Tafuta

Hotuba ya kwanza ya Papa Francisko kwa viongozi wa serikali na kidiplomasia Hotuba ya kwanza ya Papa Francisko kwa viongozi wa serikali na kidiplomasia 

Papa:Amani ya kweli ni zawadi ya Mungu itokanayo na moyo ulioponeshwa!

Ninashukuru mapokezi ya kirafiki ambayo nimepokea kutoka kwa Rais wa Ireland. Ninawasifu pia uwepo wa wawakilishi wa Ireland ya Kaskazini. Ninamshukuru Bwana Waziri Mkuu kwa maneno yake. Kanisa kwa hakika ni familia moja na ambayo inahisi ulazima wa kusaidia familia katika juhudi za kutoa jibu kiaminifu na furaha katika wito waliopewa na Mungu ndani ya Jamii.

Sr. Angela Rwezaula- Vatican

Waziri Mkuu Taoiseach. Wajumbe wa Serikali na Wanadiplomasia, Bibi na Mabwana, mwanzo wa ziara yangu ya Ireland, ninayo furaha kukaribishwa  kuhutubia umati huu ambao unawakilishwa na maisha ya raia, utamaduni na dini ya nchi hii pamoja na wanadiplomasia na wenza wao. Ninashukuru mapokezi ya kirafiki ambayo nimepokea kutoka kwa Rais wa Ireland. Ninawasifu pia  uwepo wa wawakilishi wa Ireland ya Kaskazini. Ninamshukuru Bwana Waziri Mkuu kwa maneno yake.

Huo ndiyo umekuwa utangulizi wa hotuba yake ya kwanza Baba Mtakatifu Francisko mbele ya umati wa viongozi wa serikali na wanadiplomasia nchini Ireland tarehe 25 Agosti 2018. Katika hotuba yake, Baba Mtakatifu anaelezea jinsi gani wanavyotambua kuwa ziara yake katika nchi hiyo, inajikita kwenye  Mkutano wa Familia duniani ambao unafanyika mjini Dublin. Kanisa kwa hakika ni familia moja na ambayo inahisi ulazima wa kusaidia familia katika juhudi za kutoa jibu kiaminifu na furaha katika wito waliopewa na Mungu ndani ya Jamii. Na kwa ajili ya familia Mkutano huo ni fursa, si kwa jili  kuthibitsha kwao shughuli ya upendo mwaminifu tu, lakini pia usaidi wa pamoja, kuheshimu utakatifu wa zawadi ya Mungu ya maisha kwa kila mtindo wowote. Lakini pia hata kushuhudia nafasi moja pekee ya familia katika kuelimisha jamii na maendeleo kwa usafi wa uchanuzi wa kiungo cha ndani ya kijamii.

Ushuhuda wa kinabii

Baba Mtakatifu anasema: Ninapenda kuona Mkutano wa Familia dunia kama ushuhuda wa kinabii ulio na utajiri wa urithi wa thamnai za kimadili na kiroho ambayo ni kazi ya kila kizazi kutunza na kulinda.  Siyo lazima kuwa nabii ili kutambua  matatizo ambayo familia inakabilian nayo katika jamii ya sasa yenye mapinduzi ya haraka au wasiwasi wa upendo ambao umenyauka katika ndoa na katika maisha ya familia, ambayo siyo rahisi kuzuia mwenendo kwa kila ngazi  ya wakati endelevu ya jamii zetu. Familia ni umoja  wa jamii: wema wake hauwezi kutozingatiwa, lakini pia hata kuhamasisha, na kulinda kwa kila aina ya zana binafsi.

Kadhalika anasema: Ni katika familia, kila mmoja ameanza kutembe hatua ya kwanza ya maisha. Hapo ndipo tulijifunzia kuishi kwa utulivu, ndipo tulijifunza kuongoza na kutawala hisia zetu ubinafsi, kupatana na kila utofauti na zaidi kung’amua na kutafuta zile thamani ambazo zinatoa maana ya kweli, na ujazo wa maisha. Iwapo tunazungumza katika ulimwengu mzima kama familia moja, na kulewa wito wa umoja na katika mshikamano, hasa hasa inayotazama ndugu na kaka wadhaifu.

Baba Mtakatifu ameongeza kusema kuwa: Mara nyingi tuhahisi ukosefu wa uwezo mbele ya mabaya yanayozidi  kuongezeka hasa ya chuki ya ubaguzi na ukabila, migogoro na nguvu zisizo isha, kudharau hadhi ya kibinadamu na haki msingi,wakati huo huo, ongezeka kati ya tajiri na maskini. Ni mahitaji mangapi tunapaswa kuwa nayo kwa kila kitengo cha  maisha katika sera za kisiasa na kijamii, kwa maana ya kuwa familia moja ya watu! Na tusipoteze kamwe matumaini ya amani na ujasiri wa kuvumilia, bila kujiandaa kimaadili,  kuwa wahudumu wa amani, mapatano na walinzi wa mmoja na mwingine.

Changamoto za Ireland

Kutokana na hayo yote, nchini Ireland,changamoto zinapata kwa namna ya pekee wito, kwa kufikiria kipindi cha muda mrefu cha migogoro ambayo iliwafanya kutengena ndugu na kaka wa familia moja. Miaka 20 iliyopita Jumuiya ya kimataifa ilifuatia kwa makini matukio ya Kaskazini mwa Ireland ambapo waliweka mkataba wao siku ya Ijumaa Takatifu. Serikali ya Ireland katika umoja na Viongozi wa Kisiasa, kidini, na raia wa Ireland ya Kaskazini na Serikali ya Uingereza kwa msaada wa Viongozi wengine duniani walitoa maisha na mantiki inayotoa sura ya amani dhidi ya migogoro ambayo ilikuwa umesababisha mateso makali katika sehemu zote mbili.

Tunaweza kushukuru kwa miaka hiyo ya amani ambayo imeendeleza historia ya makubaliano, wakati huo huo tujieleza kwa uthabiti wa matumaini ambayo mchakato wa amani uweze kushinda kila aina ya kizingiti kilichobaki na kusaidia kuzaa mapatano, uwelewano na imani ya kweli kwa ziku zijazo. Injili inakumbusha kuwa amani ya kweli ndiyo zawadi ya Mungu na ya mwisho ambayo inatokana na moyo ulioponeshwa na kupatana, kwa kuendelea hadi kuikumbatia dunia nzima. Lakini inahitaji mchango wa sehemu yetu daima katika uongofu ambo ni kisima cha rasilimali ya kiroho na lazima kujikita kujenga jamii ya kweli ya mshikamano, haki na huduma kwa wema wa wote.

Changamoto inayosumbua dhamiri

Tunaweza kusema kiini cha kuwa na  matarajio ya kiuchumi au fedha inajionesha yenye kataka maisha ya kijamii iliyo sawa? Ni swali la baba Mtakatifu.  Haiwezekani kukua katika utamaduni wa ubaguzi na vitu ambavyo vinatufanya kuendelea kuwa utofauti mbele ya maskini ambao hawana mtetezi wa familia ya binadamu, ikiwa ni pamoja na wale ambao hawajazaliwa, wasio na kuwa na haki ya maisha? Labda changamoto zaidi inayojikita ndani ya dhamiri  katika nyakati hizi ni ile ya wimbi na kipeo cha wahamaji ambao lakini hatutegemei kwamba wataacha na wakati huo huo ,inahitajika suluhisho la hekima, kwa mtazamowa mapana  na mahangaiko ya kibadamu ambayo lazima yatatiwe uamniz wa kisiasa kwa muda mfupi.

Aibu ya manyanyaso ya kingono

Baba Mtakatifu akiendelea na hotuba yake, amebainisha kuwa, ana utambuzi wa hali halisi ya ndugu zetu kaka na dada ambao kwa namna ya pekee wanawake na watoto ambao kwa nyakati zilizopita wameteseka na hali haisi ya matatizo; yatima kwa wakati ule. Kwa kufikiriwa hali hiyo  zaidi ya wale waathirika, anasema: hatuwezi kutotambua fedheha zilizotokea nchini Ireland za manyanyaso ya kingono kwa upande wa watu wa Kanisa waliopewa majukumu ya kuwalinda na kuwaelimisha. Mbiu hii inagongwa  tena katika moyo wangu kwa maneno aliyosemwa katika uwanja wa ndege na Waziri kwa ajili ya watoto. Ninamshukuru sana kwa meneno yale.

Kushindwa kwa viongozi wa Kanisa, maaskofu, wakuu wa mashirika, mapadre na wangine, kukabiliana inavyotakiwa ule uhalifu wa kuchukiza, kwa haki umeibua hasira na inabaki sababu ya mateso na aibu kwa jumuiya katoliki.  Mimi mwenyewe Baba Mtakatifu Fracisko anabaisnisha: ninashirikishana na hisia hizi. Mtangulizi wangu Papa Benedikto XVI aliweze kusema maneno kuhusiana na ukuu wa hali hii: ni kujiuliza  kama kweli wangeweza kuthibiti “ ki ukweli katika Injili, haki na udhati katika jibu la kusaliti matumaini ( barua ya kitume kwa wakatoliki Nchini Ireland, 10). Shughuli yao na wazi ambayo inaendelea kusimamiwa hasa katika kujikita kwa juhudi ya viongozi wa Kanisa ili kuweza kuondoa makosa yaliyopita, kwa kutafuta zana muhimu za uthibiti na kuhakikisha kuwa yaliyotokea yasirudiwe tena. Hivi karibuni, ameongeza: katika Barua ya Watu wa Mungu, nimesisitiza juu ya shughuli kubwa ya kuweza kung’oa janga hili katika Kanisa; kwa gharama yoyote, kimaadili kwa mateso.

Mtoto ni zawadi yenye thamani ya Mungu

Kila mtoto ni zawadi yenye thamani ya Mungu, ni ya kulinda , kuitia moyo kwasababu zawadi hii iweze  kukuza na kufikia ukoamavu wa kiroho na ukamilifu wa kibinadamu. Kanisa la Ireland, limejikita katika nyakati zilizopita na sasa nafasi ya kuhamasisha wema wa watoto ambao hawezi kuachwa hivi.  Ni mategemeo yangu kuwa hali mbaya ya fedheha za nyanyaso ambazo zimefanywa na wengi, ziwe fundisho kutambua umuhimu wa kulinda watoto na watu wazima waathirika kwa upande wa jamii nzima. Kwa maana hiyo wote tunatambua dharura na ulazima wa kuwapatia vijana hekima katika kuwasindikiza na thamani safi kwa ajili ya safari yao katika makuzi.

Wapendwa, karibu miaka 90 iliyopita Vatican ilikuwa ya kwanza katika Taasisi ya kimataifza kutambua Uhuru wa Ireland. Kuanishwa kwa shughuli hiyo ya ushirikiano ulikuwa ni mwanzo wa miaka mingi ya umoja na ushirikiano unaondelea, kukiwa na kivuli kimoja kilichokuwa kinatembea mbele. Hivi karibuni, jitihadia za kina na utashi kwa pande zote mbili umetoa mchakatomkubwa na wenye maana na kuendeleza utajiri wa mahusiano kwa fmanufaa ya wote.

Nyuzi zile za kihistori ameendelea Papa Francisko: zinapelekea zaidi ya miaka 1500 iliyopita ambao ujumbe wa kikristo , ulioubiriwa na Palladio na Patrick, ambao ulipata makao katika nchi ya Ireland na kuwa sehemu fungamani ya maisha  na utamaduni wa Ireland.  Watakatifu wengi na wasomi, walihisi kuacha mikondo hii ya ardhi kupeleka kwa upya imani katika ardhi nyingine, Leo hii majina yao ni Columba, Colombano, Brigida, Gallo, Killian, Brendan na wangine wengi ambao wanaheshimiwa Barani Ulaya na kwingineko. Katika kisiwa hiki wamonaki, kama kisima cha ustarabu na ubunifu wa kisanii, uliandikwa sura nyingi na nzuri za historia ya Ireland na katika ulimwengu,

Leo hii kama ilivyo wakati uliopita, wanaume na wake walioishi katika nchi, wanajibidhisha kutajirisha maisha ya taifa kwa hekima iliyozaliwa katika imani. Hata katika masaa ya giza la Ireland, walitambua namna ya kuwa na imani ambayo ni kisima na ujairi, juhudi ambayo ni muhimu ili kukabiliana na wakati unaokuja wa huru, hadhi, haki na mshikamano. Ujumbe wa Kikristo umepata kufungamana na uzoefu ule na  kutoa mfumo wa lugha, mawazo na utamaduni wa watu wa kisiwa hiki.

Baba Mtakatifu ameitimisha hotuba yake: Ninasali ili Ireland, wakati inasikiliza  muziki wa pamoja wa majadiliano ya jamii kisiasa ya sasa, isisahau hata melodia nzuri  ya ujumbe wa kikristo ambao imeiongoza kwa nyakati zilizopita na inaweza kuendelezwa hata kufanya hivyo wakati endelevu. Na kwa mawazo hayo, ninawatakia Baraka juu yenu wote na watu wa Ireland kuwa na hekima, furaha na Amani. Asante.

 

25 August 2018, 16:43