Cerca

Vatican News
Madhabahu ya Mama Maria Kitaifa yaliyoko Knock nchini Ireland Madhabahu ya Mama Maria Kitaifa yaliyoko Knock nchini Ireland  (ANSA)

Mshikamano wa sala kwa wafungwa wa magereza nchini Ireland

Mara baada ya sala ya malaika wa Bwana, Baba Mtakatifu Francisko ametoa salam maalum kwa wanaume na wanawake ambao wamefungwa katika magereza ya Ireland. Anawawakikishia uwepo wake karibu kwa sala na familia zao.

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Kati ya mawazo ya Baba Mtakatifu Fracisko ni kwa ajili ya Ireland ya Kaskazini na ambapo anawahakikishia upendo wake na ukaribu wa sala. Ameyathibitisha hayo wakati wa sala ya Malaika wa Bwana tarehe 26 Agosti 2018 akiwa katika Mahdabahu ya Mama Maria wa Knock nchini Ireland. Baba Mtakatifu anasema, “Kwa furaha ya maendeleo ya kiekumene na maana ya kukuza urafiki na ushirikiano kati ya jumuiya za kikristo, Baba Mtakatifu anasisistiza kuwa, anasali ili wafuasi wa Kristo, waweze kupeleka mbele na katika msimamo wa thati zile nguvu kwa ajili ya kuendeleza mchakato wa amani na ujenzi wa jamii ya maelewano, umoja na haki kwa ajili ya watoto wa sasa”.

Mshikamano wa sala kwa wafungwa katika magereza nchini Ireland:

Mara baada ya sala ya malaika wa Bwana, Baba Mtakatifu Francisko ametoa salam maalum kwa wanaume na wanawake ambao wamefungwa katika magereza ya Ireland. Baba Mtakatifu Francisko amesema: Ninawakikishia uwepo na familia zenu ukaribu wangu na sala zangu. Mama Maria wa Huruma akeshe juu yenu na kuwapa nguvu katika imani na katika matumaini.

27 August 2018, 11:00