Tafuta

Mkutano Mkuu wa Waoblati wa Mtakatifu Yosefu Mkutano Mkuu wa Waoblati wa Mtakatifu Yosefu  

Papa:Waoblati waige unyenyekevu wa Mt. Yosefu wa Nazareth!

Papa Francisko akizungumza na Watawa Waoblati amesema: Mkutano Mkuu wa Shirika la Kitawa ni moja ya kipindi maalum cha neema, kwa wanashirika na jumuiya zake, lakini mbali na hiyo hata kwa ajili ya Kanisa, parokia, familia, vyama vya kitume vya walei na kwa namna nyingi wanao shirikishana tasaufi ya shirika.

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Ndugu wapendwa habari za asubuhi, ninampenda Mtakatifu Yosefu, ana nguvu nyingi! Ni zaidi ya miaka 40 ninasali sala yake niliyo ikutana katika Misale ya kizamani ya kifaransa inayoelezea juu ya Mtakatifu Yosefu .... “ dont la puissance sait rendre possibles les choses impossibles” . Nguvu ya Mtakatifu Yosefu, kamwe haijawahi kusema hapana . Ni lazima kuwa na ujasiri huo.

Ninayo furaha kubwa kukutana nanyi katika fursa ya Mkutano wenu Mkuu na ninawakaribisheni. Wazo kuu kwa namna ya pekee ni kumwendea Padre Jan Pelczarski, aliyechaguliwa hivi karibuni kuwa Mkuu wa Shirika , kama vile, baraza lote la washauri ninawatakia matashi mema ya utume mpya. Wakati huohuo ninao hata utambuzi wa Padre Michelle Piscopo aliyeng’atuka katika uongozi na ambaye ameonesha ukarimu katika  huduma  ya kuongoza shirika. Kadhalika hisia zangu za upendo ziwafikie wanafamilia nzima ya watawa na wawakilishi wa mkutano mkuu, nikiwatia moyo wote kuwa na uvumilivu katika mantiki zote za kitume.

Hayo ndiyo mawazo yake ya kwanza ya Baba Mtakatifu Francisko aliyo anza nayo tarehe 31 Agosti 2018, alipokutana na wajumbe wawakilishi wa Mkutano wa Shirika la wa Oblati wa Mtakatifu Yosefu ( kwa jina jingine wanaitwa wayosefu wa Asti)

Mfano wa kuigwa wa Mtakatifu Yosefu wa Nazareth

Akiendelea na hotuba yake amesema: Mkutano Mkuu wa Shirika la Kitawa ni moja ya  kipindi maalumu cha neema, kwa wanashirika na jumuiya zake, lakini mbali na hiyo hata kwa ajili ya Kanisa, parokia, familia, vyama vya kitume vya walei na kwa namna nyingi wanao shirikishana nao tasaufi yao. Utume ambao wameonesha ni  kutoka kwa mwanzilishi wao Mtakatifu Yosefu Marello, ambao unajionesha kwa dhati katika kujitoa maisha na katika utume wa mawazo ya kuroa huduma kama alivyoishi Mtakatifu Yosefu wa Nazareth. Kuanzia kuiga mfano wake wa maisha ya undani, unyenyekevu na kazi. Yeye aliishi kwa uaminifu na urahisi wa wito wa kulinda Mama Maria na Yesu. Alikuwa karibu na mchumba wake wakati wa furaha, hata nyakati ngumu na yeye alidumisha familia ya kiajabu na Yesu ambaye aliendelea kukua chini ya ulinzi wa macho yake.

Utajiri wa wepesi na kazi ya mtatifu Yosefu.

Katika kuishi utajiri mwepesi wa kazi ya Mtakatifu Yosefu, Baba Mtakatifu anawanaalika kuwa katika ulimwengu shuhuda wa ujumbe wa kweli, wa faraja ya Neno jema: kwa maana Mungu anahudumia wote, hasa upendeleo kwa walio wadogo , wapotevu na ili kuweza kusimika na kuufanya ufalme wa Mungu ukue.

Maratajio ya kuhudumua Yesu katika Kanisa lale  na ndugu kwa namna ya pekee umakini kwa vijana na walio wanyenyekevu unaweza kweli kuwa mhuri wa maisha na furaha yao. Baba Mtakatifu amewakumbusha maneno ya Mwanzilishi wao wa shirika na kwamba maneno hayo hadi sasa bado uanahitajikwa kwa maana maskini katuka mahospitali ya magonjwa sugu, kama mapadre wadogo bado wanayo nafasi nying, na ndiyo maana Bwana anahudumiwa kwa njia yao na kwa ajili ya wema wa roho za wengi. “Semeni kuwa sisi ni watumishi wasio kuwa na faida lakini pia kuweni sehemu ya mapenzi ya Mungu kwa njia ya yule mnaye mwakilisha, na siku hadi siku mnafundishwa. Katika matendo yao, ndipo waone matunda ambayo yawezesha kusifu na kumtukuza Mungu aliye mbinguni (Barua ya Mtakati Yosefu Marello n. 241)

Joseph Marello

 Baba Mtakatifu anawatia moyo ili kuendelea kufanya kazi ndani ya Kanisa na ulimwengu kwa karama  rahisi na msingi  kama zile za mchumba wake Bikira Maria, kama vile  unyenyekevu ambao unavutia wema wa Baba; kuwa na moyo wa kina na Bwana, ambaye anafanya kila kitu cha kikristo:kuwa wakimya na wanaojificha katika kuungana kwa kina na kazi kwa ajili ya mapenzi ya Bwana, katika roho ya  moto wa Mwanzilishi wao Marello isemayo ( ninyi ni certosini katika nyumba, na mitume nje ya nyumba”) . Haya ni mafunsisho ambayo daima yaishi katika roho zao na kujikita kwa wote ndugu, kaka katika kudumisha ndani ya nyumba na jumuiya yao ile roho ya makaribisho, sala na ukimya, wakati huo huo na fursa ya mikutano ya kujumuiya. Roho ya familia inajengwa na ule msingi wa umoja katika jumuiya na kwa shirika zima.

Mtakatifu Yosefu Marello alikuwa akiwashauri watoto wake kiroho kuwa sehemu ya kwanza ya upendo na utii katika mafundisho na maelekezo ya papa. Nyakati zile zilikuwa ni zinapitia kipindi cha mateso ya kiroho; kwa maa hiyo Baba Mtakatifu anasema hata nyakati zetu, suala hili linapaswa kutiliwa mkazo katika kujenga imani na kuondoa maana potofu ya imani kikristo.

Na kutokana na hilyo anasisitiza kuwa mwanzilishi wao hajachoka hata leo hii kuwatuma wawe shuhuda wa upendo na imani kwa Kristo na katika Kanisa lake. Wao wanapaswa kwa watu wa kila kona ya dunia kwa namna ya pekee kwa vijana na ambao sehemu kubwa ya utume kama shirika  wajikita na hivyo wawafundishe kwa njia ya maisha na maneno, kama alivyo fanya Mtakatifu Yosefu wa Nazareth,aliyejiweka wakfu katika hudumia Yesu  na hasa ndiyo nia kuu rahisi na hakika ya kutimikia kwa ukamilfu furaha na maisha ya wito.

Ushuhuda kwa vijana

Mbele ya utamaduni wa kijuu ambao unatokana na kutafuta mali kwa njia za mkato zenye hatari, Baba Mtakatifu anawasihi wasikose kuhamasisha vijana katika kuinjilisha kiroho, na kuwafundisha ili wakomae na kuwa na uwezo wa nguvu , lakini pia  wawe hata na  ule ukarimu. Furaha kubwa zaidi ni kuongea na vijana wa Yesu Kristo, kusoma nao Injili na kukabiliana maisha pamoja…amekazia Baba Mtakatifu!

Hiyo ndiyo njia bora Baba Mtakatifu na kusisitiza ya kujenga wakati endelevu wenye msimamamo. Na kwa maombezi ya Mtakatifu Yosefu, Msimamizi wa Kanisa ulimwenguni, kwa ajili ya mwanzilishi wao, waweze kuzaa matunda ya kazi ya mkutano wao Mkuu. Asimamie utume wao katika Familia ya Marelliana: Waoblati wa Kike na Kiume, walei wambao wanashiirikishana nao tasaufi yao. Amewabariki na kuomba sala kwa ajili yake.

31 August 2018, 14:47