Tafuta

Vatican News
Ziara ya XXIV ya  Kitume nchini Ireland katika Mkutano wa Familia Duniani Ziara ya XXIV ya Kitume nchini Ireland katika Mkutano wa Familia Duniani  (Vatican Media)

Papa amewatakia Rais amani,ustawi na baraka ya Mungu Mwenyezi!

Baba Mtakatifu ameingia uwanja wa ndege mida ya saa mbili asubuhi , hadi kufika mahali ambapo imewekwa ndege ya faragha kwa ajili yake A320, ijulikanayo Aldo Palazzeschi. Aliyekuwa anamsubiri katika uwanja wa ndege kimataifa Fiumicino ni viongozi wa serikali na kidini. Na ametuma telegram kwa marais wa nchi alizopitia akiwa juu angani.

Sr. Angela Rwezaula - Vatican 

Baba Mtakatifu ameingia uwanja wa ndege  mida ya saa mbili asubuhi na kuondoka na ndege namba  A320, inayojulikana "Aldo Palazzeschi. Aliyekuwa anawamsubiri Baba Mtakatifu katika Uwanja wa ndege  Kimataifa  Fiumicino ni viongozi wa serikali na dini, na kama kawaida ya tabasamu yake pamoja na mfuko wake mweusi mkononi mwake , amewasalimia kwa kupeana mkono na kuendelea kupanda ngazi  hadi kufikia kilele cha ndege ambapo kabla ya kuingia amegeuka na kuwapungia wote walio kuwa wanamsindikiza kwa macho na furaha.

Baada ya kufika ndani ya ndege kama kawaida ameingia  ndani na kuwasalimu hostess wawili na Rubani ambao walikuwa wanamsubiri. Baada ya kuwasalim hao amewageuka wengine na kuwapungukia mkono.

Kama desturi wakati wa safari yake kuelekea nchini Ireland ametuma Telegram kwa Rais wa Jamhuri ya nchi ya Italia , Bwana Sergio Mattarella. Katika Telegram ya Rais wa Italia imeandikwa: wakati ninaacha  Roma kuelekea Ireland kwenye  Fursa ya Mkutano wa Familia duniani, ninaombea taifa la Italia zawadi za kudumu, hekima kwa ajili ya kuendelea kuthamanisha na kulinda thamani ya ndoa na familia. Ninakutakia wewe na wahuduma wako heri katika shughuli za kuhudumia watu wa Italia ambao ninawatumia nao baraka.

Aidha Baba Mtakatifu pia ametuma telegram nyingine kwa Marais wa nchi zote anazopitia akiwa juu angani: Uswisi, Ufaransa na Uingereza ambapo amewatakia amani,ustawi na baraka ya Mungu Mwenyezi!

25 August 2018, 09:29