Cerca

Vatican News
Papa akiwa na vijana wakati wa Mkutano wa Siku ya Vijana duniani huko Poland Papa akiwa na vijana wakati wa Mkutano wa Siku ya Vijana duniani huko Poland  (Vatican Media)

Vijana wa Poland wahimizwa kuiga mfano wa Mtakatifu Stanslaus!

Papa Francisko ametuma ujumb, hasa kwa namna ya pekee akiwalenga vijana. Ujumbe wake unasema, Mtakatifu Stanslaus awafundishe wasiwe na hofu ya kujihatarisha na ndoto zao za furaha, kwa maana kisima cha uhakika ni Yesu Kristo. Yesu ni Bwana dhidi ya hatari. Ni Bwana daima na zaidi ya yote !

Sr. Angela Rwezaula - Vatican 

Vijana wapendwa muwe wajasiri: maana Dunia inahitaji ndoto za roho zenu zenye uhuru, mtazamo wenu wa matumani juu ya wakati endelevu na kisima cha chemi chemi ya kweli, wema na uzuri. Hayo ndiyo maelezo yaliyomo katika ujumbe wa Baba Mtakatifu Francisko alio ulekeza kwa Askofu Piotr Libera, wa jimbo la Płock nchini Poland, wakati wa fursa ya kuadhimisha maika 450 tangu kifo cha Mtakatifu Stanslaus Kostka nchini Poland.  Maadhimisho hayo yalifanyika tarehe 15 Agosti 2018.

Mtakatifu huyo alikuwa ni mwanafunzi na novizi wa Kijesuit mjini Roma, na mauti yalimjia akiwa na umri wa 18 kutokana na ugonjwa mbaya. Mtakatifu Stanslaus ni moja ya watoto maarufu katika nchi yao na katika Shurika la Wajesuit anathitisha Baba Mtakatifu!

Uhuru siyo kupiga mbio kuelekea upofu.

Leo hii ni sikukuu ya Kupalizwa Bikira Maria mbinguni na ikiwa ni kumbukumbu ya miaka 450 ya kifo cha  Mtakatifu Stansalus Kostka. Katika kumbukumbu ya utukufu wake wa kuingi katika Utukufu wa Bwana, Baba Mtakatifu anapedana akuungana nao katika sala na kushukuru waamini wa Jimbo la Plock na Kanisa zima la Poland, ambao kwa muda muda huo mfupi huko Rostkowo mahali alipozaliwa Mtakatifu walikuwa waadhimishe Ibada kuu Misa  ya kufunga   mwaka wa Jubieli iliyokuwa imetolewa kwa heshima yake Mtakatifu huyo.

Baba Mtakatifu Francisko akiendelea na ujumbe wake kuwalenga vijana ambao katika nchi hiyo, Mtakatifu Stanslaus ndiye msimamizi wao, anasisitizia juu ya sentensi ya Mtakatifu Yohane Paulo II, aliyotamka katika Kanisa la Mtakatifu Andrea akiwa anatoa heshima ya masalia yake kuwa: “ Safari yake ya maisha ilikuwa fupi iliyo anzia huko  Rostkowo katika Mazowsze na kupitia  Vienna hadi kufikia Roma, safari  hiyo inawezekana kufafananisha na mbio kubwa kupitia katika kambi kuelekea mwisho wa maisha ya  kila mkristo ambayo ni utakatifu (13 Novemba 1988)

Papa Francisko anasema:Wapendwa vijana, wengi wenu mwezi Septemba mtafanya hija kwa miguu kuelekea Przasnysz huko Rostkowo mahali ambapo mtakatifu alizaliwa na alibatizwa . Hiyo ina maana ya hatua ya mbio ya mtakatifu Stanslaus kuekea utakatifu. Anawatia moyo na kuwakumbusha kuwa wakati wa msafara huo kwa miguu katika barabara zote na hata za kila siku ya maisha yao, wao wanao uwezo wa kutimiza mbio! Ndiyo hata wao kwa msukumo wa upendo wa Kristo na nguvu za neema. Kwa mfano wake, awafundishe kuwa uhuru siyo kupiga mbiu kuelekea upofu, badala yake ni uwezo wa kung’amua hatma ya maisha na kufuata njia zilizo bora za mwenendo na maisha. Yeye awafaundishe kutafuta daima hawali ya yote urafiki na Yesu; kusoma na kutafakari neno na kupokea ekaristi takatifu ya uwepo wake hai wa huruma na nguvu, ili kuweze kuvumulia na kutojiachia mikononi mwa kasumba za malimwengu

Yesu anataka mikono yao kuendela kujenga ulimwengu wa sasa. Yeye nataka kujenga ulimwengu huo na vijana (Hotuba ya Siku ya Vijana krakow 30 Julai 2016). Mtakatifu Stanslaus awasimaie na kuwafanya wendeleze kauli yake mbiu isemayo “Ad maiora natus sum” – yaani, nimezaliwa kwa ajili ya mambo yaliyo makuu. Akihitimisha ujumbe huo anamlenga askofu wa jimbo ya kuwa, kwa maombezi ya Mtakatifu Stanslaus Kostka, anawaombea ulinzi wa Mungu juu yao na maaskofu wote, mapadre, waamini na zaidi juu ya vijana wa Kanisa la Poland. Anaomba pia wasali kwa ajili yake na kuwabariki kwa jina la Baba na Bwana na Roho Mtakatifu.

 

16 August 2018, 09:43