Cerca

Vatican News
Kwa mujibu wa Papa, inawezekana kupambana na utumwa mamboleo! Kwa mujibu wa Papa, inawezekana kupambana na utumwa mamboleo!  (ANSA)

Inawezekana kabisa kupambana na mitindo mipya ya utumwa mamboleo

Papa amekuwa akisisitizia juu ya viongozi wote wa serikali na dini ili kutatufa kila njia na hasa katika sera za kisiasa, ili kuchangia ushirikiano hasa katika kutoa mchango mkubwa wa ajili ya kubuni mbinu na kukabiliana janga ili baya, kutafuta sababu na matokeo ya mitindo hii mipya ya majanga ya kufedhehesha mwanadamu!

Sr. Angela Rwezaula - Vatican.

Kwa miaka mitano iliyopitia mbiu kuu imesikika katika Kanisa katoliki  na duniani kote mara kwa mara kuendeleza wito wa kutazama kwa karibu wosia wa Baba Mtakatifu Francisko  kwa upande wa kukomesha kila aina za utumwa mamboleo na biashara haramu ya Binadamu. Hata leo hii kampeni nyingi zinafanyika karibu duniani kote ili kuweza kupambana na janga hili la hatari. Baba Mtakatifu Francisko mara nyingi amesema kwamba biashara na aina mpya za utumwa ni aibu ya kutishia binadamu.

Papa amekuwa akisisitizia juu ya viongozi wote wa serikali na dini ili kutatufa kila njia na hasa katika sera za kisiasa, ili kuchangia  ushirikiano hasa katika kutoa mchango mkubwa wa ajili ya kubuni mbinu na  kukabiliana janga ili baya, kutafuta  sababu  na matokeo ya mitindo hii mipya ya majanga  ya kufedhehesha mwanadamu, shughuli ambayo inazidi kuendelea kuwa sababu kubwa ya ya mateso ya binadamu mdhaifu.

Ikumbukwe Baba Mtakatifu mara baada ya kukutana  mwaka huu na wajumbe wa mkutano wa kimataifa kuhusana na suala la  biasharaharamu ya binadamu na aina mbalimbali za utumwa mamboleo alisema,kwamba ni matarajio yake siku ambazo walikaa na  kutafakari kwa kubadilishana uzoefu, ziliweza kuwapa mwanga zaidi wa tatizo hili sugu la kidunia, na zaidi katika nchi  mahalia kuhusiana na suala la biashara haramu ya binadamu

Uzoefu wa namna hiyo unaonesha ni jinsi gani mitindo ya utumwa imesambaratika kiasi kama mafuta ya petroli kiasi cha kutoweza kuamini hadi kufikia kuona aibu ndani ya maisha ya kila siku na hasa kuondoa matarajio ya jamii zetu. Kwa mujibu wake anasema kilio cha Mungu juu ya Kaino anayeonesha katika maandiko matakatifu ya Biblia, na kuuliza: yuko wapi kaka yako, kinatoa mwangwi ndani ya hisia zetu kwa nguvu zaidi kuona mitindo hii mipya utumwa inavyozidi kukua ndani ya jamii na ambapo haitakiwi kufumbiwa macho, kwa namna ya pekee kama mambo mengine yanayofichika kichini chini kama vile unyanyaswaji wa binadamu, wanawake na watoto, ambazo zaidi ni waathirika mana hawana wa kuwatetea, na manyanyaso ya kijinsia.

Umuhimu wa kuendelea  kupambana na biashara haramu ya maisha ya watu, kwa dhati lengo lake  ni kuondoa mzizi na nyavu za kihalifu zilizo tapakaa kila upande  na  ambazo lazima zifikiriwe kama kitengo kilicho kikubwa cha kupangwa na kivaliwe njuga, kwa mfano utumiaji  wahusika wa kiteknolojia na vyombo vya mawasiliano , bila hata kutazama mafunzo magumu ya maadili ya kisasa ambayo yanazidi kukua kiuchumi kwa  kupendelea  kujinufaisha kupitia jasho na  miili ya watu.

Aidha mategemeo ya Papa Francisko kwa wajumbe wa Mkutano wa kitaifa ilikuwa kwamba majadiliano yao yaweza kuwasaidia kuwa na utambuzi wa dhati juu ya ukuaji wa hali hii mbaya, hata ulazima wa kuwasaidia waathirika ili kuweza kuwasaidia waweze kushirikikiswa katika jamii na ili waweze kuhisi ya hadhi ya kibindamu. Kutokana na mapendekezo hayo Baba Mtakatifu  aliongeza kusema kwamba Kanisa halina budi  kutoa shukrani kwa juhudi ambazo zinaendelezwa na hasa za kuonesha huruma ya Mungu kwa  kwa wale ambao wanateseka , kwasababu hiyo wanawakilisha hatua muhimu kwa ajili ya kutuliza na kupyaisha jamii kwa pamoja.

Hata hivyo Kardinali Vicent Nichols Askofu Mkuu wa Westminster Rais wa Baraza la Maaskofu wa Uingereza na Galles na Rais wa Kikundi cha Mtakatifu Marta wakati akimsalimia Bara Mtakatifu katika Ukumbi wa Clementina Mjini Vatican alitaja kuwa tukio la janga  hili ni sehemu nyeusi ya ulimwengu  katika biashara haramu ya binadamu na mitindo mbalimbali za utumwa

Hili ni changamoto kubwa ambapo alimshukuru Papa Francisko kuwatia moyo juhudi za kikundi hiicho cha kimataifa kwa namna ya pekee kujikita katika kushirikiana kuhamasisha kwa dhati dhamiri na ewajibikaji mahalia na hasa katika kuunda vikundi washiriki kama vile  kutoka nchi ya Argentina, Ulaya Mashariki, Afrika na Asia.  Pamoja na hayo yote juhudi ya kukabiliana  hasa ni ile ya serikali mahalia ili waweze kutazama na kukabiliana janga la utumwa mamo leo kwa kujikita kwa dhati kuwatafuta wahalifu wa matendo ya  kinyama na ambayo ynamwondolea hadhi mwanadamu

Kwa mujibu wa Kardinali Nichols wakati wa kuzungumza na vyombo vya habari vya Vatican News  alisema chambo hiki cha kimataifa “ Kikundi cha Mtakatifu Marta, kiliundwa na Baba Mtakatifu Francisko kunako mwaka 2014, ambapo kwa sasa wameshakuwa mamia ya watu kutoka nchi 30 duniani , wakiwa mstari wa mbele kupambana na biahara  haramu ya binadamu, na zaidi pia kuwa na waathirika karibu sana kwa ajili ya kuwasaidia na kuwatuliza kuathirika kwao.

Kuna milioni 42 za watu ambao ni watumwa duniani alithibitisha Kardinali Nichols, pamoja na hayo pia alionesha kuwa kuna milioni 44 za wavuvi baharini ambao wananyonywa na kunyanyaswa   katika dunia nzima. Ili kuweza kuwakomboa inahitaji kazi kubwa ya kujenga madaraja na ushirikiano kwa ngazi mahalia, kitaifa na kimataifa.  Lakini pia kuna ripoti kati ya nchi mahalia na nchi ambazo wanaelekea, kwa maana hiyo haiwezekani kabisa kufikiria tu nchi ambazo watu wanalekea lakini pia zaidi kufikiria mahali watu hao wanatokea na ndiyo maana ndipo wanapoanzia kuwa watumwa wapya alithibitisha.

14 August 2018, 16:34