Cerca

Vatican News
Nembo tatu za Ziara ya kitume ya Papa katika nchi ya Latvia, Lithuania na Estonia Septemba 2018 Nembo tatu za Ziara ya kitume ya Papa katika nchi ya Latvia, Lithuania na Estonia Septemba 2018 

Ziara ya kitume ya Papa iwe chini ya ulinzi wa Mama Maria

Katika ujumbe kwa wakatoliki nchini Estonia, Msimamizi wa Kitume wa nchi za Ulaya Mashariki, Monsinyo Jourdan anatuma ujumbe wake ili kuwaalika waamini washiriki kwa wingi katika ziara ya kitume za Baba Mtakatifu Francisko mwezi Septemba, kusali Rosari na kutoa sadaka hasa ya kufunga kwa siku moja kwa ajili ya ufanisi wa tukio hilo !

Sr. Angela Rwezaula - Vatican.

Katika ziara ya Kitume ya Baba Mtakatifu Francisko nchini Lithuania, Latvia na Estonia inayotarajiwa kufanyika kuanzia tarehe 22 hadi 25 Septemba ijayo, Msimamizi wa Kitume wa Estonia, Askofu Mkuu Philppe Jourdan, ametuma Ujumbe kwa wakatoliki wa nchi za Ulaya Mashariki, kuwashukuru kwa kile ambacho wanajikita na ili kuweza kufanikisha tukio la ziara hiyo na kuzidi kuwaomba wasali zaidi ili matunda mema yaweze kupatikana.

Kila maandalizi yafanywe kwa upendo

“Kila tukio kubwa la maelfu ya mambo mengi hata kwa ajili ya madogo zaidi yana maana yake kuu, tufanya shughuli hiyo kwa upendo kwa maana  kama kuna upendo mdogo, shughuli hiyo ugeuka isiyokuwa na maana lakini kama kuna upendo mkuu hata katika matendo yaliyo madogo hugeuka kuwa ya maana iliyo kuu”. Amethibitisha Msimamizi wa Kitume nchini Estonia na kusisitizia  juu ya umuhimu wa kuaandaa zana na vifaa lakini zaidi ya hayo ni kujiandaa kiroho. Katika mchakato wa kihistoria, anaandikia, wakristo walikuwa wakijandalia matuki makubwa kwa kusali na kufunga. Ziara ya Papa kwa hakika ni tukio muhimu kwa ajili ya Kanisa la Eastonia na kwa kila mkatoliki binafsi. Kwa maana hiyo, kutokana na ziara sasa kukaribia, nia yake ni kuwaomba wote wajiandae kikamilifu na kwa kina zaidi.

Kufunga na kusali.

Katika mwezi wa Agosti, unajieleza na sikukuu za Mama Maria na hivyo,Askofu Mkuu Jourdan anaomba kwa namna ya pekee waamini wakatoliki kusali Rosari ili kuweza kufanikisha  ziara ya Baba Mtakatifu na kuheshimu tarehe za kufunga angala kwa ajili ya lengo lilelile Kwa kufanya hivyo amependekeza iwe siku ya Jumamosi ya tarehe Mosi Septemba 2018.

Katika Ujumbe wake, Askofu Mkuu Philppe Jourdan anahitimisha akiwatia moyo pia wa kuweza kijiandikisha kwa wingi katika Misa Tatakifu ya  Baba Mtakatifu itakayofanyika katika  Uwanjawa mkubwa wa Uhuru au katika mkutano mwingine wa vijana katika Kanisa la Mtakatifu Caroli huko Tallinn kwa kupitia katika ukurasa wa mtandao wao: https://paavsteestis.ee/, mahali ambapo pia wanaweza kupata maelezo kamili ya lazima kuhusiana na maandalizi hayo na ziara ya Papa Francisko Septemba 22 -25 Septemba 2018.

18 August 2018, 09:55