Cerca

Vatican News
Mkutano Rimini 2018 wa Jumuiya ya Comunione e Liberazione Mkutano Rimini 2018 wa Jumuiya ya Comunione e Liberazione 

Nguvu zinazotoa msukumo wa historia ndizo nguvu za kuleta furaha

Nguvu ambazo zinatoa msukumo wa historia ndizo hizo nguvu zenyewe zinazo mfanya binadamu awe mwenye furaha. Na ndiyo kauli mbiu ya Mkutano wa 2018 wa Jumuiya ya Comunione e liberazione ambapo mwanzilishi wa jumuiya hiyo Padre Giussani alikuwa aliwakabidhii vijana 1968 wagundue ni nguvu gani zinabadili historia!

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Ujumbe wa Mkutano kwa mwaka 2018 wa Jumuiya ya Comunione e Liberazione uliofunguliwa 19 Agosti 2018, ambapo   Baba Mtakatifu Francisko umetuma ujumbe huo ulio sainiwa na Kardinali Pietro Parolin Katibu wa Vatican unasema kuwa imani inatakiwa daima kuwa shauku ya kutoa msukumo wa historia. Mkristo hawezi kuacha kuota ndoto  ya kuona dunia iliyo bora.

Nguvu ambazo zinatoa msukumo wa historia ndizo hizo  nguvu zenyewe zinazomfanya binadamu awe mwenye furaha. Kwa maneno haya ambayo ndiyo kauli ya Mkutano wa 2018 wa Jumuiya ya Comunione e liberazione ambapo mwanzilishi wa jumuiya hiyo Padre Giussani alikuwa aliwakiwakabidhi vijana wagundue ni nguvu gani ambazo zinabadili historia ,na kujikita  kupima njia za kufanya mapinduzi mwaka 1968.

Mwaka 1968 na uzuri kwa ajili ya mabadiliko

Kuvunjika kwa wakati uliopita ulikuwa ni wenye mtindo wa kizazi ambacho kilikuwa kikijiweka katika matumaini yake katika mapinduzi ya muundo wenye uwezo wa kuhakikisha kwa kiasi kikubwa udhati wa maisha. Waamini wengi waliamini sehemu hii yenye kuwa na matarajio na kufanya imani kuwa katika  maadili ambayo bila hata kujua kuwa ni Neema, walikuwa wakiamini katika nguvu ya kutimiza matendo katika dunia iliyo bora.

Ni ujumbe ulioelekezwa kwa Askofu wa Jimbo la Rimini, Askofu Francesco Lambiasi  huko Rimini katika fursa ya Mkutano huo ambao hufanyika kila mwaka, na kuwaunganisha maelfu na maelfu ya watu mbalimbali, au kutoa mada mbalimbali kuhusiana na masuala ya Kanisa na jamii kwa mantiki ya mtazamo wa dunia, kadiri ya maono ya mwazilishi wa Jumuiya hii  Padre Giusani.

Kuongezeka kwa hofu kuelekea wakati ujao.

Ni kitu gani kinabakia katika utashi ule wa kubadili kila kitu? Kwasasa inajirudia hali ya kujenga kuta badala ya kujenga madaraja. Ipo tabia inayoendelea ya kujifungia badala ya kumfungulia mwenzako. Kadhalika inazidi kuku ana kuongezeka utofauti badala ya kushirikishana na kuwa na utashi wa kijikita pamoja katika ubunifu wa mabadiliko, na zaidi inazidi kuongezeka hali ya hofu dhidi ya tumaini la wakati endelevu. Kutokana na hilo, suala linakuja kujiuliza katika nusu karne je ulimwengu huo umeweza kuwa eneo zaidi la kuishi? Maswali hayo yanatazama hata sisi wakristo, ambao kwa nyakati zilizopita kwa njia ya kpindi cha mwaka 1968 ambacho hata leo hii, tunalikwa kujitafakari pamoja na wahanga wengine kujiuliza: ni kitu gani tumejifunza ? Ni kitu gani tunaweza kufanya kikawa kama tunu?

Kichawishi cha binadamu ni kile cha kujitosheleza binafsi.

Kishawishi daima cha binadamu ni kile cha kufikiria kuwa akili yake ,na uwezo wake ndivyo msingi ambao unatawala ulimwengu;na kujidai huku kunatendekea kwa mitindo ya aina mbili: wa kwanza ni ule wa kipindi cha kumkana Mungu, mahali ambapo wadau wake wanabaki wamejifunga kwa sababu zao ( ragione au hisia zao. Ya pili ni ile ya kujiona mwenye akili tu na kujaminisha moja kwa moja kutegemea nguvu binafsi... Kwa maana hiyo ujumbe unauliza swali je mkristo anayetaka kuzuia vishawishi hivi viwili, lazima ajikane kwa dhati kuwa na shauku ya mabadiliko?

Mkristo hajikani kamwe katika dunia iliyo bora.

Lakini hiyo kwa dhati haina maana ya kujiondoa katika ulimwengu ili usiweze kujiweka katika hatari ya kukosea kwa  kutaka kuhifadhi ile imani ambayo inatambulia katuka usafi wake ulioharibiwa. Hiyo ni kwa maana ya kwamba imani ya dhati inajikita daima kwa kina katika shauku ya kutaka mabadiliko ya ulimwengu kutoa msukumo wa historia kama kauli mbiu inayoongoza Mkutano huo wa mwaka 2018 Ujumbe unathibitisha. Lakini jeinawezekana? Mkristo hawezi kukataa kutoota ndoto ili kuweza kuona ulimwengu unakuwa bora. Hii na maana yake hasa ya kutazama kwa kina mzizi wake na mabo ni wa  uhakika. Mzizi huo msingi ni kwamba Kristo ndiye mwanzislishi wa ulimwengu mpya, ambaye Papa Francico anaeulezea kwa kifupi katika maneno haya: Ufufuko wake siyo wa wakati uliopita; ndani mwake unajikita katika nguvu ya maisha ambayo yamepenyeza katika ulimwengu, mahali ambapo utafikiri kila kitu kimekufa na kila sehemu inaanza kujitokeza vichipukizi vya ufufuko. Ni nguvu ambayo haina usawa.

Hakuna mapinduzi yanaweza kukidhi moyo wa mtu.

Hakuna nguvu yoyote na  hakuna mapinduzi yoyote yana uwezo wa kukidhi moyo wa binadamu, ujumbe wa Baba Mtakatifu kwa ajili ya Mkutano wa Rimini anahitimisha,  Ni Mungu peke yake ametuumba kwa utashi usio kuwa na kikomo, yeye peke yake anaweza kuujaza uwepo wake usio na mwisho; na ndiyo maana alijifanya mtu; ili kila mtu anao uwezo wa kukutana na Yeye anayeokoa na kutimiza matakwa ya furaha zakekama pia usemavyo Waraka wa Aparecida wa mwezi Juni 2007 ambao ulikuwa ni kama tunda la Mkutano V wa Baraza la Maaskofu wa wa Bara la Amerika ya Kusini na Visiwa vya Carribien.

20 August 2018, 15:52