Tafuta

Vatican News
Misa ya Baba Mtakatifu Katika Uwanja wa Phoenix mjini Dublin, Ireland Misa ya Baba Mtakatifu Katika Uwanja wa Phoenix mjini Dublin, Ireland  (AFP)

Papa ahimiza kupendana ndani ya familia kama Kristo!

Mkutano wa ujao wa Familia duniani utafanyika mjini Roma mwaka 2021. Ikiwa ni katika kufanya kumbukumbu ya mwaka V wa Wosia wa Kitume wa Amoris Laetitia. Ametangaza hayo Kardinali Kevin Farrell, mara baada ya hitimisho la Misa Takatifu iliyoongozwa na Baba Mtakatifu Francisko mchana katika Uwanja wa Phoenix mjini Dublin kwa waamini karibia 300 elfu.

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Mkutano wa ujao wa Familia duniani utafanyika mjini Roma mwaka 2021. Ikiwa ni katika kufanya  kumbukumbu ya mwaka V wa Wosia wa Kitume wa Amoris Laetitia. Ametangaza hayo Kardinali Kevin Farrell, mara baada ya hitimisho la Misa Takatifu iliyoongozwa na Baba Mtakatifu Francisko mchana katika Uwanja wa Phoenix mjini Dublin kwa waamini karibia 300 elfu.

Kipindi cha hitimisho la Ziara ya 24 ya kitume ya Baba Mtakatifu Francisko mjini Ireland, kilikuwa ni Misa Kuu iliyo adhimishwa mchana katika uwanja wa Phoenix , moja ya Kiwanja kikubwa maarufu sana cha Ulaya mahali ambapo hata Mtakatifu Yohane Paulo II aliadhimisha Misa takatifu kunako mwaka 1979. Maelfu ya familia wamejaza uwanja huo wa kijani kwa furaha na ambao tayari una ushuhuda mkubwa! Mwanzo wa  Ibada kuu, Baba amenguliza na tendo maalum  la maungamo kwa ajili ya kuomba msamaha kutokana na janga la manyanyaso kwa watoto na watu wazima yaliyotokea nchini Ireland , yaliyosababishwa na makleri.

Kuweni kisima cha kuwatia moyo wengine

Baba Mtakatifu katika mahubiri yake anakumbusha kuwa kila siku katika maisha ya familia zao na katika kila kizazi kuna ahadi mpya ya Pentekoste; Pentekoste inayoanzia nyumbani na  ambayo Yesu anaituma kama mfariji wa Roho Mtakatifu ambaye anatoa ujasiri. Baba Mtakatifu answakabidhi wote waliokuja katika Mkutano wa IX wa familia kugeuka kuwa “ kisima cha kuwatia wengine moyo.

Ni upendo tu unaweza kuokoa dunia

 Akitafakari somo la Pili la Mtakatifu Paulo, mahali ambapo anazungumzia ndoa kama ushiriki wa fumbo la uaminifu wa Kristo na Kanisa mchumba wake, Papa amesisitiza kuwa, Mafundisho hayo yanaweza kuonekana  kwa mtu kama “neno gumu”, lakini ni  kielelezo kinachotumiwa na wafuasi wengi wa Injili ya sasa. “ Kuishi katika upendo kama Kristo alivyotupenda, kwa dhati inapelekea  kujifia sisi wenyewe kwa ajili ya kutoa upendo ulio mkubwa zaidi”. Ni kwa njia ya upendo huo tu, unao weza kuokoa dunia dhidi ya utumwa wa dhambi na utofauti kwa wenye shida na wale ambao hawana bahati. Huo ndiyo upendo ambao tumeutambua kwa Yesu Kristo” anathibitisha Baba Mtakatifu! Yeye alijiumba katika ulimwengu wetu kwa njia ya familia na kwa njia ya ushuhuda wa familia za kikristo katika kila kizazi  ina uwezo wa kuwa familia mmoja ya kibinadamu ambayo inaishi pamoja katika haki, utakatifu na katika amani.

 Haina haja ya mipango yenye mikakati

Changamoto ambayo leo hii familia inakabiliana nayo ni sawa na matatizo ambayo siyo machache waliyo kabiliana nayo wamisionri wa kwanza wa Ireland , kama vile Mtakatifu Colombano na kundi lake dogo ambao walipeleka Injili katika ardhi za Ulaya katika nyakati  zilizokuwa zimeanguka kwa upande wa utamaduni. Mafanikio yao makubwa ya kimisionari, yalikuwa hasimamii juu ya mitindo au mipango ya kimkakati, bali juu ya unyenyekevu na uhuru wa wema kutokana na ushauri wa Roho Mtakatifu. Ndiyo yalikuwa maisha yao ya kila siku kushuhudia kwa imani katika Kristo na kati ya hayo waliweza kupata mioyo mingi iliyokuwa inatamani kwa nguvu zote neno la neema na kuchangia katika kutotoa utamaduni wa Ulaya. Kama ilivyokuwa kwa Mtakatifu Colombano na wenzeke , walioweza kukabiliana na maji ya theruji na maji ya dhoruba kwa ajili ya kufuata Yesu, ndivyo Baba Mtakatifu amewaalika wote kuwa na ujasiri wa “kukabiliana na upepo wa dhoruba na vizingiti”.

Kuwatetea wadhaifu

Baba Mtakatifu kwa utambuzi wake juu ya mafundisho ya Yesu kuwa magumu kwa maana tendo la kusamehe aliyekujeruhi ni gumu amesema: Changamoto daima imekuwa ile ya kuwakaribihsa wahamiaji na wageni, Jinsi gani natoa uchungu na kukatidha tamaa kukataliwa au kusalitiwa! Jinis gani inaudhi kulinda haki za wadhaifu, ambao hawajazaliwa au wazee , ambao utafikiri wanaiba maana yetu ya uhuru. Kwa maana hiyo wao wanaweza kushirikishana Injili ya familia kama furaha ya Ulimwengu.

27 August 2018, 12:13