Ziara ya Kitume ya Papa nchini Estonia Ziara ya Kitume ya Papa nchini Estonia 

Papa nchini Estonia:wakati endelevu wahitaji uwepo na ushiriki!

Hotuba yake ya kwanza katika ziara ya Papa nchini Estonia ni ile ambayo amehutubia mbele ya Rais wa Jamhuri ya Estonia, Bi Kersti Kaljulaid, viongozi wa kidiplomasia na raia wa nchi katika Bustani ya Mawaridi ya Ikulu huko Tallin, tarehe 25 Septemba 2018

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

“Watu watakuwa na uwezo wa kutoa wakati endelevu katika kipimo ambacho watu hao wanatoa maisha katika mahusiano ya uwepo, kati ya watu wote na ushikirishwaji”. Ndiyo wito ambao Baba Mtakatifu Francisko ameutoa kwa viongozi wa Serikali, na wanadiplomasia katika Bustani ya Mawaridi katika Ikulu, mjini Tallin, ikiwa ndiyo mara yake ya kwanza kutembelea nchi ya Estonia na kituo chake cha mwisho wa ziara yake, katika  nchi ambayo imefanya uzoefu wa utawala wa kidikteta wa wakomunisti. Baba Mtakatifu katika hotuba yake amewakiwakikishia  msaada Kanisa Katoliki japokuwa iliyo  “jumuiya ndogo ambayo inawakilisha asilimia 0,5%  tu ya watu wote, lakini wenye utashi wa kutoa mchango katika  kutoa matunda ya ardhi”.

Matunda yanatokana na mizizi

“Leo hii, nchi inakabiliwa na kumezwa na ulimwengu, kwa asilimia 70% ya watu ambao wanadhihirisha “hawana  dini” na kiasi kikubwa cha  watu wenye kuwa na talaka ya ndoa”. Kwa wote Baba Mtakatifu Francisko anawakumbusha kuwa, ili ardhi iweze kuwa na rutuba, lazima iwe na mizizi. Hakuna jambo baya zaidi kuliko kufanya uzoefu wa kutokuwa na mizizi na kuhisi kuwa si mali ya mtu yoyote.  Nchi itazaa mataunda, watu watatoa matunda na watakuwa na uwezo wa kuzalisha wakati endelevu iwapo watakuwa tu  na kipimo cha kutengeneza mahusiano ya uwepo kati ya watu wake na  kipimo ambacho kinakuwa na uwezo wa kufanya mahususiano na vifungo vya ushirikiano kati ya vizazi na jumuiya mbalimbali zinazoijumuisha.

Nchi ya kumbukumbu

Ni ardhi ya Maria, Baba Mtakatifu anathibitisha, kwa maana ya karne nyingi, nchi hizi zimeitwa hivyo. Na Maria anasema maneno mawili: kumbukumbu na kuzaa. Kufanya kumbukumbu kwa watu wa Estonia, maana yake ni kukumbuka kipindi kigumu cha kihistoria, walichopitia katika kipindi cha mateso na dhiki, jitihada za uhuru na uhuru kamili, mambo ambayo yamewekwa daima  katika mjadala   au kutishiwa”. Hata zaidi ya miaka 25 yaani tangu uhuru kunako 1991, nchi ya Estonia imepiga hatua kubwa na sasa iko kati ya nchi zilizo za kwanza katika maendeleo ya kibinadamu, kwa uwezo wake wa ubunifu, uhuru wa vyombo vya habari na kisiasa. Kwa maana hiyo Papa anathibitisha kuwa, kuna sababu ya kutazama wakati endelevu lakini pia ni lazima kukumbuka historia ya wanaume na wanawake , yaani wahanga waliopambana ili kuwezesha uhuru huo”.

Nchi ya matunda

Kwa upande mwingine, Papa anasema , ni mwaliko wa kuwa na ardhi ya matunda; kwa maana  ustawi daima  sio sawa na kuishi vizuri, anathibitisha, kwa kutazama, “moja ya matukio ambayo yanaweza kutazamwa katika jamii zetu za kijamii katika masuala ya kiteknolojia, na kwamba ni kupoteza maana ya maisha, maana ya furaha  ya kuishi”,  na kwa jinsi hiyo, kuna umuhimu wa kuwa kusimika mizizi ya watu na utamaduni, na kwamba ili vijana waweze kupoteza mizizi mahali ambapo waweze kujenga wakati uliopo na endelevu kwa maana wanakosa uwezo wa kuota ndoto na kijimudu maisha yao bila kuogopa kujihatarisha katika kutafuta.

Kuwa na imani  katika maendeleo ya kiteknolojia, kama mojawapo ya uwezekano wa maendeleo, unaweza kusababisha kupotea kwa uwezo wa kuunda uhusiano binafsi, katika kizazi, kiutamaduni, kwa maana ya kusema kile kiungo hai cha maisha ambacho ni muhimu, ili kuhisi kama ushitiki wa kuwa sehemu moja na mwingine na kushirikiana katika mpango wa pamoja kwa maana ya kuwa na upeo mpana. Na matokeo yake, mojawapo ya majukumu muhimu tuliyo nayo kwa wale wanaohusika na jukumu la kijamii, kisiasa, elimu na kidini, ni sawa na jinsi tunavyoweza kugeuka kufanya kazi ya ufundi wa mahusiano. Amehitimisha Baba Mtakatifu.

Rais wa Estonia: Vatican ni kisima cha mamlaka ya kiroho kwa taifa enzi za wahanga dhidi ya ukomusti.

Kabla ya hotuba ya Baba Mtakatifu Francisko, naye Rais wa Jamhuri ya nchi ya Estonia, Bi Kersti Kaljulaid kwa niaba ya viongozi wote wa serikali amemkaribisha kwa shangwe na kutoa sifa kwamba , katika Mamlaka  yake ya kimaadili na kisiasa aliyo nayo, Vatican imekuwa daima kisima cha nguvu ya kiroho cha mataifa la Ulaya, kwa utambuzi mkuu wa  kuwasaidia wahanga dhidi ya Wakomunisti. Vatican iliwasaidia wahanga hao ili waweze kweli kuwa na uhuru na amekumbusha maneno ya Mtume Paulo katika Barua ya Warumi: msiache kushindwa na ubaya bali kushinda ubaya kwa wema”. Kadhalika amekumbua historia nzima ya miaka 100 iliyopita wakati wa vita ngumu ya kupambania uhuru wa nchi ya Estonia.

25 September 2018, 14:29