Vatican News
Wanafamilia nchini Ireland katika maandalizi ya Mkutano wa Familia duniani Wanafamilia nchini Ireland katika maandalizi ya Mkutano wa Familia duniani  (Desmac1)

Familia ifuate kauli mbiu: Injili ya familia furaha ya ulimwengu

Padre F. Pesce mtaalam wa masuala ya familia na mtunzi wa kitabu cha Barua za Upendo,zinazojikita katika Amoris Laetitia anaeleza matunda yanayoweza kupatikana kutokana na Wosia wa Furaha ya Upendo ndani ya Familia kwa mtazamo wa Mkutano wa IX wa Familia huko Dublin, Ireland na kwa ujumla katika ulimwengu mzima.

Sr. Angela Rwezaula - Vatican 

Katika mahojiano na Padre Francesco Pesce mtaalam wa masuala ya kichungaji ya familia na mtunzi wa kitabu cha Baura za upendo “ kuhusu Wosia wa Kitume wa Amoris Laetitia yaani Furaha ya upendo ndani ya familia kuhusu Mkutano wa IX wa Familia duniani utakaofunguliwa Jumanne 21 Agosti 2018 na kufungwa tarehe 26 Agosti 2018, katika hitimisho la Misa Takatifu itakayoongozwa na Baba Mtakatifu Francisko. Anao mtazama mzuri kwa upande wa Mkutano na hata familia nzima ya Mungu!

Kwa familia nyingi duniani kwa wakati huu zimefika na wengine wanaendelea kufika ili kuweza kushiriki mkutano huo wenye maana kubwa mahali ambapo tukio hili linawadia mara baaya sinodi mbili kuhusu familia na kutangazwa kwa Wosia wa kitume wa Amoris Laetitia. Padre F. Pesce anaanza kuelezea juu ya matunda ambayo yanaweza kuwepo kuhusiana  na wosia huo, na kwamba ni matumaini yake kwamba familia kwa mara nyingine tena inaweza kuwa uthibitisho hai ya maisha ya ndoa.

Na pia kupongezwa kwa Kanisa ambalo limejikita juu ya familia na kama jinsi ilivyo, kila mara katika familia inapotambuliwa na kupongezwa kwa upande wa Kanisa kwa kile ambacho familia niafanya na jinsi ilivyo, ki ukwli ni kama kuanza kuvuta kwa upya hewa nzuri  na hivyo kwa upande wake anafarijika kwasababu kuna utambuzi kwamba  Kanisa ni kama jumuia na siyo kama taasisi nyingineyo.

Katika kusikiliza maoni juu ya Wosia wa kitume wa Amoris Laettia, anasema kwa upande wa familia wamesoma wosia huo na wanaendelea kuutafakari kwa kina, na kwamba inajionesha jinsi gani familia zinajihisi na  kujiuliza kwa jinsi gani wameweze kuishi jinsi walivyo, hivyo hayo si mapendekezo ya kutazama mtindo wa familia tofauti na kunyume ilivyo kwa thadi bali kutazamana kama  mfano wa familia hai ambayo inajitahidi jinsi ilivyo na yenye kuhitaji msaada wa kusindikizwa , kutambuliwa, kupendwa na kutiwa moyo.

Pamoja na hayo ni lazima kujikita katika matendo ya dhati hata kuweza kuwasindikiza  hatua kwa hatua katika hali inayowazunguka , kama vile katika  kujenga na kudumisha mahusiano yao, na kuipokea jinsi ilivyo. Kwa maana hiyo ni kuwatia moyo watembee kwa miguu yao kidete hatua moja baada ya nyingine iwezekanavyo, bila kuhukumu na kulaumu. Kadhalika jambo jingine anaongeza padre Pece:  kwa kusikiliza familia ambazo zimesoma Wosia wa Amoris Laetitia wanathibitisha kwa jinsi gani wosia huu umeweka kiini cha mahusiano ya wanandoa, hivyo wanandoa wanahisi kueleweka kwa dhati ndani ya Kanisa.

Kwa wana familia wakristo wote kama vile wa Ireland au kwa nchi za mashariki, wanaweza kusema nini katika mantiki ya mabadiliko ya ulimwengu  wa sasa hivi kama ilivyo huko Ireland na duniani kote, Padre Pesce anasema: kauli mbiu inayoongoza Mkutano wa familia, ni Injili ya familia , furaha ya ulimwengu, kwa maana hiyo anaamini  mwelekeo huo ndiyo mweleko huo huo unaowalenga familia ziweze  kujikita kuhudumia ulimwengu, si katika kutazama dunia kama inakwenda kinyume cha imani, au kutazama mabadiliko ya familia, badala yake kutazama dunia hiyo uwezekano wa kuijenga na kuibadili lakini kwa pamoja .Na njia ya kufanikisha hilo hasa ni ile ya kukutana kwa pamoja ili kuisaidia , kuinga jumuiya  hata ahusiano wake. Kulingana na kwamba dunia sasa imechanganikana yenyewe inawezekana kabisa kuifanya nyumba ya pamoja ya dunia na kufikiri kama wosia wa amaros Laetitia usemavyo ni “ lazima kwenda zaidi ya vizingiti vya nyumba yako.

Shughuli ya Padre Pesce ni kusindikiza, kuongoza na kuwa katikati ya maisha ya familia nyingi , kutokana na uzoefu huo kama padre wa familia amethibitisha jinsi gani anaendelea kupokea na kufanya uzoefu wa dhati wa maisha, uwezekano wa kufanya kazi na ubinadamu , kwa hatua inayowezekana na kuhakikisha ulazima wa kuwa na uvumilivu hasa katika kutoa muda, kijiweka karibu na kuongoza, lakini pia hata uwezekano mkubwa kwa kuona jinsi gani anapendwa yeye  hivyo jinsi alivyo!

20 August 2018, 14:58