Vatican News
Maaskofu kutoka maeneo ya Kimisionari kukutana na Papa Vatican Maaskofu kutoka maeneo ya Kimisionari kukutana na Papa Vatican   (Vatican Media)

Askofu ni mchungaji anayejua kuomba kama Musa kwa ajili ya watu!

Papa Francisko alikutana na Maaskofu kutoka katika maeneo ya Kimisionari, wanaofanya Semina yao hadi tarehe 15 Septemba. Papa akifafanua maana ya nafasi ya Askofu anasema, yeye haishi tena kwa ajili yake, bali kwa ajili ya kutoa maisha kwa ajili ya kondoo, kwa namna ya pekee walio wadhaifu na ambao wako hatarini.

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Wapendwa ndugu maaskofu, ninayo furaha ya kuwakaribisheni katika fursa ya Semina ya mafunzo. Kwa kupitia kwenu ninawasalimia hata jumuiya ambazo mmekabidhiwa ikiwa ni mapadre, watawa kike na kiume, makatekista na waamini walei. Ninanao utambuzi wa  Kardinali Filoni, kwa maneno ambayo mmeyatoa na kumshukuru hata Askofu Mkuu Rugambwa na Dal Toso. Huo ni utangulizi wa hotuba ya Baba Mtakatifu Francisko wakati alipokutana na wajumbe Maaskofu kutoka Mabara manne duniani wanao fanya semina ya mafunzo. Hawa ni maaskofu waliochanguliwa miaka miwili ya mwisho katika daraja la uaskofu, miongoni mwao wapo hata Askofu Anthony Lagwen wa Jimbo Katoliki la  Mbulu na Askofu Baatus Christian Urassa wa Jimbo la Katoliki la Sumbawanga nchini Tanzania.

Askofu ni nani: Akiendelea na hotuba yake, ameuliza je Askofu ni nani? : “Tujiulize utambulisho wa kichungaji  ili kuwa na  utambuzi zaidi, japokuwa Baba Mtakatifu anabanisha kuwa haupo mtindo  wa utambulisho  wenye kiwango sawa mahali popote. Lakini, huduma ya Askofu inatia msisimko, kwa maana ya ukuu wa huduma ambayo anaichukua binafsi. Yeye ameitwa kwa maana hiyo kuwa sawasawa na Mchungaji mwema na kufanya moyo wa kikuhani wa kijisadaka maisha yake yote. Kwa hiyo yeye haishi tena kwa ajili yake, bali kwa ajili ya kutoa maisha kwa ajili ya kondoo, kwa namna ya pekee walio wadhaifu na ambao wako hatarini. Askofu kwa maana hiyo anawakishia usimamizi kwa dhati  wa umati wa ndugu ambao ni kama kondoo wasio kuwa na mchungaji (taz Mk 6,34, na ambao kwa maana nyinyine wamebaguliwa. Kutokana na hilo,Baba Mtakatifu anatoa msisitizo na kuwasihi: “Ninawaomba muwe na ukaribu na maneno kwa namna ya pekee wanaofanya uzoefu wa kuishi mpembezoni na maisha yasiyo ridhisha; zaidi wengi wao wanahitaji kuhisi upendeleo wa Bwana ambao ninyi wenyewe ni mikono ya huruma”.

Askofu ni nani? : “Kwenu ninyi ninataka kelezea  mambo matatu msingi: Askofu ni mtu wa sala, mtu wa kutangaza na mtu wa umojaAskofu ni mtu wa sala: Baba Mtakatifu Francisko akitaka kufafanua zaidi misingi mitatu ya Askofu ni nani amesema: Askofu ni mfuasi wa Mitume na kama mitume walioitwa na Yesu kukaa na Yeye (Mk 3,14). Ni pale anapopata nguvu na imani. Mbele ya Taberkulo anajifunza kujikabidhi na kumwamini Bwana. Na kwa namna hiyo anakomaa katika yeye, ule utambuzi hata wakati wa giza, akiwa amelala, au siku, katika kazi ngumu na kutoa jasho katika shamba anakopalilia, mbegu inakomaa” (taz Mk, 4 26-29). “Sala siyo ibada ya mazoea ya Askofu ya kila siku tu, anaongeza Baba Mtakatifu, bali ni ya lazima; siyo shughuli kati shughuli zilizo nyingi, bali ni uwajibikaji wa uhuduma yao ya  maombi: Yeye analazimika kupeleka kila siku mbele ya Mungu watu na hali halisi. Ni Kama Musa alivyo kuwa akinyosha mikono yake juu kwa ajili ya kuwaombea watu wake (kut 17,8-13) na mwenye uwezo wa kuomba bila kuchoka kwa Bwana ( taz Kut 33,11-14), ni mtu wa  kufanya mchakato na Bwana kama  alivyofanya Ibrahimu, kwa maana ya  maombi yasiyoisha. Maombi bila msisitizo siyo maombi”, Baba Mtakatifu amethibitisha!

Huyo ndiye Mchungaji anayesali! Aliye na ujasiri wa kujadili na Mungu kwa ajili ya zizi lake. Mbunifu katika sala, anashiriki upendo upeo na msalaba wa Bwana wake. Yeye halipwi, bali anatafuta daima kufanana na Yeye katika njia, ili apate kugeuka kuwa kama Yesu dhabihu na altare kwa ajili ya wokovu wa watu wake. Hiyo haitokani na kujua mambo mengi, Baba Mtatifu anafafanua zaidi ya kwamba, ni kutaka kujua kitu kimoja tu kila siku katika sala yaani, Yesu Kristo na Kristo msulibiwa (1 Kor 2,2). Ni rahisi kuvaa msalaba kifuani, lakini Bwana anataka kubeba vizuri msalaba mzito nyuma ya mabega na katika moyo: kwa hiyo anataka tushikirikishane msalaba wake. Papa anaongeza mfano kuwa: Petro alipowaeleza waamini ni kitu gani walipaswa kufanya mashemasi wale alio kuwa muda mfupi amewachagua, aliwambia kwamba: ni sala na kutangaza Neno. Nafasi ya kwanza ni sala; na hiyo inawahusu hata maaskofu wote, Baba Mtakatifu anasisitiza na kuongeza kusema: mara nyingi anapendelea kuuliza kila Askofu, je ni masaa mangapi anasali kila siku?

Askofu ni Mtu wa kutangaza: Akifafanua anasema,Wafuasi kama Mitume, kama maaskofu wanatambua kwa dhati juu ya utume ambao Yesu aliwapatia: Nendeni  mkatangaze Injili ( Mk 16,15). Nendeni: Injili haitangazwi ukiwa umekaa, bali ukiwa katika mwendo. Askofu hakai katika ofisi, kama vile meneja wa kampuni, badala yake yupo katikati ya watu, katika barabara za ulimwengu kama Yesu. Anampeleka Bwana wake mahali ambapo hajajulikani mahali ambapo hatambuliki na kuteseswa. Naye akijitoa ndani yake binafsi, anajifahamu zaidi. Yeye haipendi faraja, haipendi maisha ya utulivu na hajihurumii nguvu zake, hajisikii kama mfalme, anafanya kazi kwa ajili ya wengine, hujiachia kwa uaminifu wa Mungu. Na kama anajaribu kutafuta sifa na uhakikisho wa kidunia, yeye hawezi kuwa mtume wa kweli wa Injili.

Je ni  mtindo  gani wa kutangaza?  Ni kushuhudia kwa unyenyekevu wa upendo wa Mungu, kama alivyo fanya Yesu ambaye kwa ajili ya upendo alijinyenyekeza. Hata hivyo Baba Mtakatifu Francisko amebainisha kuwa,  kutangaza Injili kunaleta wakati mwingine vishawishi vya  kutaka kujulikana na madaraka, kujisikia na kutaka sifa, za kidunia. Kutokana na hili ametoa onyo ya kuwa na tahadhali ya malimwengu! Daima kuna hatari ya kutaka kubadili dhana halisi na kuifanya kuwa wadau zaidi ya kuwa mashihidi kwa  kuchakachua Neno la wokovu katika kupendekeza Injili isiyo na Yesu Msulibiwa na mfufuka. Lakini kwa upande wao anasisitiza kwamba, wameitwa kuwa kumbukumbu hai ya Bwana, ili kukumbusha wote ya kwamba Kanisa linatangaza maana ya kutoa maisha bila kipimo na kuwa tayari hata kwa kukubali sadaka ya kujitoa maisha binafsi.

Askofu  ni mtu wa muungano: Askofu hawezi kuwa na vipawa vyote;  yaani upamoja wa karama, lakini wengine wanajidai kuwa navyo vyote, Baba Mtakatifu kwa masikitiko anaongeza, maskini! Lakini Askofu ameitwa kuwa na karama ya upamoja. Kwa maana ya kuhakikisha unakuwapo umoja na kudumisha muungano. Kanisa linahitaji muungano lakini usiwe ule wa nje ya kawaida au wa kiongozi anayepambana binafsi. Mchungaji anakusanya: Askofu kwa waamini wake ni mkristo na waamini wake. Hatangazwi katika magazeti, hatafuti sifa ya kujulikana duniani. Yeye hana nia ya kulinda jina lake liwe zuri, lakini yeye anapenda kuinua na kukuza  muungano kwa kuhusika akiwa mstari wa mbele na kutenda kwa dhati. Hateseki kusikia kuwa yeye siyo  kiongozi wa mstari wa mbele,  lakini yeye anaishi amesimika mizizi katika eneo hilo, kwa kuvikataa vishawishi vya  kuondoka mara kwa mara kwenda mbali na jimbo lake.

Askofu hachoki kusikiliza: Askofu ni yule ambaye hashikilii juu ya mipango ya kufanya mezani, lakini anaacha atumwe na sauti ya Roho, ambayo inapenda kuzungumza kwa njia ya imani na watu rahisi. Anahangaika kuwa na kitu kimoja na watu wake na zaidi makuhani wake, daima ni tayari kuwapokea na kuwatia moyo mapadre wake. Anahamasisha kwa mifano zaidi ya maneno na undugu wa kweli wa makuhani na mapadre, kuwaonesha kuwa ni Mchungaji wa zizi na si kwa sababu ya sifa au nafasi kazi, jambo ambalo ni baya sana Baba Mtakatifu amebainisha! Msiwe wapandaji na wala wenye tamaa, tafadhali, Baba Mtakatifu amewahimiza, walakini wachunge zizi la Mungu na wasiwatawale kwa mabavu hao waliowekwa chini ya ulinzi wao bali wawe mfano kwa hilo kundi (taz 1Pt 5,3). Ameongeza kuwaonya wahepuke ule uklero: kwa maana ya mtindo usio hitajika wa kupenda madaraka katika Kanisa na ambao anathibitisha umeonekana katika jumuiya kadhaa na pamekuwa na mienendo ya manyanyaso, kama vile madaraka, ya dhamiri na manyanyaso ya kingono. Kupenda madaraka ya kikuhani, yanaharibu umoja na kuzua uhasi wa mwili wa Kanisa ambao unatoa msingi na kusaidia kushitaki mabaya mengi ambayo leo hii yapo. Kusema hapana kuhusu madaraka, dhamiri na kila aina ya manyanyaso, maana yake ni kusema kwa nguvu zote hapana kwa kila aina yoyote ya kupenda ukuu. ( taz barua ya Watu wa Mungu , 20, Agosti 2018.

Kwa njia hiyo Baba Mtakatifu ameongeza kusema, wao wasijisikie mabwana wa zizi, kwa maana wao siyo mabwana wa zizi, hata kama wengine wanaweza kuwa au kama ilivyo kawaida katika sehemu nyingine. Watu wa Mungu ambao wao wamewekwa wakfu kwa jili yao, ni Baba, na siyo mabwana; Hao ni baba waangalifu: hakuna yoyote ajionesha kuwa na hali ya kuwa chini. Anaongeza kusisitiza: Katika hali hii ya kihistoria ya tabia fulani ya “uongozi” inaonekana kuwa imeongezeka katika sehemu mbalimbali. Kujionesha wenye nguvu ambao unaweka umbali na kuamrisha wengine inaweza kuonekana vizuri na yenye kupendeza, lakini sio ya kiinjili. Mara nyingi uharibu na uharibifu  usio wezs kuunda zizi ambalo Kristo alitoa maisha yake kwa upendo upeo, kwa kujinyeneyekeza na kuhangamia binafsi. Kwa njia hiyo “kuweni watu maskini wa mali na matajiri wa uhusiano, kamwe msiwe wagumu na waopendelea ugomvi, lakini rahisi wenye subira na wawazi”, amesema Baba Mtakatifu.

Baba Mtakatifu aidhaa amewaomba moyoni mwao waweke hasa katika baadhi ya mambo halisi: Kwanza katika Familia:  Akifafanua amesema familia  pamoja na kubobea katika utamaduni ambao unaonesha dhana ya muda mfupi na kuhamasisha   marupurupu ya haki za kibinafsi, bado hubakia kiungo cha kwanza cha kila jamii na Makanisa ya kwanza, kwa sababu ni makanisa ya nyumbani. Kwa maana hiyo amewaomba wakuze mchakato wa maandalizi kwa ajili ya ndoa na kuwasindikiza wanafamilia. Semina hizo zitatoa matunda  kwa wakati wake anasisitiza! Watetee maisha ambayo bado hayajazaliwa na kama ilivyo kwa wazee, kuwasaidia wazazi na babu na wajukuu katika utume wao wa kimisionari. Pili amesema: Waseminari: wao ni vioto vya kesho, wakati maaskofu  pale seminarini wanapaswa kuwa ndiyo nyumbani kwao. Baba Mtakatifu amewataka maaskofu wahakikishe kwa umakini wanao waongoza ni watu wa Mungu, walimu wenye uwezo na wakovavu ambao kwa msaada wa sayansi iliyo bora ya kibinadamu inayo hakikisha mafunzo  katika mstari mnyoofu, uliofunguliwa, wa dhati na kweli. Watoe kipaumbele katika mang’amauzi ya miito kwa ajili ya kuwasaidia vijana watambue sauti ya Mungu kati ya sauti nyingi zinazodunda katika masikio na moyoni.

Vijana: Baba Mtakatifu anasema Sinodi ijayo ambayo ni kwa ajili ya vijana, wote watajiweka katika kusikiliza na kuacha nafasi ya kusikiliza shauku, wasiwasi mapendekezo na kipeo chao. Wao ni maisha endelevu ya Kanisa na uendelevu wa jamii, na dunia iliyo bora inategemea wao. Hata kama inaonekana matokeo ya virus vya kushambulia katika ufujaji wa mali ovyo, ukosefu wa imani, lakini ni vema kutowaweka pembezoni. Baba Mtakatifu ameshauri,maaskofu  kwenda kuwatafuta na kuhisi kuwa wapo rohoni mwao kwa sababu moyo wao utaendelea kuomba maisha na uhuru. Kwa njia hiyo ni kuwapa nafasi tena kwao ya kuwapatia Injili kwa ujasiri.

Maskini: Kuwapenda maana yake ni kupambana dhidi ya umaskini, kiroho na mali. Baba Mtakatifu amewashauri maaskofu kutumia muda wao na nguvu zao kwa watu walio wa mwisho, bila kuogopa kuchafua mikono yao. Kama mitume wa upendo, wawafikie mahalia walipo yaani pembezoni mwa ubinadamu na kuwasaidia katika majimbo yao. Na hatimaye amemalizia akiwaomba maaskofu wasiwe na ubaridi, kwa maana amesema ubaridi huo,hupelekea hali ya kutokuwa wema na uvivu. Jihadharini na hilo. Jihadharini na utulivu unaoondolea kujisadaka kama  dhabihu; jihadharini na haraka ya kichungaji ambayo huleta mateso ya kuvumiliana; wahepuke kuwa na wingi wa mali ambayo inaondoa sura ya Injili na mwisho:  wasisahau kwamba shetani huingia kwenye mifuko yake!

08 September 2018, 15:13