Tafuta

Vatican News
Katika Katekesi ya Baba Mtakatifu amekumbusha siku ya kuombea huduma ya viumbe Katika Katekesi ya Baba Mtakatifu amekumbusha siku ya kuombea huduma ya viumbe   (Vatican Media)

Papa:Mosi Septemba ni siku ya Dunia ya kuombea huduma ya viumbe!

Mara baada ya Katekesi yake, Baba Mtakatifu Francisko, amekumbuka Siku ya IV ya Maombi ya dunia kwa ajili ya viumbe ambayo itaadhimishwa Jumamosi 1 Septemba na kusisitiza juu ya suala la maji.

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Baba Mtakatifu Francisko amkumbusha kuwa Jumamosi tarehe 1 Septemba ni Siku ya IV ya Dunia ya kuombea huduma kwa viumbe. Ametamka hayo mara baada ya kumaliza katekesi yake kwa waamini na mahujaji wote waliofika katika kiwanja cha Mtakatifu Petro Mjini Vatican tarehe 29 Agosti 2018. Baba Mtakatifu amesema, katika hitimisho la Katekesi hii tuadhimishe kwa umoja na ndugu kaka na dada wa Kiorthodox na makanisa mengine na jumuiya ya kikristo.

Katika ujumbe wa mwaka huu, ninapenda kuwaalika kuwa na umakini juu ya suala la maji, wema msingi wa kulindwa na kujikita kwake kwa pamoja. Ninawapongeza kwa shukrani kubwa kuanzishwa katika sehemu mbalimbali za makanisa kwa namna ya pekee katika taasisi za maisha ya kitawa, na ushiriki mwingi wa makanisa ambao wamekuwa tayari kujikita katika suala hili. Ninawaalika wote kuungana kwa sala Jumamosi kwa ajili ya nyumba yetu ya pamoja na kuilinda nyumba yetu ya pamoja.

Ikumbukwe Papa Francisko, siku hii alizindua kwa mara ya kwanza Siku ya Dunia ya Sala ya Kuombea Huduma kwa viumbe, kunako tarehe 1 Septemba 2015 kwa mujibu wa barua yake aliyochapishwa tarehe 6 Agosti 2015. Katika barua hiyo, Papa Francisco alilihimiza Kanisa Katoliki kuungana na Mkuu wa Kanisa la Kiekumeni la Kiotodosi, Patriaki Bartholomayo I, ambaye kwa namna ya kipekee ameonyesha kujalimustakabali wa viumbe hai.  Kulingana na Waraka" Sifa kwa Bwana kwa ajili ya utunzaji wa dunia makazi ya wote” Laudato Si, Papa alitangaza maamuzi yake ya kuanzisha katika Kanisa Katoliki, Siku ya Maombi kwaajili ya kujali huduma kwa  viumbe Dunia, tarehe mosi Septemba. Tarehe ambamo Kanisa la Kirthodox imekuwa ni desturi ya kuombea viumbe kwa miaka kadhaa sasa.

Waraka wa Baba Mtakatifu ulitaja madhumuni ya Siku ya Dunia ya kuombea huduma kwa viumbe, kuwa ni kutoa muda kwa waamini, kwa mtu binafsi na jamii kw ujumla, nafasi ya kufaa kuthibitisha wito binafsi wa kuwa mawakili wa viumbe na  kumshukuru Mungu kwa kazi ya ajabu ya  mikono yake,  ambayo aliikabidhi chini ya huduma ya binadamu. Hivyo siku hiyo ya sala ya kuombea kujali huduma kwa viumbe, pia inatuhimiza kutafuta msaada wa Mungu kwa ajili ya ulinzi wa viumbe, na vile vile kuomba msamaha wake kwa dhambi tulizofanya dhidi dunia ambayo ni makazi ya viumbe wote. Aidha Papa anafurahi kwamba, maadhimisho ya siku hiyo, yanakwenda sambasamba na desturi ya Kanisa la Kiorthodox na hivyo inakuwa ni fursa ya thamani kubwa, kama tukio jingine linaloshuhudia mpanuko wa umoja wa Wakatoliki na Waorthodox kama ndugu moja.

Kadhalika Barua ya Baba Mtakatifu Francisco alieleza na kuonya kwamba, tunakiishi kipindi hiki  ambamo Wakristo wanapambanishwa na changamoto nyingi katika kufanya maamuzi thabiti. Na hivyo inakuwa ni lazima kwa kila Mkristo, kufanya kila jitihada, katika utoaji wa jibu la pamoja, nzitothabiti la kuaminika na ufanisii zaidi.

Papa alionyesha tumaini lake kwamba, katika siku hii, pia Makanisa mengine na Jumuiya za kikanisa, zitashiriki katika Ibada hii, kama ilivyoshauriwa na Baraza la Makanisa Duniani. Barua hiyo pia inawahimiza watu wote ikisema kwamba: kama mtu binafsi, au kama taasisi, au kama jamii ya watu, tunahitaji mabadiliko ya moyo kwa ajili ya kuhifadhi na kulinda sayari ya dunia kwa watoto wetu na vizazi ambavyo bado kuzaliwa. Kwa hiyo, Barua ya Baba Mtakatifu Francisko inahimiza Tume za Liturujia za kanisa Katoliki, kukiingiza kipengere hiki katika maombi ya ibada kwa ajili ya kutoa msisitizo katika wajibu binadamu kulinda viumbe wote wa Mungu na kwa Maadhimisho ya Sikukuu kwa Mtakatifu Francis na Mtakatifu Isidore.

29 August 2018, 15:31