Watoto waliocheza mbele ya Papa katika Uwanja wa Croke mjini Dublin Watoto waliocheza mbele ya Papa katika Uwanja wa Croke mjini Dublin 

Papa:hakuna familia iliyo kamili, msamaha unahitaji!

Kuangaza furaha ya upendo wa Mungu na kupeleka amani, iwe ndiyo ngao dhidi ya chuki na kusameheana, kwani bila msamaha, familia taratibu inaanguka. Muwe matumaini ya Kanisa na Ulimwengu. Ndiyo maneno ya wito wa Baba Mtakatifu alioutoa kwa maelfu ya wanafamiglia katika Uwanja wa Croke, Dublin tarehe 25 Agosti jioni

Sr. Angela Rwezaula - Vatican.

Mji wa Dublin kwa hakika umeishi kipindi cha furaha ya familia kutoka zaidi ya nchi 114. Na kweli katika Tamasha la Uwanja wa Croke mjini Dublini, mahali ambamo  watu 75,000  kwa mujibu wa waandalizi wa mkutano huo wamethibitisha, kwamba wamempokea Baba Mtakatifu Francisko kwa furaha kubwa! Bendera zikiwa zinapepea kila upande, nyimbo na ngoma, sauti za kila dunia, mavazi ya kila rangu kuwakilisha taifa, zimewasha mioyo ya kila mmoja katika uwanja huo.

Kadhalika ushuhuda wa baadhi ya  wanafamilia walio andaliwa kusimulia historia zao ambazo zilioneshwa kwa njia ya videozilisisimua umati mkubwa na baadaye kufuata hotuba ya baba Mtakatifu.  Na ndiyo katika sikukuu hii kilichokuwa kinasubiriwa kwa hamu kusikiliza  maneno ya Baba Mtakatifu Francisko ambayo yamelta furaha na kutia moyo. Hotuba yake, mara nyingi imekatishwa kwa kupigiwa makofi na ambayo inazingatia utume  wa familia katika ulimwengu wa leo, kuanzia tema ya Kauli mbiu ya Mkutano wa IX wa Familia duniani: Injili ya Famiglia, furaha ya Ulimwengu.

Katika hotuba yake Baba Mtakatifu anasema ushuhuda wenu katika Injili, unaweza kusaidia Mungu atimize ndoto yake. Mnaweza kuchangia na kufanya watoto wa Mungu wakaribie  na ili umoja ukue na kujifunza ni nini maana ya dunia nzima kuishi kwa amani kama familia moja na kubwa. Akizungumza  hivi bila kusoma, amewaomba wawabatize watoto wakiwa tangu wadogo kwasababu anasema, mtoto akiwa mdogo, roho Mtakatifu ni mwenye nguvu , anayo nguvu ya mungu ndani mwake.

Angazeni furaha ya upendo wa Mungu

Ili kuwa na furaha ya kweli katika ulimwengu, katika familia lazima kutafuta kuwa na Yesu. Familia kama taa lazima iangaze furaha ya upendo wa Mungu katika dunia, kwa maana ya kuonesha upendo huo, kwa njia ya ishara ndogo za wema wa maisha ya kila siku. Hiyo ina maana ya kuwa kama watakatifu walioko katika mlango ulio karibu, ambapo Baba Mtakatifu maranyingi anapenda kuelezea ya kuwa si jambo ambalo halitakiwi kupiga mbiu, lakini ni jambo ambalo lipo la kuweza kutenda kwa ukimya katika moyo wa familia zote ambao watoa upendo, msamaha na huruma.

 Ndoa ya kikristo na maisha ya familia, yanatambulikana uzuri wake wote iwapo umeshikamana na upendo wa Mungu. Hiyo ina maana kwa, Baba,mama na watoto, vijukuu, bibi,  hata mama wakwe na mawifi: kwa neema ya Mungu inawezekana kutambua na kusamehana hata kama siyo kitu rahisi. Ametoa mfano kuwa, kama jinsi unavyoandaa chai, inahitaji chujio na ndiyo maana inatakiwa muda na uvumilivu katika familia.

Msamaha

Baba Mtakatifu katika hotuba yake, ameweza kujibu maswali yaliyokuwa yanahusu ushuhuda wa wanafamilia walio tanguliwa. Mfano  Familia moja kutoka nchini Burkina Faso, wametoa ushuhuda kuhusu uzoefu wa msamaha. Kwa maana wameeleza jinsi gani walimzawadia mtoto wao, kuendesha kampuni yao binafsi ya ndege  na baadaye akaifilisi na yeye akapotea. Lakini baada ya siku nyingi wazazi hao, walikwenda kumtafuta mtoto wao na kuishi uzoefu wa mapatano. Hizi ni ishara ndogo na rahisi za msamaha, ambazo lazima zipyaishwe kila siku, kwa maana ni msingi ambao unajengeka katika msimamo wa ule  thabiti wa maisha ya familia ya kikristo anathibitisha Papa na kuongeza: mara nyingi tunataka kufanya amani lakini hatujuhi namna ya kufanya. Wakati huo huo inatosha tu ishara ndogo ya kubembeleza. Kutokana na hilo, Baba Mtakatifu amewaomba kurudia kwa lugha ya kingereza maneno matatu ambayo ni ufunguo wa familia: samahani, tafadhali na asante. Amani lazima kuitafuta  kabla ya kwenda kulala, kwasababu siku inayofuata itakuwa na vita baridi; Baba Mtakatifu amebainisha juu ya umuhimu huo wa kuomba msamaha mara moja bila kuchelewa.

Haipo familia iliyo kamili:

Kadhalika Baba Mtakatifu amesema hakuna familia iliyo kamili; bila kuwa na tabia ya kuomba msamaha, kwa maana bila msamaha, familia inakua ikiwa inaugua na taratibu inaanguka. Msamaha maana yake ni kutoa jambo moja muhimu na la binafsi. Kwa hakika watoto wanajifunza kusamehe wanapoona kwamba wazazi wao wanasamehana kati yao.

Familia na mitandao ya kijamii

Baba Mtakatifu akigusia juu ya ushuhuda wa Ted na Nisha wazazi ambao wamefika na watoto wao kutoka nchini India.  Kuhusu kiini cha uhusiano na mitandao ya kijamii ambayo Baba Mtakatifu amesema inaweza kuwa ya manufaa iwapo inatumika kimpangilio na hekima, lakini haipaswi kugeuka kuwa hatari katika mtandao wa mahusiano ya dhati, wa  mwili na damu, kwa kufuta hali halisi ya waketi. Maetoa mfano kwamba, kama vile, wakati watu wakiwa mezani, badala ya kuzungumza kati yao, wanatazama simu za mkononi. Historia ya familia wa India inaweza kwa namna moja kuwasaidia familia zote, kujiuliza juu ya mahitaji ili kupunguza wakati ambao wanautumia kwa ajili ya kutengeneza zana hizi za kiteckolojia na kuweza kutumia zaidi  muda mwafaka  kwa ajili  familia na Mungu.

Familia ni msingi dhidi ya chuki

 Ushuhuda wa wanafamilia wa nchi ya Iraq ambao ni wakimbizi nchini Australia, Baba Mtakatifu ametumia mfano katika kusisitizia kwamba, familia katika jamii inaleta amani kwasababu inafundisha upendo, kupokaribisha na kusamehe, mambo ambayo ni msingi mkuu dhidi ya kulipiza visasi. Kama walivyo fanya wao mara baada ya ndugu yao Padre Gianni kuwawa na wanamgambo nchi Iraq, waliona kwa dhati ya kuwa ubaya unaweza kupingwa tu kwa njia ya wema na chuki inaweza kushindwa kwa njia ya msamaha.

Upendo mwaminifu

Baba Mtakatifu anashukuru ushuhuda wa upendo na imani ya wanafamilia wa Ireland ambao wana watoto 10. Amesema ni vizuri kuwa na watoto kumi! Wazazi wao wakiwa vijana walikuwa wamedumbukia katika shimo la madawa ya kulevya, lakini waliondokana nayo. Upendo wa Kristo unao uwezo wa kubadilisha kila kitu, na ndicho chenye uwezo katika ndoa na upendo wa wanafamilia unaoundwa na uaminifu, usiogawanyika, umoja na kufungulia maisha. “Na ndiyo nilitaka kusisitiza katika sura ya nne ya Wosia wa Amoris Laetitia yaani Furaha ya Upendo ndani ya Familia! Baba Mtakatifu amebainisha.

Babu na bibi

Katika ushuhuda wa Aldo na Merisa: Wameishi ndoa yao zaidi ya miaka 50 wanatoka Canada na walikuwa pamoja na wajukuu zao. Uzoefu wao umetajwa na Baba Mtakatifu kuwa, katika jamii ambayo kwa sasa hawathamini babu na bibi ni jamii isiyo na wakati endelevu. Na Kanisa ambalo halina moyo wa mapatano kati ya kizazi litashia kukosa kwa dhati kile kinacho hesabiwa yaani upendo! Kwa maana hiyo ni lazima kuzungumza na wazee.

Watu wa kuhama hama wasibaguliwe (Nomadi

Ushuhuda wa Bi Missy Coliins, anayewakilisha familia za watu wa kuhama hama nchini Ireland ambao wanaishi kwa muda mrefu bila kuwa na haki, Baba Mtakatifu anaongeza kusema, lakini ni ambao katika meza ya Mungu nafasi ipo kwa kila mtu na hakuna ambaye anabaguliwa.

Sala ya Maalum na Wosia wa Amoris Laetitia

Muwe na matumaini ya Kanisa na Ulimwengu, amehitimisha Baba Mtakatifu na kwa maana hiyo amependelea kuwakabidhi wote walioudhuria mkutano huo, wosia wa Amoris Laetitia ambapo amekumbusha kuwa ameuandika ili uwe kama kiongozi katika kuishi furaha ya Injili  katika familia

Na baadaye amepmba wasali sala maalumu iliyotungwa kwa ajili ya Mkutano wa familia duniani: Mungu Baba yetu, sisi ni ndugu kaka na dada katika Yesu Mwana wa Mungu wa familia moja, katika Roho ya upendo wako. Utubariki sisi sote kwa furaha ya upendo, ili tufanye tuwe wavumilivu na wema, wenye upendo na ukarimu, wanaokaribisha walio na mahitaji.

Tusaide tuishi msamaha wako na amani yako. Utulinde familia zote kwa jina lako, hasa wale ambao sasa wanasali kwako. Tuongezee imani, tutie nguvu ya matumaini ili tudumishe upendo wako na kutambua daima kushukuru zawadi ya maisha ambayo tunashirikishana. Tunaomba hayo kwa njia ya Kristo Bwana wetu. Amen.

Maria mama na kiongozi wetu, utuombee. Mtakatifu Yosefu, baba na msimamizi wetu, utuombee. Watakatifu Yohakimu na Anna, mtuombeee. Watakatifu Luigi na Zelia Martin, mtuombee.

27 August 2018, 09:01