Cerca

Vatican News
Papa Francisko wakati wa sala ya Malaika wa Bwana Papa Francisko wakati wa sala ya Malaika wa Bwana 

Papa:Kwa njia ya mwili na damu ya Yesu tunajifunza maisha ya milele

Yesu anatualika leo hii kama vile alivyo fanya miaka 2000 iliyopita akiwa katika Sinagogi ya Kafarnaum, mara baada ya kugawa mikate mitano na samaki wawili, ili kula nyama yake na kunywa damu yake na kwamba tuwe na uzima wa milele. Na sisi tubaki katika mwaliko huo kama vile wasikilizaji waliokuwa katika Sinagogi hiyo.

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Baba Mtakatifu Francisko ametafakari mahubiri ya Kristo akiwa katika hekalu huko Kafaranaum na kusema kuwa “msipokula mwili wangu na kuinywa damu yangu hamtaishi milele. Yesu anatualika kuingia katika muungano na Yeye na kuishi kwa ajili ya Bwana na ndugu. Lakini iwapo inatuwia vigumu kutenda hivyo ni kwasababu tupo kinyume na  mantiki zake kwani  ni tofauti za na zile za ulimwengu.

Yesu anatualika leo hii kama vile alivyo fanya miaka 2000 iliyopita akiwa katika hekalu huko Kafarnaum mara baada ya kugawa mikate ili kula nyama yake na kunywa damu yake ili nasi tupate maisha. Na sisi tubaki katika mwaliko huo , kama vile wasikilizaji waliokuwa katika hekalu, na wakati inakuwa vigumu kurekebisha mwenendo  kuenenda kama Yesu,  kutenda kadiri ya matakwa yake na siyo yale ya ulimwengu.

Mkate ni mwili wangu kwa ajili ya maisha ya ulimwengu

Ndiyo tafakari ya Baba Mtakatifu Francisko aliyo anza nayo wakati wa sala ya Malaika wa Bwana tarehe 19 Agosti 2018, kwa waamini na mahujaji wote waliofika toka pande za dunia kushiriki naye sala hii. Akiendelea na tafakari hiyo ya Injili ya 20 ya Mwaka B wa Kanisa ya Mtakatifu Yohane  na sehemu ya pili ya Yesu aliyo hutubia Bwana Yesu, Yeye anajiwakilisha kama Mkate hai ulioshuka mbinguni”na mkate anao utoa Yeye ni wenye uzima wa milele, na kuongeza Mkate ambao nitatoa mimi ni mwili wangu kwa ajili ya maisha ya ulimwengu.

Katika mkate anao ushirikisha ni zawadi binafsi hadi kujitoa sadaka yake.

Baba Mtakatifu anakazia kusema, watu waliokuwa wanamsikiliza walijiuliza na kuwa na wasiwasi, ni jinsi gani huyu anaweza kutupatia mwili  wake na kuula? walikuwa hawajuhi maana ya kweli ya ishara ya mkate wa kushirikisha, yaani zawadi binafsi hadi kufikia kujitoa sadaka. Ni kwa maana hiyo inafikia kumkana yule ambaye mwanzo walimwona kama mwenye kuleta ushindi. Mwanzo walitaka kumfanya hata mfalme baadaye, wanajiondoa kwasababu hawakupenda maneno yake Yesu.  Lakini Kristo aliendelea kusema, kama msipo ula mwili wa mwana wa adamu na kunya damu yake hamtaishi milele.

Baba mtakatifu anasisisiza, watu na mitume watakapo anza kutambua kuwa Yesu anawaalika kuingia katika muungano Naye, kula Yeye, ubinadamu wake , kwa ajili ua kushirikishana na Yeye zawadi ya maisha kwa ajili ya ulimwengiu ndipo ushindi mkubwa wa kiajabu na mafanikio!

Ekaristia ni utangulizi wa kuonja mbingu hapa duniani.

Mkate wa maisha, Baba Mtakatifu anaweka bayana ni sakramenti ya Mwili na Damu ya Kristo inayotolewa kwetu bure katika karamu ya Ekaristi. Ndicho kinachotushibisha na kutunywesha kiroho leo hii na milele. Kila mara unaposhiriki Misa Takatifu, kwa maana nyingine ni utangulizi wa kuiona mbingu chini ya ardhi hii, kwasababu  kwa njia ya chakula cha ekaristi , Mwili na Damu ya Yesu, tunajifunza nini maana ya maisha ya milele. Hii ina maana ya kuishi kwa ajili ya Bwana: Yule anilaye, ataishi kwa ajili yangu: Ekaristi inatuimarisha kwa upya kwasababu hatuishi kwaajili yetu sisi, bali kwa ajili ya Bwana na ndugu. Furaha na maisha ya milele yanategemea na uwezo wa kuyafanya yazae matunda ya upendo wa kiinjili ambayo tunapokea katika ekaristi.

Ugumu wa kurekebisha namna ya kuishi kwetu kadiri ya maisha ya Yesu.

Yesu anatualika hata leo hii kula mwili wake na damu yake ili nasi tuwe na maisha, anasisitiza Baba Mtakatifu na kuongeza, lakini si chakula cha kawaida, bali ni mkate hai na unamwilisha na kutoa uhai, ambao unajieleza katika maisha yenyewe sawaswa na  Mungu. Ili  kupata maisha haya ni lazima kujimwilisha Injli na upendo na ndugu. Na iwapo mbele ya mwaliko wa Yesu tunahisi kujadili juu yake na kupinga, kama vile ilivyokuwa kwa wasikilizaji wa wakati ule katika hekalu basi hiyo ni kwasababu ni vigumu kurekebisha namna yetu ya kuishi kadiri ya maisha ya Yesu, kutenda kwa mujibu wa mantiki zake na siyo kwa mujibu wa mantiki za ulimwengu.

Tumpokee Kristo hai ambaye anatuandalia mbingu

Tunapolishwa mwili huo, Baba Mtakatifu akihitimisha, tunaweza kuingia moja kwa moja na maelewano  na Kristo , kwa hisia zake na mwenendo wake, kwa njia hiyo ni muhimu sana kuwasiliana ; ni muhimu kwenda katika Ibada ya Misa na kupokea komunio kwasababu ni kupokea Mwili wa Kristo, ni kupokea Kristo ambaye anatugeuza ndani na kupokea Kristo hai anaye tuandalia mbingu.

Mama Maria anayetusimamia atusaidie kwa maana ndiyo ilikuwa sala yake ya mwisho, katika mapendekezo ya kufanya muungano na Yesu Kristo kwa kujimwilisha ekaristi yake ili maisha yetu kwa mara nyingine tena  yawe mkate unao megeka kwa  ndugu!

20 August 2018, 09:05