Tafuta

Vatican News
Baba Mtakatifu akizungumza na waandishi habari 70 katika ziara yake nchini Ireland Baba Mtakatifu akizungumza na waandishi habari 70 katika ziara yake nchini Ireland  (AFP or licensors)

Papa: Ninarudi nchini Ireland mara baaada ya miaka 38!

Baba Mtakatifu Francisko akizungumza na waandishi wa habari 70 katika ndege kuelekea mjini Dublin, amekumbuka kipindi alichokaa nchini Ireland, miaka 38 iliyopita akijifunza lugha ya kingereza. Pia amesema baada ya Mkutano wa Philadelfia, wa Dublin ni Sikukuu yake ya pili ya Familia.

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

“Hii itakuwa Sikukuu yangu ya pili ya Familia; ya kwanza ilikuwa ya Philadelfia, na hii ndiyo ya pili. Mimi ninapenda kuwa na familia na ninafurahi kwa ziara hii”. Ni maneno ya Baba Mtakatifu Fransisko kwa waandishi wa habari akiwa njiani kuelekea Ireland; Ni ziara ya Pili ya Khalifa wa Mtume Petro, Papa kutoka Vatican kueleka katika Kisiwa hiki cha Ireland, kwani kwa mara ya kwanza kukanyaga huko alikuwa ni Mtakatifu Yohane Paulo II mnamo mwaka 1979.

Baba Mtakatifu pia ameonesha sababu nyingine ambayo imemgusa rohoni mwake katika ziara hiyo ya kwamba “Ninarudi nchini Ireland baada ya miaka 38 mahali ambapo nilikaa karibu miezi mitatu nikiwa najifunza kingereza, mwaka 1980. Na hata kwa upande wa msemaji Mkuu wa Vatican Bwana Greg Burke akimshukuru, Baba Mtakatifu kwa kuwasalimu waandishi wa habari, amesema hata yeye ni kumbukumbuku.

Kadhalika amesema, “tunafanya safari hii fupi lakini ya kina, katika nchi ndogo lakini ambayo ni muhimu inayojulikana sana duniani, kwa upande wa Kanisa na pia duniani. Amemjulisha Baba Mtakatifu kuwa, “Wapo waandishi wa habari 70 hapa, amesema Bwana Burke na walio wengi wanatoka Ireland kwa maana wengine wanaishi Roma na ambao wameamua kufanya  safari na sisi, kwa maaana hiyo ninaweza kusema kuna matarajio makubwa na mazuri ya safari hii”.

 

 

26 August 2018, 12:56