Tafuta

Maandalizi ya kumsubiri Papa Dublin yapamba moto Maandalizi ya kumsubiri Papa Dublin yapamba moto 

Familia mjini Dublin wanamsubiri Papa Francisko kwa shangwe kuu!

Katika umati wa watalii njini Dublin wamechanganyikana na makundi mbalimbali ya wahujaji na wanafamilia wengi, walio sindikizwa na maaskofu na mapadre. Familia nyingi kutoka nchi 116, wanashuhudia imani yao na kumsubiri kwa hamu kubwa kufika kwa Baba Mtakatifu Francisko Jumamosi 25 Agosti 2018 nchini Ireland!

Sr. Angela Rwezaula - Vatican. 

Katika kiangazi cha mwaka huu mjini Dublin kinajikuta katika masaa haya na sikukuu kubwa ambayo inajionesha katika rangi za benedera mbalimbali na sura zinazoonesha matumaini na furaha ya Mkutano wa Familia Duniani, ulio funguliwa tarehe 21 Agosti 2018. Katika umati wa watalii wamechanganyikana na makundi mbalimbali ya wahujaji, waliosindikizwa na maaskofu na mapadre. Familia nyingi kutoka nchi 116, wanashuhudia imani yao na kumsubiri kwa hamu kubwa kufika kwa Baba Mtakatifu Francisko Jumamosi 25 Agosti 2018 nchini Ireland

Ni nyimbo sala, na furaha kubwa ya watoto, ambazo zinasikika katika masaa haya kwa furaha ya kusubiri Papa na wakati huo huo, kongamano ya kichungaji ikiendelea katika vitengo mbalimbali vilivyoandaliwa na tume ya maandalizi. Njia atakayopitia Baba Mtakatatifu Francisko tayari imepambwa kwa Bendera ya Ireland na ya Vatican, kiasi cha kuufanya mji uoenekane  kweli na rangi zuri ya kuvutia ya furaha.

Lakini kwa wakati huo hu mji wote tayari umekwisha weka  ulinzi wa vyombo vya usalama, kwani hata watu wa kujitolea wanaonekana ni wengi katika msululu,  wakisindikiza watu na kwa hakika ni furaha katika mji wa Dublin. Familia ni nyingi hata wale ambao wamfika na watu wasiojiweza kutoka bara la Afrika India na kwingineko wanaonesha hata wao furaha yao, na hata mahitaji yao. Lakini kila kitu ikemepangwa katika mwanga wa sikuuu hiyo  hata kwa njia ya Neno la Mungu. Katika mikutano mbalimbali hadi sasa ambayo imepangiliwa kwa ajili ya mkutano wa familia duniani, wanaendelea kujikita katika tema mbalimbali hasa zinazo husu uzoefu na ushuhuda wa maisha ya kila siku.

Eamon Martin: Zawadi ya Maisha mpaya

Askofu Mkuu Eamon Martin wa Jimbo Kuu la Armage na Mkuu wa Kanisa la Ireland akizungumzia juu ya Wosia wa kitume wa Papa Francisko Amoris Laetitia, amejikita kwa kina katika hotuba yake juu ya zawadi kubwa ya maisha mapya. Amesisitiza juu ya kushangazwa kwa mfano wanawake na waamini walei, ambo kwao wengi ni mama na baba wamekuwa tayari kuwa sauti ya watoto ambao hawajazaliwa na wasio kuwa na sauti. Kadhalika amesema vijana wamezunguka, na kama vile apendavyo kusema Baba Mtakatifu Francisko juu ya utamduni wa ubaguzi, hata pia kuhusu mawazo ya uzazi wa mpango na kinyume na kuzaliwa.

Kuweni wamisionari kwasababu ya maisha

Kwa upande wa vijana ameongeza kusema Askofu Mkuu: imejitokeza hata tabia ya “mchanganyiko wa technokrania” yaani biashara ya mtoto kuzaliwa hata “bila kujali uhusiano wowote wa kijinsia”. Lakini anasisitiza, “iwapo sisi ni watu wanaoongozwa na Injili ya Maisha  na Injili ya familia, sisi wote tunaitwa kuwa “wamisionari kwa ajili ya maisha”, nyumbani  katika familia zetu, lakini pia katika parokia na maeneo ya kazi “.

24 August 2018, 14:58