Papa amesali kwa ajili ya waathirika wa daraja la Genova
Sr. Angela Rwezaula – Vatican
Ndugu wapendwa Kaka na dada, kwake Mama yetu mfariji wa wenye uchungu, ambaye tunamtafakari katika utukufu wa mbingu, ninataka kumkabidhi uchungu na maombolezo wote ambao katika sehemu mbalimbali za dunia wanateseka kimwili na kiroho. Mama yetu wa mbinguni aweze kuwafariji na kuwapa nguvu, ujasiri na utulivu!
Ni mwanzo wa maombi ya Baba Mtakatifu Francisko mara baada ya takafakari ya Malaika wa Bwana kwa waamini na mahujaji waliofika katika viwaja vya Mtakatifu Petro mjini Vatican, wakati Kanisa katoliki linaadhimisha Sikukuu ya Kupalizwa kwake Mbinguni Mama Maria ifanyikayo kila ifikapo tarehe 15 Agosti ya kila mwaka.
Kuanguka kwa daraja huko Genova, Italia.
Akiendelea na maelezo anakumbuka kwa namna ya pekee waliojaribiwa na janga la kuanguka kwa daraja tarehe 14 Agosti huko Genova Italia na kusambabisha waathirika wengi na wasiwasi mkubwa wa watu. Kwa maana hiyo anawakabidhi wote katika huruma ya Mungu watu wote waliopoteza maisha na kuonesha ukaribu wa kiroho na maombi kwa ajili ya familia zao, majeruhi na watu wengi ambao kwa sasa wamerundikana pamoja kutokana na kuharibiwa nyumba , aidha hata wengine walioguswa na wanateseka kutokana na tukio hilo. Anawaalika wote kuungana naye katika sala na kuomba kwa ajili ya waathirika na kwa ajili ya wapendwa wao kwa sala ya Salam Maria…
Na mwisho amesalimia watu wote Roma, mahujaji kutoka maeneo mbalimbali ya nchi dunani kote, na kuwashukuru uwepo kwa kuwatakia sikukuu njema ya Bikira Maria Mpalizwa lakini pia wasiwasahau kamwe kusali kwa ajili yake!