Tafuta

Kristo Yesu ni chemchemi ya maisha ya uzima wa milele Kristo Yesu ni chemchemi ya maisha ya uzima wa milele 

Mh. Padre Martin Boucar Tine ateuliwa kuwa Askofu wa Kaolack, Senegal.

Askofu mteule Martin Boucar Tine alizaliwa tarehe 16 Septemba 1966 huko Koudiadiène, Jimboni Thiès. Baada ya masomo, malezi na majiundo yake ya kitawa na kipadre huko Kinshasa, DRC., tarehe 6 Okoba 1995 akaweka nadhiri zake za daima na kupewa Daraja Takatifu ya Upadre hapo tarehe 6 Julai 1996.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. - Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko amemteua Mheshimiwa sana Padre Martin Boucar Tine, S.S.S., Makamu Mkuu wa Shirika la Sakramenti kuu, kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki la Kaolack, nchini Senegal. Askofu mteule Martin Boucar Tine alizaliwa tarehe 16 Septemba 1966 huko Koudiadiène, Jimboni Thiès. Baada ya masomo, malezi na majiundo yake ya kitawa na kipadre huko Kinshasa, DRC., tarehe 6 Okoba 1995 akaweka nadhiri zake za daima na kupewa Daraja Takatifu ya Upadre hapo tarehe 6 Julai 1996.

Baada ya Upadrisho katika maisha na utume wake, amewahi kuwa Paroko-usu; mlezi wa Wapostulanti huko Dakar, nchini Senegal. Kati ya mwaka 1999 hadi mwaka 2001 alipelekwa na Shirika lake kwa masomo ya juu huko nchini DRC na kujipatia shahada ya uzamili kwenye taalimungu ya mafundisho sadikifu ya Kanisa. Kati ya mwaka 2001 hadi mwaka 2006 akateuliwa kuwa Mkurugenzi wa Kituo cha Elimu ya juu cha Emmaus, kilichoko Kinshasa, nchini DRC.. Kati ya mwaka 2006- 2011 akachaguliwa kuwa Padre mkuu wa Kanda wa Shirika la Sakramenti kuu nchini Senegal.

Kati ya mwaka 2008 – 2011 akateuliwa kuwa Rais wa Mashirika ya Kitawa na Kazi za Kitume nchini Senegal. Baadaye, akateuliwa pia kuwa Paroko-usu; mjumbe wa Halmashauri kuu ya Shirika na mratibu wa majiundo ya Mapadre wa Shirika kutoka Afrika. Mwaka 2017 akateuliwa kuwa Makamu mkuu wa Shirika la Sakramenti kuu.

 

25 July 2018, 15:42