Papa:Inahitajika siasa nyenyekevu,jasiri na ushuhuda kikristo!
Sr. Angela Rwezaula- Vatican
Baba Mtakatifu Francisko amekutana mjini Vatican na wanasheria Katoliki, ambapo amewaleza kuwa, ili kuweza kuwa wanasiasa katoliki lazima hawali ya yote wawe mashuhuda, kwa maana kuna hali inayozidi kuwa ngumu kwa wakristo na madhehebu madogo madogo katika kanda nyingi zenye misimamo mikali. Pamoja na hayo anasema, hatari ya kweli ni ile ya kupambana na itikadi kali na katika matendo ya kudharau na kutojali utu wa mwingine. Amesisitiza hayo Baba Mtakatifu Francisko tarehe 22 Agosti kwa wawakilishi wa Mkutano wa kimataifa ulioandaliwa na Mtandao wa Wanasheria kimataifa Katoliki, na kuwapa mwelekeo kamili wa kufuata njia ya kufanya siasa ya kikristo.
Nji hiyo anasema, hawali ya yote ni mwaliko wa kutafuta kwa unyenyekevu na ujasiri wa kuwa shuhuda, na kupendekeza kwa kutumia taaluma yao na mpango wa sheria ya dhati katika maono ya kikristo na kibinadamu kijamii. Kwa namna ya pekee wale ambao wanajikita kuhamasisha wema wa pamoja anasisitiza kuwa wanaweza na wanapaswa kutoa mchango wa hali na mali hata katika masuala magumu yanayohusu uhuru wa kidini.
Ubaguzi kwa wakristo na mateso
Akikimbuka pia juu ya Mkutano wao wa mwaka huu 2018, ambao umejikita katika mada yao kuhusiana na uhuru wa kidini na dhamiri, Papa Francisko amesisitiza juu ya hatua ya tamko la hadhi ya binadamu, Dignitatis humanae ya mwaka 1965. Waraka huo unaonesha wazi hata suala hili la ukosefu haki na uhuru wa dini, kwasababu ya kwamba: hapakosekani udkiteta ambao hata kama ndani ya katiba yake unaonesha kuwapo uhuru na utendaji wa kidini, lakini wanajitahidi kuharibu raia kutoka na taaluma ya dini na kuifanya iwe ngumu kiasi chake, hata kuhatarisha maisha ya jumuiya ya kidini.
Kuna vivuli vingi vyeusi vinavyo ongezeka
Katika hali hiyo,Baba Mtakatifu anaongeza kusema, vivuli vingi na vipya vinakusanyika na kuongezea janga kubwa la hali mbaya ya wakaristo, hata wale wa madhehebu madogo madogo katika kanda ambazo itikadi kali inapitia. Hizi ni chini ambazo zinashambuliwa na kusambaa hata kuifika upinzani mkubwa, vurugu na gajsa ambazo hadi sasa zinazidi kuongeza ubaguzi, unyanyasaji na mateso ya kweli ambayo hayatakuwa kutekelezwa na mamlaka iliyoanzishwa.
Misingi mikali ambayo ni hatarishi na uharibifu
Akiendelea na hotuba yake amesisitiza pia kuwa kama kuna itikadi mbili na tofauti lakini wakati huo huo ni hatarishi, kwa ajili ya uhuru wa dini na dhamiri, uhusiano wa kiulimwengu na mizizi ya kidini kwa hakika kwa namna ya pekee ni hatari. Hizi ni hatari na kupambana nazo hasa itikadi kali na madharau ambayo zaidi yanasasabisha uharibifu iwe kwa upande wa tabia na mwenendo ,hata kwa maneno. Ikumbukwe kuwa, Mtandao wa wanasheria katoliki, ni mtandao wa wabunge katoliki duniani, ambao ulianzishwa mnamo mwaka 2010 kama ubunifu wa kimataifa unaojitegemea na uendeshaji wake