Cerca

Vatican News
2018.08.12 Angelus Papa Francisko akiwa katika tafakari ya Malaika wa Bwana  (Vatican Media)

Papa anasema tuishi kwa ulinganifu wa ahadi za ubatizo

Baba Mtakatifu Francisko akiendelea kulezea juu ya kuishi ukristo anasema, mkristo hawezi kuwa mnafiki, kwani anapaswa kuishi kwa udhati. Na ahadi za Ubatizo zina mantiki ya aina mbili, ya kwanza ikiwa ni ile ya kukataa ubaya na ile ya ni pili kutenda wema.

Sr. Angela Rwezaula - Vatican.

Wapendwa kaka na dada na wapendwa vijana wa Italia habari za Asubuhi. Katika somo la Pili la siku Mtakatifu Paulo anatoa mwaliko kwetu sisi: msimhuzunishe Roho Mtakatifu wa Mungu, maana Roho huyo ni alama ya Mungu kwenu kwamba nyinyi ni watu wake na uthibitisho kwamba siku itakuja ambapo Mungu atawakomboeni (Efe 4,30). Lakini mimi ninawauliza: ni namna gani ya kuhuzunisha Roho Mtakatifu? Sisi sote tumepokea Ubatizo na katika kipaimara, kwa maana hiyo, ili  tusije kuhuzunisha Roho Mtakatifu ni lazima kuishi kwa ulinganifu wa  ahadi za Ubatizo, uliopyaishwa na Kipimara. Hiyo ni kuishi kwa dhati na siyo kuishi unafiki msisahau hilo!  Mkristo hawezi kuishi kinafiki, lazima aishi kwa ulinganifu na siyo kuishi kinafiki!

Ni utangulizi wa tafakari ya Baba Mtakatifu Francisko wakati wa sala ya Malaika wa Bwana Jumapili tarehe 12 Agosti 2018, katika viwanja vya Mtakatifu Petro, vilivyokuwa vimepambwa kwa  rangi za Vijana 70,000 kutoka nchini Italia, maujaji na   waamini wengine wengi, wakati mama Kanisa anaadhimisha Dominika ya 19 ya kipindi cha kawaida cha  mwaka B.

Baba Mtakatifu Francisko akiendelea kulezea juu ya kuishi ukristo anasema, mkristo  hawezi kuwa mnafiki, kwani anapaswa kuishi kwa udhati. Na  ahadi za Ubatizo zina mantiki ya aina mbili, ya  kwanza ikiwa ni ile ya kukataa ubaya na pili kutenda wema.  Kukataa ubaya maana yake ni kukataa vishawishi, dhambi na shetani. Kwa maana ya dhati ni kukataa  utamaduni wa kifo ambao unajionesha katika maficho ya hali halisi inayoelenga na kuelekea katika furaha za uongo na amnazo zinajielezea kwa njia za ulaghai,ujanja, uhaini unyang’anyi, kokosesha haki na kudharu wengine. Mambo yote hayo ni kuyakataa. Maisha mapya tuliyo pewa katika Ubatizo na ambayo Roho Mtakatifu ni kama chemichemi,yanasukumia mbali tabia ambayo inatawala hisia za migawanyiko na ukosefu wa maelewano.

Kutokana na hili Baba Mtakatifu anathibitisha kwamba Mtakatifu Paulo anatoa wito akisema: basi achaneni na uhasama, chuki, hasira, kelele na matusi. Acheni kila uovu (Efe 4: 31). Mambo sita haya au tabia hizi zinasumbua furaha ya Roho Mtakatifu na kuweka sumu ndani ya moyo, hadi kufikia kumchukia Mungu, hata jirani Baba Mtakatifu anathibitisha!

 Haitoshi kutofanya ubaya ili uwe mkristo wa kweli; ni lazima kukubali wema na kutenda yaliyo mema. Ndiyo maana Mtakatifu Paulo anaendelea kusema kuwa: muwe na moyo mwema na mwenye kuhurumiana; kila mmoja na amsamehe mwenzake kama naye Mungu alivyowasamehe nyinyi kwa njia ya Kristo. (Efe 4:32). Mara nyingi Baba Mtakatifu anasema, inatokea kusikia wengine wanasema: mimi simtendei mtu ubaya na kujiaminisha kuwa ni watakatifu: ni kweli Baba Mtakatifu anaongeza,  lakini je unatenda wema? Ni mara ngapi  na watu wangapi hawatendi ubaya, lakini vilevile hata hawatendi  wema  na maisha yao yanazidi  kutiririka katika utofauti, ubaridi na kutojali.

Tabia hiyo ni kinyume na Injili   na  kinyume na mwenendo wa vijana, ambapo kwa asili ya vijana ni wenye bidii, wenye kupenda sana na wajasiri. Lazima kukumbuka hilo, na iwap owatakumbuka basi Baba Mtakatifu amewasihii  warudie kwa pamoja kutamka:ni vema kutotenda ubaya, lakini pia ni vibaya kutotenda mema. Kwa maana hayo ni maneno ambayo yalikuwa yakitamkwa na Mtakatifu Alberto Hurtado, Baba Mtakatifu amebainisha!

Akendelea na tafakari lake  amewataka waendelea kuwa mstari wa mbele kwa ajili ya wema na katika wema!. Wasijihisi kuwa wamefika wakati hawatendi ubaya, na kutambua kuwa  kila mmoja ni mdhambi dhidi ya wema ambao alitakiwa kutenda lakini hakufanya hivyo. Haitoshi kutochukia, bali ni lazima kusamehe; haitoshi kutokuwa na na chuki, bali ni lazima kusali kwa ajili ya maadui; haitoshi kujiingiza katika sababu za migawanyiko na mikwaruzo,  bali, lazima kupeleka amani pale ambapo hakuna amani; haitoshi kutowateta vibaya wengine, bali, ni lazima kukatisha mazungumzo ubaposikia wangine wakizungumza vibaya juu ya wengine:

Ni muhimu kukatisha uchochezi, na ndiyo kutenda wema Baba Mtakatifu ameonya!. Iwapo hatutoi mkazo wa kukatiza ubaya ni kuuungozwa kwasababu ya kukaa kimya. Ni lazima kuingilia kati mahali ambapo ubaya unatawanyawa; maana ubaya inasambaratika mahali ambapo kuna ukosefu wa wakristo wenye ari na moyo wa kupenda yaliyo mema, kutembea katika upendo  kwa mujibu wa Mtakatifu Paulo kwamba : upendo uongoze maisha yenu kama vile Kristo alivyotupenda kwa ajili yetu akajitoa mwenyewe kama dhabihu yenye arufu nzuri na sadaka impendezayo Mungu. (Efe 5,2)

Akihitimisha Baba Mtakatifu Francisko amewambia vijana, siku hizi  wametembea sana, kwa maana hiyo wamefanya mazoezi  hivyo amewamia  watembee katika  wema, watembee katika upendo! Watembee kwa pamoja kuelekea katika Sinodi ya Maaskofu na Bikira Maria kwa umama wake na kwa maombezi yake awasimamie  ili kila siku, waishi kwa kufanya matendo mema  na kutamka hapana katika ubaya na ndiyo katika wema!  

12 August 2018, 16:13