Tafuta

Mkutano wa Papa na Maaskofu wa Ireland wakati wa hitimisho la Mkutano wa Familia duniani mjini Dublin Mkutano wa Papa na Maaskofu wa Ireland wakati wa hitimisho la Mkutano wa Familia duniani mjini Dublin 

Papa:Maaskofu wa Ireland kuweni jasiri na wabunifu!

Baba Mtakatifu amependa kutoa neno moja la kuwatia moyo ili kuwa na uvumilivu katika kutoa huduma yao angavu ya Injili na kuwa wachungaji wa zizi la Yesu kwa maaskofu Katoliki wa Ireland kabla ya kuondoka katika kisiwa hiki kinachotawaliwa na uoto wa kijana wa asili, mahali ambapo amefanya ziara ya siku mbili 25-26 Agosti 2018.

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Kwa kuongozwa na mwanga wa Imani katika kupyaisha kwa kina Kanisa la sasa na Taifa, maaskofu wa Ireland wawe wachungaji, baba na ukaribu kwa watu wa Mungu. Na siyo kujiona. Ndiyo mojawapo ya ushauri wa Baba Mtakatifu Francisko aliyoutoa katika Mkutano wake wa mwisho mjini Dublin kwa Maaskofu kabla ya kuondoka kurudi mjini Roma.

Baba Mtakatifu amependa kutoa neno moja la kuwatia moyo ili kuwa na uvumilivu katika kutoa huduma yao angavu ya Injili na kuwa wachungaji wa zizi la Yesu kwa maaskofu Katoliki wa Ireland kabla ya kuondoka katika kisiwa hiki kinachotawaliwa na uoto wa kijana wa asili, mahali ambapo amefanya ziara ya siku mbili 25-26 Agosti, kipindi ambacho kimakuwa muhimu na cha kina kwa wanafamilia kutoka duniani kote. Mkutano wa Baba Mtakatifu Francisko na viongozi wa Kanisa la Ireland , umefanyika katuka nyumba ya Shirika la  watawa wa Kidomenikani wa Mama Yetu wa Rosari na Matakatifu Katerina wa Siena, ambao wanajikita katika mafundisho katoliki kwa shule katika zana za utunzaji bora wa mazingira.

Matumaini kutoka kwa papa na baraka.

Katika koventi hiyo Papa amepokelewa na Askofu Mkuu Kardinali Eamon Martin Rais wa Baraza la maaskofu Ktoliki nchini Ireland ambapo katika salam,Askofu ameonesha jinsi gani ziara ya Papa imekuwa ya baraka  na sababu ya matumaini ya wakati endelevu wa Kanisa la Ireland na taifa zima kwa ujumla. Vile vile ameonesha ni jinsi gani maaskofu wote wanayo shauku ya kuwasaidia vijana wa Kirosto ili waweze kuwa na sababu ya kuishi na zaidi kuhisi furaha ya kweli katika maisha yao, kwa mang’amuzi ya dhati.

Kuwa karibu na mapadre.

Nafasi ya maaskofu katika Kanisa pia ni maneno yaliyoguswa kwa kina katika kinywani cha Papa Francisko ya kwamba lazima kuwa Baba kwa ajili ya watu waaminifu wa Mungu, na  hapo ndipo inajieleza kazi ya kutia moyo, kuhamasisha, kupatanisha na zaidi kuvumilia yote mema ambayo yanatokana na Kanisa. Kwa maana hiyo   Baba Mtakatifu anasema “maneno ninayo wakabidhi ni kuwatia moyo kwa ajili ya kukabiliana na changamoto ya wakati huu na kufurahia huduma ambayo wanajikita kwasababu ya kuwasaidia maskini hata mapadre wengi pia. Mtu wa karibu zaidi Baba Mtakatifu amesema, mnaye kwa maana ni adhabu na ambayo inakatisha tamaa ya matokeo ya fedheha za hivi karibuni ambazo daima zilikuwa zimedharauliwa.

Utambuzi ba malipizi ya dhambi kubwa

Baba Mtakatifu katika hotuba yake, hakuacha kukabiliana kwa mara nyingine na maaskofu juu ya tema ya mtazamo mpya na ulazima wa Kanisa kuwa na utambuzi na uharaka wa kufanya malipizi kwa njia ya ukarimu wa Injili na ujasiri wa utambuzi wa makosa yaliyopita ambayo ni dhambi kubwa, inayo tazama ulinzi wa watoto na watu wazima waathirika, kati yao wakiwemo wanawake. Baba Mtakatifu amesema, kutambua mchakato wa wa kufita kwa haraka katika kutubu na kupatana na waathirika ambao wamekumbwa na manyanyaso ya kingono ndiyo wajibu mkubwa kwa sasa uliopo. Na jinsi gani ya kutafuta suluhisho la pamoja katika sheria kwa ajili ya ulinzi na usalama wa vijana. Kadhalika maesema:Kwa miaka hii sisi sote tumefunga macho kwa maana  ni uchungu mkubwa kufungulia macho katika mambo magumu ya kusambaa kwa manyanyaso, nguvu, na dhamiri na  kwa mantiki mbalimbali ya kijamii. Nchini Ireland kama ilivyo mahali pengine, ukarimu na ufungamani na Kanisa kuamua kukabiliana na suala hili la uchungu wa hisotria  yake unaweza kuwa  mfano  wa wito kwa jamii nzima na hivyo endeleni namna hiyo.

Hakuna kufanya umbali na kujiona

Unyenyekevu kwa kawaida ni  uchungu amesisitiza Baba Mtakatifu kwa nguvu lakini “wote tumekombolewa kwa njia ya unyenyekevu wa Mwana wa Mungu na hivyo tia juhudi”. Madonda ya Kristo yanatupatia ujasiri. Ninawaomba tafadhali ukaribu.  Ukaribu ni ufunguo kwa Bwana na kwa watu wa Mungu. Msirudie tabia za kuwa mbali na kujiona ambamo wengine katika historia zenu, wametoa picha iliyo mbaya katika Kanisa  hasa kwa kuonekana kuwa ni yenye madaraka, ni ngumu na inayojitosheleza. Akiendelea,Baba Mtakatifu amekabiliana na maskofu juu ya mada mbalimbali walizozungumza wakati walipofika katika Ziara yao ya kichungaji mwezi Januari mjini Vatican , na kusema kuwa changamoto katika jamii ya sasa inayoendelea na mapinduzi inabaki kuoneshwa kwa imani katika ufungamani wake na uzuri wake wa dhati.  Hiyo ni kama inavyojionesha katika Mkutano wa Familia duniani ambapo wanafamilia wanaendelea kuwa watambuzi daima wa nafasi yao isiyo badilishwa kamwe. Kwa sababu imani inathibitha,na lazima iwe na mapokeo na kuoneshwa katika familia na kwa njia ya kugha ya kuzaliwa yaani lugha ya familia!

Majaribu kama fursa ya upyaishao.

Matukio ya miaka ya mwisho imeweka majaribu ya imani katika utamaduni wa nguvu ya watu wa Ireland, lakini pamoja na hayo, Papa Francisko anathibitisha kuwa hata wameweza kutoa fursa ya upyaisho wa ndani katika Kanisa nchini humo na kuelekeza mitindo mipya ya kufikiria maisha yake na utume wake. Kutokana na hiyo ndipo papa anatoa mwaliko kwa maakofu: Kwa unyenyekevu, matumaini katika neema mnaweza kung’amua na kuchukua njia mpya katika vipindi hivi vipya. Muwe wajasiri na wabunifu. Kwa hakika maana kuu ya kimisionari iliyo na mizizi katika roho za watu wenu, zitaweza kufungua nja za ubunifu na kutoa ushuhuda katika ukweli wa Injili na kufanya ikue Jumuiya ya waaimini wa upendo wa Kristo na katika kukua kwa ufalme wake wa mbinguni.

Kadhalika wamewamba maaskofu wawe baba na wachungaji na siyo wawe  “baba wakambo” kwa familia ya Mungu, waunganishe hata matumaini yanayojikita kwa kina juu ya ukweli wa maneno ya Yesu Kristo na juu ya uhakika wa ahadi zake. Mara nyingine, Baba Mtakatifu anawashuri,  na watu wenu wa Mungu mtakapohisi kuwa zizi dogo ambalo linakumbana na changamoto,na matatizo msikate tamaa. Kama Mtakatifu Yohane wa Msalaba anavyotufundisha “ni usiku wa giza nene ambao mwanga wa imani unaangaza zaidi kwa usafi wa roho zetu. Mwanga ule utawaonesha njia za upyaisho wa maisha ya kikristo katika nchi ya Ireland kwa miaka ijayo! Baba Mtakatifu amaethibitisha.

Amehitimisha akiwakabidhi kwake Mama Maria na Roho wa umoja wa Kanisa na kuwaomba wote watende kwa mantiki ya kiekumene na kijamii. Amesisitiza juu ya kuhamasisha umoja na udugu kati yao kwa maana ni muhimu kushirikiana na viongozi wengine wa jumuiya za kikristo, kusali kwa pamoja kwa ajili ya mapatano, amani kati ya wote familia ya nchi ya Ireland.

Wakati wa kurudi Italia wametuma telegram kwa Rais wa nchi ya Ireland  Bwana Michael D. Hiddings, mahali ambapo anatoa shukrani kubwa kwa makaribisho ya nguvu aliyo pokea na viongozi na watu wapendwa wa Ireland. Kadhalika akiwa ndani ya Ndege ametuma ujumbe wa salam kwa Malkia Elizabeth na watu wa nchi ya Uingereza na kuwatumia baraka. Rais Macron wa Ufaransa na rais wa Uswisi, na kuwatakia Baraka tele kutoka kwa Mungu.

28 August 2018, 09:30