalia Grybauskaite na wawakilishi wa taasisi mbalimbali waliounganika karibu na ikulu ya rais, Papa ametaja ziara yake kuwa, imejikita katika fursa ya kuadhimisha miaka 100 tangu kutangazwa kwa uhuru wa nchi. Papa Francisko amethibitisha kuwa wanachi wa lithuania kwa miaka 100 ya mwisho wamekumbana na majaribu mengi na mateso, hadi kufikia ushahidi. Ni majaribu lakini ambayo haya kuwafanya watu wakate tamaa, kwa maana ni watu wenye roho ya nguvu!

Historia ya Lithuania ina tabia ya kukaribisha

Baba Mtakatifu akiendelea na hotuba yake, amesema, ni muhimu kukumbuka katika kutazama changamoto za wakati uliopo  na kulekeza maono ya wakati endelevu katika hali ya mazungumzo na umoja kati ya wazalendo, kwa namna ya kutomwacha mtu yeyote yule nyuma.  Amesema hayo kutokana na kwamba, katika hotuba hiyo, mada yake ilikuwa juu ya mazungumzo na kukaribisha. Akiendelea anasema, wananchi wa Lithuani wametambua kupokea watu tofauti, wa kabila na dini. Wote “wameishi kwa pamoja kwa amani hadi walipoingiliwa tikadi za kikatili  ambazo zilivunja uwezo wa kupokea na kuunganisha tofauti kwa kupanda vurugu na kutoaminiana".

Kukaribisha utofauti kama mfano wa Ulaya

Lakini pamoja na hayo Papa anaongeza kusema, “kuchota nguvu ya wakati uliopita, ina maana ya kurudisha mizizi na kuhifadhi uhai wake wa kuvumilia, kukaribisha, kuheshimu na mshikamano”. Kwa maana hiyo nchi ya Lithuania ameitafsiri kama kisima cha ardhi ya umoja na matumaini. Baba Mtakatifu pia akitazama hali halisi ya dunia tunamoishi, mahali ambamo anasema “kelele zinazidi kukua ambazo zinapanda mgawanyiko na mivutano, kutenganisha na mara nyingine kutumia suala la  usalama na mgogoro au ambao wanatangaza kuwa, njia pekee inayo wezekana ya kuhakikisha usalama na kuwepo kwa utamaduni, ni kujaribu kuondoa, kufuta au kuwatoa wengine”;  anaongeza kusema, “ lakini kwa watu wa Lithuania, wamekuwa na neno moja asili katika  kupeleka mbele, yaani “kukaribisha utofauti, kwa njia ya mazungumzo, uwazi na uwelewa ya kwamba, wao wanaweza kubadilisha kuwa daraja la umoja kati ya Mashariki na magharibi ya Ulaya. Hiyo ndiyo “inaweza kuwa tunda la historia iliyo komaa ambayo kama watu, "ninyi mnaendelea kutoa katika jumuiya ya kimataia, kwa namna ya pekee ya Umoja wa Ulaya”.

Kuwategemea vijana ili watazame wakati endelevu kwa matumaini

“Ninyi mmteseka katika ngozi yenu majaribu ya kulazimishwa mtindo mmoja wa kufuta utofauti”, Baba Mtakatifu anaendelea kusema, ni  “wakati  huo migogoro inayosikika, inaweza kusuluhishwa, iwapo ni kukaa katika mzizi  kwa umakini wa dhati na watu, hasa walio wadhaifu”. Kwa maana hiyo anathibitisha kwamba,  “kuchota nguvu ya wakati uliopita maana yake ni kutoa kwa namna ya pekee umakini zaidi hasa kwa vijana”. Katika watu, mahali ambapo vijana wanapata nafasi ya kukua na kufanya kazi, inawazidishia kuhisi  kwao yakuwa wako mstari wa mbele katika ujenzi wa kiungo cha kijamii na umoja.

Hiyo  itawawezesha kutazama wote, upeo wa matumaini ya kesho kwa Vijana ambao wanaota ndoto ya nchi ya Lithuania ambayo inaendelea kutafuta, kuhamasisha sera za kisiasa ambazo zinaongeza ushiriki hai wa vijana katika jamii. Baba Mtakatifu akihitimisha hotuba yake, anasema hiyo ndiyo itakuwa ni mbegu ya matumaini ambayo itapeleka katika mwendo wa roho ya watu hawa na kuendelea kuongeza ukarimu na  makaribisho. Makaribisho kwa ajili ya wageni, makaribisho kwa vijana, makaribisho ya wazee, makaribisho ya masikini na mwishowe, makaribisho ya wakati endelevu”.

Shukrani kwa Rais wa Lithuania Dalia Grybauskaite

Kwa upande wa Rais wa nchi ya Lithuania, Bi Dalia Grybauskaite kwa Papa Francisko. Amemshukuru Papa Francisko kwa ziara yake na  kwamba "ni zawadi nzuri, katika mwaka wa mia moja  wa ujenzi wa nchi" . Hata hivyo ameongeza kusema kwamba, Vatican imekuwa daima ikiunga mkono mawazo ya nchi ya Lithuania. Kadhalika amesisitiza kwamba, katika miaka ya mwisho ya majaribu yao, watu wa Lithuania walikombolewa  kwa kuwa na imani ya na thabiti. Imani ambayo hadi sasa inawawezesha watu hao hasa vijana kutazama wakati endelevu kwa matumaini!

22 September 2018, 13:33