Cerca

Vatican News
 Mkutano wa Papa Francisko na wawakilishi wa Mkutano wa kimataifa kwa wanasheria katoliki Mkutano wa Papa Francisko na wawakilishi wa Mkutano wa kimataifa kwa wanasheria katoliki   (Vatican Media)

Papa:Inahitajika siasa nyenyekevu,jasiri na ushuhuda kikristo!

Papa Francisko akikimbuka juu ya Mkutano wao wa mwaka huu 2018, ambao umejikita katika mada kuhusiana na uhuru wa kidini na dhamiri, amesisitiza juu ya hatua ya tamko la hadhi ya binadamu ya Dignitatis humanae ya mwaka 1965. Waraka huo unaonesha wazi pia juu ya suala linahusu ukandamizaji na ukosefu wa uhuru wa kidini

Sr. Angela Rwezaula- Vatican

Baba Mtakatifu Francisko amekutana mjini Vatican na wanasheria Katoliki, ambapo  amewaleza kuwa, ili kuweza kuwa wanasiasa katoliki lazima hawali ya yote  wawe mashuhuda, kwa maana kuna hali inayozidi kuwa ngumu  kwa wakristo na madhehebu madogo madogo katika kanda nyingi  zenye misimamo mikali. Pamoja na hayo anasema, hatari ya kweli ni ile ya kupambana na itikadi kali na katika matendo ya kudharau na kutojali utu wa mwingine. Amesisitiza hayo Baba Mtakatifu Francisko tarehe 22 Agosti kwa wawakilishi wa Mkutano wa kimataifa ulioandaliwa na Mtandao wa Wanasheria kimataifa Katoliki, na kuwapa mwelekeo kamili wa kufuata njia ya kufanya siasa ya kikristo.

Nji hiyo anasema, hawali ya yote ni mwaliko wa kutafuta kwa unyenyekevu na ujasiri wa kuwa shuhuda, na kupendekeza kwa kutumia taaluma yao na mpango wa sheria ya dhati katika maono ya kikristo na  kibinadamu kijamii. Kwa namna ya pekee wale ambao wanajikita kuhamasisha wema wa pamoja anasisitiza kuwa wanaweza na wanapaswa kutoa mchango wa hali na mali hata katika masuala magumu yanayohusu uhuru wa kidini.

Ubaguzi kwa wakristo na mateso

Akikimbuka pia juu ya Mkutano wao wa mwaka huu 2018, ambao umejikita katika  mada yao kuhusiana na uhuru wa kidini na dhamiri, Papa Francisko amesisitiza juu ya hatua ya tamko la hadhi ya binadamu, Dignitatis humanae ya mwaka 1965. Waraka huo  unaonesha wazi hata suala hili la ukosefu haki na  uhuru wa dini, kwasababu ya kwamba: hapakosekani udkiteta ambao hata kama ndani ya katiba yake unaonesha kuwapo uhuru na utendaji wa kidini, lakini wanajitahidi kuharibu raia  kutoka na  taaluma  ya dini na kuifanya iwe ngumu kiasi chake, hata kuhatarisha maisha ya jumuiya ya kidini.

Kuna vivuli vingi vyeusi vinavyo ongezeka

Katika hali hiyo,Baba Mtakatifu anaongeza kusema, vivuli vingi na vipya vinakusanyika na kuongezea janga kubwa la hali mbaya ya wakaristo, hata wale wa madhehebu madogo  madogo katika kanda ambazo itikadi kali inapitia. Hizi ni chini ambazo zinashambuliwa na kusambaa hata kuifika upinzani mkubwa, vurugu na gajsa ambazo hadi sasa zinazidi kuongeza ubaguzi, unyanyasaji na mateso ya kweli ambayo hayatakuwa kutekelezwa na mamlaka iliyoanzishwa.

Misingi mikali  ambayo ni hatarishi na uharibifu

Akiendelea na hotuba yake amesisitiza pia kuwa kama kuna itikadi mbili na tofauti lakini wakati huo huo ni hatarishi, kwa ajili ya uhuru wa dini na dhamiri, uhusiano wa kiulimwengu na mizizi ya kidini kwa hakika kwa namna ya pekee ni hatari. Hizi ni hatari na  kupambana  nazo hasa itikadi kali na madharau  ambayo zaidi yanasasabisha uharibifu iwe kwa upande wa tabia na mwenendo ,hata kwa maneno. Ikumbukwe kuwa, Mtandao wa wanasheria katoliki, ni mtandao wa wabunge katoliki duniani, ambao ulianzishwa mnamo mwaka 2010 kama ubunifu wa kimataifa unaojitegemea na uendeshaji wake

23 August 2018, 13:44