Tafuta

Vatican News
Ziara ya Baba Mtakatifu nchini Ireland katika Mkutano wa Familia duniani mjini Dublin Ziara ya Baba Mtakatifu nchini Ireland katika Mkutano wa Familia duniani mjini Dublin  (Vatican Media)

Papa: Sala iliyotungwa kwa ajili ya Mkutano wa familia duniani

Tusaide tuishi msamaha wako na amani yako. Utulinde familia zote kwa jina lako, hasa wale ambao sasa wanasali kwako. Tuongezee imani, tutie nguvu ya matumaini ili tudumishe upendo wako na kutambua daima kushukuru zawadi ya maisha ambayo tunashirikishana.

Sr. Angela Rwezaula - Vatican 

Mara baada ya tafakari ya Baba Mtakatifu Francisko wakati wa tamasha la Familia duniani, lililofanyika katika Uwanja wa Croke mjini Dublini  Jumamosi 25 Agosti 2018, imefuatia sala iliyotungwa kwa ajili ya Mkutano wa 9 wa Familia duniani , ambao unaongozwa na kauli mbiu Injili ya familia: Furaha ya ulimwengu ambapo Baba Mtakatifu amesali hivi:

Mungu Baba yetu, sisi ni ndugu kaka na dada katika Yesu Mwana wa Mungu wa familia moja, katika Roho ya upendo wako. Utubariki sisi sote kwa furaha ya upendo, ili tufanye tuwe wavumilivu na wema, wenye upendo na ukarimu, wanaokaribisha walio na mahitaji.

Tusaide tuishi msamaha wako na amani yako. Utulinde familia zote kwa jina lako, hasa wale ambao sasa wanasali kwako. Tuongezee imani, tutie nguvu ya matumaini ili tudumishe upendo wako na kutambua daima kushukuru zawadi ya maisha ambayo tunashirikishana. Tunaomba hayo kwa njia ya Kristo Bwana wetu. Amen.

Maria mama na kiongozi wetu, utuombee.

Mtakatifu Yosefu, baba na msimamizi wetu, utuombee.

Watakatifu Yohakimu na Anna, mtuombeee.

Watakatifu Luigi na Zelia Martin, mtuombee.

26 August 2018, 15:03