Tafuta

Vatican News
Papa Katika Kanisa Kuu la Kianglikani huko Latvia Papa Katika Kanisa Kuu la Kianglikani huko Latvia  (Vatican Media)

Papa huko Riga: Roho Mtakatifu awe silaha ya mazungumzo!

Kuwa “wafuasi wa kimisionari wa Bwana katikati ya dunia tunamoishi”, ndiyo wito wa Baba Mtakatifu Francisko kwa waamini wa makanisa tofauti ya wakristo wa Latvia ambao wanawakilisha karibia asilimia 60% ya watu wote, waliounganika katika Kanisa Kuu la Kiluteri la Mtakatifu Maria huko Riga, tarehe 24 Septemba 2018

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Baba Mtakatifu katika mkutano wa kiekuemene kwenye Kanisa Kuu la Kianglikani huko Riga nchini Latvia ameomba Mungu ili ushuhuda wa ndugu ambao leo hii wanaishi uhamishoni, hadi kufikia ushahidi kwa ajili ya kutetea imani yao, unawezesha kugundua kuwa Bwana anatuita wote kuiishi Injili kwa furaha, shukrani na uthabiti!

Wafuasi wa kimisionari

Kuwa “wafuasi wa kimisionari wa Bwana katikati ya dunia tunamoishi”, ndiyo wito wa Baba Mtakatifu Francisko kwa waamini wa makanisa tofauti ya wakristo wa Latvia ambao wanawakilisha karibia asilimia 60% ya watu wote, waliounganika katika Kanisa Kuu la Kiluteri la Mtakatifu Maria huko Riga, tarehe 24 Septemba 2018.

Mara baada ya kusalimiana viongozi kumi wa makanisa tofuati na baada ya kutoa heshima katika kaburi la Mtakatifu Meinardo, Baba Mtakatifu amesali kwa ajili ya nchini ili  kuweza kuendelea kupiga muziki wa Injili katika ardhi  hiyo ya Latvia, na amaayo ndiyo tabia ya nchi kwa mujibu wa maoni ya Papa Francisko.  Akiendelea na sala hiyo amesema:“ ili kuweza kutimizia safari kwa mujibu wa  ushirikiano na urafiki wa kiekumene, mahali ambapo wanaweza kuwa na  umoja kwa kuhifadhi utajiri wa kila moja ya jumuiya ya kikristokatika uekemene huo ambao ni sababu ya matumaini na kushukuru neema ya Mungu…

Njia yenye uwezekano kwa ajili ya uekumene

“Ili wote wawe na umoja” ndiyo sala ambayo Yesu alimwelekeza Baba wa Mbinguni  kabla ya sadaka yake kuu ya mwisho, kwa “kutazama na  uso wake  juu ya msalaba na msalaba wa ndugu wengi ambao wanapitia katika njia hiyo wakielekea njia ya kumfuasa Yesu”. Akiwa amejikita katika sala ya kina, kama waamini wake, katika Kanisa, likitamani umoja wa neema ya Baba aliyo nayo kwa ajili ya binadamu wote, Baba Mtakatifu anaongeza: “ tunapata njia moja yenye uwezekano wa kila njia ya  uekuemene. Katika msalaba wa mateso ya vijana wengi, wazee na watoto ambao mara nyingi wananyonywa, kuonekana hawana maana, ukosfu wa fursa na hata upweke. Wakati Yesu anatazama Baba yake na sisi ndugu; Yeye hachoki kamwe kuomba ili sisi tuwe wamoja”, Baba Mtakatifu amethibitisha.

Kazi ya fundi seremala

Akimsalimia Askofu Mkuu Jānis Vanags, ambaye kabla alikuwa ametoa hotuba yake na akikumbuka kwa ufupi mzigo mzito wa nusu karne ya kukana Mungu wakati wa kipindi cha wasovietiki, Baba Mtakatifu amebainisha kuwa Kanisa Kuu la mji mkuu haswa ni shuhuda ambao kwa zaidi ya miaka 800 wanakaribisha maisha ya kikristo katika miji na ushuhuda wa waamini wengi na ndugu wengi ambao wameweza kuingia humo kusali, kuabudu na kuonesha matumaini katika nyakati ngumu za mateso na kupata ujasiri wa kukabiliana na kipindi cha ukosefu wa haki na uchungu.

Leo ni Roho Mtakatifu anakaribisha na kuendelea kuwa kama serelemala, akitengeneza mahusiano kati yetu na kutufanya fundi seremala kati yetu katika umoja kati ya watu , kwa namna ya tofauti zetu zisiwe chanzo cha utengano. Na hivyo ameomba wamwachie Roho Mtakatifu aweze kuwa ndiyo silaha ya mazungumzo, maelewano na kutafuta namna ya kuheshimiana mmoja na mwingine kama ndugu

Kuelekea katika jamii ya kisasa

“Umoja ambao Bwana anatuita dima ni ufunguo wa kimisionari ili kutoka nje na kufikia moyo wa watu, utamaduni wa jamii ya kisasa ambayo tunaishi”. Na huo ndiyo utume wa Kiekuemene ambao tutaweza kuukamilisha, na dhahiri iwapo tutoacha Roho wa Kristo afanye kazi ndani mwetu!

 

 

24 September 2018, 14:12