Maombi ya Papa kwa watu wa Kerala ili wasikose msaada kimataifa
Sr. Angela Rwezaula - Vatican.
Mara baada ya sala ya Malaika wa Bwana, Baba Mtakatifu, Jumapili 19 Agosti 2018, ameomba msaada kwa ajili ya watu wa serikali ya India, waliopatwa na janga la mafuriko. Inasemekana hali ni mbaya na watu 350 wamekufa kutokana na janga hili la sili , wakati huo huo operesheni ya kuokoa bado inaendelea.
Ukaribu na Kanisa mahalia
Mbele ya uharibifu huo Baba Mtaktifu ameomba, wakose ndugu hawa kupewa msaada wetu wa mshikamano na msaada wa dhati kutoka jumuiya ya kimataifa. Kwa maana hiyo anaonesha ukaribu wake kwa Kanisa mahalia la Kerala ambao kwa dhati wakiwa mstari wa kupeleka msaada kwa watu. Amewataka watu wote kusali kwa ajili yao, wote waliopoteza maisha na watu wote ambao wamejaribiwa na janga hili kubwa.
Idadi ya waathiririka na waliorundikana inazidi kuwa kubwa
Kulingana na vyombo vya habari vinaeleza, namba ya waathirika imezidi kupanda hadi kufikia 357 kutokana na mafuriko hayo huko Kerala, kati yao 33 kwenya masaa 24 yalipopita. Kuna zaidi ya watu 223,000 walio lazimika kuacha makazi yao na kukimbilia katika makambi yaliyojenga ili kuweza kukabiliana na dharura hiyo.
Ni makadirio ya ubaribifu wa milioni 3 za dola za kimarekani
Kwa mujibu wa serikali mahalia wanasema uharibifu ni mkubwa mno ambao umesababisha na janga hili la asili na kadirio l dola 2.900 za kimarekani zitahitajika. Gharama ya mwisho itaweza kutolewa kwa ufasaha hasa kama wataweza kurudisha maji moja kwa moja.
Kwa sasa inahitajika kuongeza juhudi kubwa za operesheni hiyo , mkuu wa uendeshaji wa Kerala ameomba fedha za kuongeza na kutuma Helikopta 20, mitumbwi 600 za injini zaidi ya zile ambazo zilikuwapo tayari zipo katika ardhi hiyo. Waziri Mkuu wa India Bwana Narendra Modi ambaye Jumamosi alikwenda na helikopta katika serikali iliyokumbwa na mafuriko ametangaza dharura ya kitaifa inayohitaji msaada wa haraka wa milioni 75 za dola za Marekani.