Ujumbe wa Papa Francisko kwa watu wa China Ujumbe wa Papa Francisko kwa watu wa China 

Ujumbe wa Papa kwa waamini wa China:Imani inabadili historia!

Katika ujumbe wa Papa Francisko kwa wakatoliki wa China na Kanisa la Ulimwenguni, anaeleza sababu iliyowafikisha kutia saini ya Makubaliano ya muda na Jamhuri ya watu wa China. Ni kuhamasisha utangazaji wa Injili na kufikia umoja wa jumuiya ya wakatoliki

Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Ujumbe wa Papa Francisko alioutangaza wakati wa kumalizia Katekesi yake tarehe 26 Septemba 2018, unaanza kwa kuwatia moyo wakatoliki wa China ambao anawathibitishia kuwa yeye anawakumbuka kila siku katika sasa zake. Papa Francisko anakumbusha maneno ya Yesu, kama alivyokuwa amekwisha fanya Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI katika barua yake ya tarehe 27 Mei 2007 ya kwamba “Msiogope zizi dogo” (taz Lk 12,32).

Dumbwi la maoni mengi yayounda michanyo na wasiwasi

Katika ujumbe wake, Papa anasema, “ katika kipindi cha mwisho kumekuwa na mzunguko wa sauti nyingi zilizokwenda kinyume na uwepo hasa , wakati ujao wa wakatoliki wa China. Nina utambuzi wa kuwa, dumbwi la maoni na mitazamo, inawezakana ikawa imeunda michanganyo na kufanya mioyo ya wengi kuwa na hisia tofauti.  Kwa wengine wamekuwa na wasiwasi na maswali; wengine wamekuwa na hisia kama vile wameachwa peke yao na Vatican, wakati huohuo hata kutokea maswali mengine yenye kuleta mawazo mabaya juu ya mateso yaliyokabiliwa katika kuishi kwa uaminifu kwa Mfuasi wa Petro. Wengine lakini, wamekuwa na maoni chanya ya matarajio mema  na tafakari linaloongozwa na matumaini ya wakati ujao wa utulivu na wenye kuleta matunda ya ushuhudia imani katika ardhi ya China”. Baba Mtakatifu anathibitisha  kuwa, ni “katika hali hiyo ambayo imewezesha Makubaliano ya muda kati ya Vatican na Jamhuri ya Watu wa China kuhusiana na uteuzi wa Maaskofu, katika saini iliyotiwa hivi karibuni mjini Beinjing.

Shukrani kwa wakatoliki wa China na ushuhudwa wa Injili hadi kutoa maisha

Baba Mtakatifu Francisko , anawasifu kwa dhati Kanisa Katoliki la China kutokana na zawadi ya uwaminifu wa wakatoli wa china, msimamo wao katika majaribu na kujitoa kwa imani katika mema ya Mungu, hata kama matukio mengine yalijionesha kwa namna ya pekee tofauti na ngumu. “Uzoefu wa namna hiyo unatokana na tunu ya kitasaufi ya Kanisa la China na watu wote wa Mungu, mahujaji katika dunia. Bwana kwa njia ya moto wa wa ukarimu , hakosi kamwe kutoa tulizo la faraja na kuwaandalia furaha kubwa zaidi”. Baba Mtakatifu anawaalika watazame mfano wa waamini wengi na wachungaji ambao walitambua kujiotoa na kushuhudia ( Rej 1Tm6,13) Injili hadi kujitoa maisha yao binafsi. Hawa ni wa kufikiria marafiki wa kweli wa Mungu!

Mazungumzo yalianzishwa na Mtakatifu Yohane Paulo II na kufuatia Papa Benedikto XVI

Katika ujumbe huo, pia Baba Mtakatifu anathibitisha kwamba, Mkataba wa muda ni zawadi ya mchakato wa muda mrefu na mgumu wa mazungumzo ya  Vatican na Viongozi wa Serikali ya China, ulioanzishwa na Mtakatifu Yohane Paulo II, na kuendelezwa na Papa mstaafu Benedikto XVI. Kwa njia ya mchakato huo. Vatican haijawa na lolote zaidi na wala kuwa na roho ambayo haiwezi kufikia lengo la kitasaufi na kichungaji kwa Kanisa mahalia, kwa maana ya kusaidia, kuhamasisha kutangaza Injili na kufikia, kuhifadhi kwa ujazo mkuu na kutazama umoja wa Jumuiya ya wakatoliki wa China.

Kwa Imani unatembea bila kujua barabara uelekayo

Baba Mtakatifu,akiendelea na ujumbe huo, anaelekeza juu ya hatua mpya wanayoalikwa kuifuata. Ni safari ambayo anamtaja kwa mara nyingine  tena, Barua ya Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI kwa wakatoliki kwamba hiyo, “inahitaji muda na  matashi mema kwa sehemu zote mbili”. Papa anatoa mfano kwamba wa Ibrahimu ambaye aliitwa na Mungu na kumtii kwa kuanza safari kuelekea mahali ambapo alikuwa hajuhi, na ili aweze kupokea urithi , bila kutambua safari iliyokuwa inafunguka mbele yake. Iwapo Ibrahimu angeweza kuweka vizingiti vya mawazo, kijamii na kisiasa, kabla ya kutoka nje ya nchi yake, labda hasingeweza kusafiri. Ibrahimu  kinyume chake aliweza kuamini Mungu na Neno lake, akaacha nyumba yake na usalama wake.  Haikuwa ni mbadiliko ya kihistoria ya kumwezesha kuamini Mungu tu, bali ilikuwa ni imani safi iliyosababisha mabadiliko ya historia. “ Kama mfuasi wa Petro, Baba Mtakatifu kwa nguvu anaendelea, ninatamani kuthibitisha imani hii (… ) kwa  kuwaalika kufuata daima kiasi kikubwa katika kuweka imani kubwa katika Bwana wa hisotria  na katika kufanya mang’amuzi ya mapenzi yake yaliyotimilizika katika Kanisa”.

Suala ya kuteua maaskofu

“Ilikuwa ni msingi, Papa anaendelea kueleza, kukabiliana, hawali ya yote , masuala ya uteuzi wa Maaskofu. Na kwa wote ninagundua kwa bahati mbaya, historia ya hivi karibuni ya Kanisa Katoliki nchini China, imekuwa na uchungu mkubwa wa mivutano ya kina, majeraha na migawanyiko, iliyovuma hasa katika sura za Maaskofu ambao ndiyo walinzi wa kweli wa imani na wahakiki wa umoja wa Kanisa. Hata hivyo katika nyakati zilizopita, kulikuwapo na ukaguzi wa maisha ya ndani ya jumuiya katoliki, kwa kuwawekea ukaguzi wa moja kwa moja mbali na kuwa na sheria ya madaraka ya serikali, ndani ya   Kanisa la China  ambalo lilijulikana kama la mafichoni.

Naomba Maaskofu waliopatana kujieleza  katika umoja uliopatikana kwa ishara zinazoonekana

Baba Mtakatifu ameonesha pia jinsi gani amepata faraja kubwa, katika kutazama udhati wa matashi ya wakatoliki wa China kuishi kwa imani yao na ujazo wa umoja na Kanisa la ulimwengu, na mfuasi wa Mtakatifu Petro. Wakiwemo maaskofu ambao wamejeruhi umoja wa Kanisa kwasababu ya udhaifu na makosa, lakini hata sio mara chache, wanaokosolewa kwa nje. Kwa maana hiyo baada ya kutathimini kwa makini  kwa kila hali ya mtuna kusikiliza mapendekezo, Baba Mtakatifu anaongeza, nimetafakari, na kusali sana nikitafuta wema wa kweli wa Kanisa la China na mbele ya Bwana na kwa utulivu katika hukumu, kwa mwendelezo wa maelekezo ya wenzangu walionitanguliwa, nimeamua kuwapatia upatanisho, kwa maaskofu saba waliobaki rasmi, ambao waliwekwa wakfu bila ruhusa ya Papa, na baada ya kutazama sheria za Kanisa na kuwaaingiza moja kwa moja katika muungano wa Kanisa. Na kwa wakati huo huo, ninaomba wao wajieleze, kwa haraka ishara za dhati na zinazoonekana, wakati wanajikita katika Umoja wa Vatican na Kanisa lote duniani, kwa kuendelee kuwa waaminifu licha ya matatizo”.

Kukumbatia anayejitambua amekosea

Mwaliko kwa Wakatoliki wote wa China ni ule wa kuwa wasanii wa mapatano, kwa utambuzi kuwa, “hakuna sheria wala kanuni ambayo inaweza kumzuia Mungu hasimkumbatie mwanae, ambaye anarudi kutoka nje mara baada ya kutambua kwamba alikuwa na makosa, lakini ameamua kuanza kwa upya”. Katika roho hiyo, Baba Mtakatifu anathibitisha kuwa “ni wazi inawezekana kuwa mwanzo wa mchakato usiyokuwa wa kawaida, ambao tunatarajia utasaidia kuponya majeraha yaliyopita, kurejesha ushirikiano  kamili wa Wakatoliki wote wa China”.

Nafasi ya wakatoliki nchini China

Nafasi ya Kanisa katoliki nchini China katika Jamii. Katika mpango wa raia na sisasa, Baba Mtakatifu anasema kwa wakatoliki kuwa, wawe wazalendo wema ambao wanaoongozwa na nchi kwa kuihudumia kwa jitihada na ukarimu, kwa mujibu wa uwezo wao. Na kwa upande wa maadili, wawe na utambuzi kuwa, wazalendo wengi wanasubiri  kipimo cha hali ya juu katika hudumu ya wema wa pamoja na maendeleo ya pamoja katika jamii nzima. Kwa namna ya pekee,wakatoliki watoe mchango wa kinabii na ujenzi ambao unavutia imani ya familia ya Mungu.

Maaskofu na mapadre washinde vizingiti kwa ajili ya uinjilishaji

Kwa maaskofu, mapadre, na  watawa wote, Papa anawaomba washinde zaidi vizingiti vya wakati uliopita, katika kutatafuta wema wa  pamoja, ili kuweza kuwasaidia waamini na juhudi kwa unyenyekevu wa mapatano na umoja , wakiongozwa na nguvu shauku ya safari ya uinjilishaji, kama inavyolekeza Mtaguso wa Vatican II.

Wito kwa vijana wakatoliki wa China: kupelekea furaha ya Injili kwa wote

Baba Mtakatifu anawageukia vijana wakatoliki katika ujumbe wake, kwa wito wa kushirikiana katika ujenzi wa wakati ujao wa nchi na kupeleka kwa shauku na furaha Injili kwa wote, kushinda hukumu binafsi na malumbano kati ya makundi na jumuiya. Wafungue kwa ujasiri na udugu katika safari inayongozwa na mwanga wa dhati katika utamaduni wa makutano.

Waamini duniani kote wasiache wakatoliki wa China peke yake

Hata hivyo katika ujumbe wa Papa, anawaomba wakatoliki wote duniani kote kuwasindikiza kwa sala bila ukomo, urafiki kindugu hao kaka na dada wa China. Kwa dhai wao lazima wahisi kuwa katika safari ya wakati huu inafunguliwa kwao lakini hawako peke yao”.

 

26 September 2018, 16:29