Cerca

Vatican News
Vijana Katoliki nchini Italia wakiwa uwanja wa Mtakatifu Petro Vijana nchini Italia wakiwa uwanja wa Mtakatifu Petro  (AFP or licensors)

Yahitaji uvumilivu kufanya kazi na vijana

Baba Mtakatifu akizungumza kuhusiana na Siku ya vijana kutoka majimbo katoliki ya Italia waliofika na kufanya mkesha naye Jumamosi 11 Agosti 2018 katika uwanja wa Circo Massimo mjini Roma amesema, katika siku hizi wameweza kuzunguka barabara za Roma kwa shauku yao na imani yao.

Sr. Angela Rwezaula - Vatican 

Ninatoa salamu kwa wote, watu wa Roma na mahujaji wanaotoka pande mbalimbali za dunia. Kwa namna ya pekee vijana kutoka majimbo katoliki ya Italia, walio sindikizwa na maaskofu wao, mapadre na viongozi wao. Ni Meneno ya utangulizi wa  Baba Mtakatifu Francisko mara baada ya sala ya Malaika wa Bwana Jumapili 12 Agosti 2018 katika viwanja vya Mtakatifu Petro mjini Vatican kwa waamini na mahujaji waliofika kusali naye katika siku hii Takatifu.

Baba Mtakatifu akiendelea kuhusiana na Siku ya vijana kutoka majimbo katoliki ya Italia waliofika na kufanya mkesha naye Jumamosi 11 Agosti 2018  katika uwanja wa Circo Massimo  mjini Roma amesema, katika siku hizi wameweza kuzunguka katika barabara za Roma kwa shauku yao na imani yao. Anawashukuru kwa uwepo wao na ushuhuda wao kikristo!

Aidha amekumbuka kwamba, Jumamosi 11 Agosti  jioni wakati wa mkesha wakati wa  kutoa shukrani, alisahau kutoa neno moja kwa mapadre, kwa maana hiyo, anawashukuru kwa kazi yao wanayojikita kila siku, anawashukuru kwa uvumilivu wao, kwasababu ameongeza kusema, inahitaji moyo kufanya kazi na vijana! Kwa maana hiyo amezidi kuwashukuru sana mapadre kwa uvumilivu wao. Vilevile amethibitisha kuwa aliwaona hata watawa wanaofanya kazi na vijana na hivyo shukrani kubwa imewandea hata wao!

Kadhalika Baba Mtakatifu Francisko ametoa shukrani kubwa kwa Baraza la Maaskofu wa Italia waliokuwapo na kwa kuwakilishwa na Kardinali Gualtiero Bassetti Rais wa Baraza hilo ambaye amehamasisha Siki hiyo ya Vijana wa Italia ambao wanafanya maandalizi ya Sinodi  ijayo ya Maaskofu, inayotarajiwa hivi karibuni mwezi wa kumi. Na kwa wote amewatakia Jumapili  njema pia safari njema ya kurudi makwao, lakini wasisahau kusali kwa ajili yake!

 

13 August 2018, 13:38