Tafuta

Vatican News
Baba Mtakatifu ametuma barua yake kwa wajumbe wa Sinodi ya  Wametodisti na wavaldese Baba Mtakatifu ametuma barua yake kwa wajumbe wa Sinodi ya Wametodisti na wavaldese  (ANSA)

Papa:Kuweni mashuhuda wa upendo kwa ajili ya Razaro wako wengi!

Papa Francisko ametuma barua ya matashi mema ya Sinodi ya makanisa ya Wametodisti na Wavaldese katika fursa ya Sinodi yao ya kila Mwaka. Kutangaza kwa upendo na kusali kwa pamoja kwa ajili ya umoja kamili ndiyo kiini cha ujumbe wake Baba Mtakatifu Francisko!

Sr.Angela Rwezaula - Vatican 

Katika barua yake  kwa  Sinodi ya makanisa ya Wametodisti na Wavaldese katika fursa ya Sinodi yao ya kila  mwaka, anaanza na salam ya kindugu na kuonesha shauku yake ya kuwatumia ujumbe katika tukio hilo. “Ninataka kuonesha ukaribu wangu wa kindugu kwa niaba ya Kanisa Katoliki na binafsi ameandika Baba Mtakatifu na kisisitiza kuwa, “anawahakikishia kuwakumbuka katika maombi, hasa kumshukuru Bwana kwa zawadi ya imani katika Yeye na kwa ajili ya maelewano ya pamoja ambayo yanaendelea kukua kati yao.

Akisali kwa ajili yao, anafikiria kama yuko pamoja na katika  kuomba Mungu Baba yetu ili wakristo waweze kutembea katika ukweli katika moyo kuelekea katika umoja kamili.  “Ni njia hiyo tu, anathibitisha, inawezekana kujibu kwa uthabiti wito wa Bwana katika sala ya ili wote tuwe wamoja ( taz. Yh 17,21 ) na kwa maana hiyo tunaweza kutangaza vema Injili”.

Tanaalikwa kutumia muda wetu katika kutangaza, Yesu ambaye ataaminiwa iwapo atashuhudiwa katika maisha na kuuishi upendo wa dhti kwa namna ya pekee katika kijikita kwa matendo ya wahitiaji walio wengi kama Lazaro, anaye bisha hodi kila siku katika milango yetu. Kwa hakika katika kuhudumia binadamu wa leo, kulinda hadhi ya walio wadhaifu zaidi na kuhamasisha haki na amani, tunageuka sote kwa pamoja kuwa wahudumu wa ile amani ambayo Bwana alitangaza siku ya Pasaka (taz. Yh 20, 19) na ambayo alitupatia urithi”.

Baba Mtakatifu anaongeza kusisitiza: “Ninayo furaha kubwa ya kuwaleza hata mimi ndugu wapendwa kaka na dada: amani kwenu! Katika fursa ya tukio la Sinodi ya mwaka Baba Mtakatifu Francisko aidha anasema, bado anazo kumbukumbu za mkutano wao wa hivi karibuni huko Torino na Roma, kama vile wa huko Argentina.

“Wakati nikifanya kumbukumbu kwa shukrani ya wakati uliopita wa mkutano nchini Argentina, na mwingine wa hivi karibuni Torino, na Roma , ninatoa matashi mema kwa ajili ya Sinodi yenu na kwa kila mmoja wenu  katika siku za sala, ushirikishaji na kazi yenu. Juu yenu ninawabariki na Baraka ya Bwana, wakati nikiwaomba tafadhali msisahau kusali kwa ajili yangu na kwa ajili ya wote, ndugu zenu kaka na dada”!

Ikumbukwe kuwa: Katika sinodi ya Makanisa ya wamethodisti na wavaldese, ambayo itafungwa tarehe 31 Agosti 2018, wanajikita katika  umakini wa nafasi ya Kanisa, kati ya uwepo ndani ya  umma na maisha ya pamoja, udiaconia kati ya huduma na kutangaza, uhamiaji na mapokezi vilevile na  uekumene.

29 August 2018, 09:00