Maandalizi ya ziara  ya kitume ya Papa  mjini Dublin katika Mkutano wa Familia duniani Maandalizi ya ziara ya kitume ya Papa mjini Dublin katika Mkutano wa Familia duniani  

Bi Ghison:Tuishi mantiki ya mazingira ya kweli mahali tulipo!

Wakiwa na wosia huo mkononi wa Amoris Laetitia,wanafamilia wanashiriki katika mikutano mbalimbali kama vile meza ya mduara na kwa maana hiyo kila siku familia zinakabiliana na fadhila tatu za kitaalimungu, yaani imani, matumaini na upendo.

Sr. Angela Rwezaula - Vatican.

Katika kusubiri kuwasiri kwa Baba Mtakatifu Francisko Jumamosi 25 Agosti 2018, Wosia wa Kitume wa Amoris Laetitia ndiyo unaongoza kwa washiriki wote wa Mkutano wa Familia duniani mjini Dublin. Kati ya sura 9 za Amoris Laetitia, yaani Furaha ya Upendo ndani ya Familia, inaendelea kufanyiwa kazi yake  kwa siku tatu za Kongamano la kichungaji tangu 21-24 Agosti 2018, kwa kuudhuriwa  na washiriki 37,000 kutoka nchi 116 duniani.

Wakiwa na wosia huo mkononi wanashiriki katika mikutano mbalimbali kama vile  meza ya mduara na kwa maana hiyo kila siku familia zinakabiliana na fadhila tatu za kitaalimungu, yaani imani, matumaini na upendo. Katika kufafanua hayo, kwenye hotuba ya Linda Ghison, Katibu Msaidizi wa Baraza la Kipapa la Walei, Familia na Maisha, amesisitiza kuwa si kwa njia ya kufikiri tu,  na kama mkataba wa kitaalimungu, bali na kumaanisha maisha halisi ambayo “sisi wanafamilia tunavyoishi katika maisha ya kila siku, mahali pale pa dhati  tunaishi, kwa mantiki ya  mazingira ya kweli.

Mazungumzo, kukabiliana na kushuhudia

Mazungumzo, kukabiliana na kushuhudia ndiyo ufafafanuzi ambao Baba Mtakatifu, hachoki kusisitiza na kuomba kwa dhati kwa wote. Zaidi ya mambo mengi yanayo jikita ndani yake, bado kuna mtindo na namna ya Kanisa ambalo linatakiwa kujieleza na kujfafanua kama lilivyo, ameelezea Bi Ghison kwa wawakilishi wa kikundi ambacho yeye kama mratibu amepata kutafakari somo la Barua ya Mtakatifu Paulo kwa Wakorinto na kusisitiza juu ya Upendo ni fadhila kubwa kuliko zote kama Mtakatifu Paulo asemavyo!

Aidha amefafanua zaidi kuwa,Familia nyingi zinaishi kwa matatizo kila siku, ni hakika kwamba haitukuwa ni kufanya mazingaombwa ili yaweze kubadili familia mara baada ya mkutano na kuondokana na changamoto na matatizo ya kila siku, haitawezekana lakini jambo moja ni kwamba, “ iwapo tutakuwa tumeishi uzoefu wa Kanisa, kwa umoja bila hukumiana, na mahali ambapo kila mmoja anamtajirisha mwingine kwa  ushuhuda wake wa maisha, ni wazi kwamba tunaweza kupeleka nyumbani ule mtindo wa Kanisa ambao unasimamia msingi wa kuishi kwa umoja, kushirikishana, na  zaidi ya zana mbalimbali ili kuweza kuwa waaminifu katika wito wetu na kuwa kweli wenye furaha”,  amethibitisha Bi Ghison Katibu Msaidizi wa Baraza la Kipapa la Walei, Familia na Maisha!

24 August 2018, 15:29