Tafuta

Vatican News
Baba Mtakatifu Francisko wakati wa Katekesi yake, Jumatano Baba Mtakatifu Francisko wakati wa Katekesi yake, Jumatano  (Vatican Media)

Papa Francisko asema, Ukristo ni safari ya ukombozi

Baba Mtakatifu Francisko katika katekesi yake kila Jumatano, ameendelea kufafanua kuhusu Amri za Mungu kama muhtasari wa safari ya maisha ya Kikristo inayomwajibisha mwamini kujikita katika kutekeleza Amri za Mungu kama dira na mwongozo wa maisha adili na matakatifu.

Na Sr. Angela Rwezaula. - Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko amesema, Katika ukumbi wa Paulo VI kuna watu wengi wagonjwa ili waweze kujizuia jua kali na joto na  kukaa vema pale. Pamoja na hayo watafuatilia  moja kwa moja na sisi hapa, kwa maana hakuna katekesi mbili bali moja, na hivyo nituwasalimie wagonjwa walioko katika Umbi wa Paulo VI....  Tuendelee kuongea juu ya amri kama ambavyo tumekwisha kusema kuwa, amri ni maneno ya Mungu aliyo wapatia watu ili wapate kutembea vema; ni maneno ya upendo wa Baba. Maneno ya amri kumi yanaanza hivi:” Mimi ni Bwana, Mungu wako, niliyekutoa katika nchi ya Misri, katika nyumba ya utumwa”(Kut 20,2), Mwanzo huo utafiriki ni a  kiajabu katika sheria ya  kweli na zile ambazo zinafuata lakini japokuwa siyo hivyo.

Ndiyo utangulizi wa maneno ya Baba Mtakatifu Francisko  aliyo anza nayo wakati wa katekesi yake Jumatano tarehe 27 Juni 2018 kwa mahujaji na waamini wote waliofika katika kiwanja cha Mtakatifu Petro kusikiliza katekesi hiyo ambayo inajikita katika mwendelezo wa tafakari ya Amri za Mungu na iliyotanguliwa na somo kutoka katika Kumbukumbu la Torati: “Je! Watu wakati wo wote wameisikia sauti ya Mungu ikinena toka kati ya moto, kama ninyi mlivyosikia, wasife?  Au Mungu amekwenda wakati gani akajitwalia taifa toka kati ya taifa lingine, kwa majaribu, na kwa ishara kwa maajabu, kwa vita,na kwa nguvu yake kuu, akasababisha mambo ya kutisha ambayo ninyi mlishuhudia kwa macho yenu kule Misri. Ninyi mlijaliwa kuyaona mambo hayo, ili mpate kutambua kwamba Mwenyezi-Mungu ndiye peke yake na wala hakuna mwingine.  (Torati 4,32-35).


Baba Mtakatifu Francisko akiendelea na ufafanuzi anasema: Je ni kwanini kutangaza jambo hili  na kuokoa? Ni kwa sababu walifika  chini ya Mlima Sinai,  mara baada ya kuvuka katika Bahari ya Shamu, Mungu wa waisraeli kwanza aliwakomboa na baadaye akawaomba wawe waaminifu. Kwa maana hiyo amri kumi zinaanza na na ukarimu wa Mungu. Mungu kamwe  haombi bila kutoa kwanza. Na ndiyo Baba yetu na Mungu mwema Baba Mtakatifu anathibitisha. 

Kutokana na hilo  ndipo tunaweza kutambua umuhimu wa tangazo la kwanza lisemalo “Mimi ndimi Mungu wako”. Hapa ni kuonesha mamlaka aliyo nayo Mungu juu yetu , kuna uhusiana ambao unatuhusu, kwa  maana Mungu siyo mgeni,ni Mungu wako. Tangazo hili linaangazia amri kumi zote na kuonesha hata siri ya utendaji wa mkristo,na  ndiyo tabia ya Yesu mwenyewe akithibitisha pia: “ Kama vile Baba alivyonipenda mimi, nami nilivyo wapenda ninyi, kaeni katika pendo langu (Yh 15,9). Kristo ni pendo la Baba na anatupenda kwa upendo ule ule. Hakujileta yeye mwenyewe bali ni Baba. Akifafanua zaidi ametoa mfano kuwa, mara nyingi shughuli zetu zinaharibika kwa sababu tunatanguliza nguvu zetu na siyo kutokana na shukrani. Je anaye anzaia kwake atafika wapi?; atajifikia yeye binafsi ! kwa maana hana uwezo wa kutengeneza njia. Anajizunguka yeye mwenyewe. Na ndiyo tabia ya ubinafsi ambayo katika kutania watu utasikia wanasema “mtu yule anajiona kwa sababu anatoka ndani yake na kujirudia.

Maisha ya mkristo hawali ya yote ndiyo jibu la shukrani ya Baba mkarimu. Wakristo ambao wanafuata tu majukumu binafsi, hawana uzoefu binafsi wa kukuta na Mungu ambaye ni Baba Yetu. Hiyo ni kutokana na kwamba wanajikuta wakifikiria kufanya hiki na kile kwa maana ya majumu tu. Lakini wanakosa jambo fulani! Je ni msingi gani wa majukumu? “ninapasw kufanya kile….?Hapana: Baba Mtakatifu anatoa jibu kwamba, msingi wa majukumu hayo ni upendo wa Mungu Baba, ambaye kwanza anatoa na baadaye anaamuru. Na licha ya hayo kupendekeza sheria kwanza katika mahusiano haisaidi njia ya imani!

Je, ni kwa njia gani kijana anaweza kuwa na shauku ya kuwa mkristo iwapo tunaanzia katika kulazimisha, shughuli, uthabiti na siyo kuanzia katika kutoa uhuru? Japokuwa  kuwa mkristo ni njia ya uhuru! Amri za Mungu zanatoa uhuru wa kweli ili kujikwamua  na ubinafsi, hatimaye kuwa huru kwa sababu kuna upendo ambao unakupeleka mbele. Mafunzo ya kikristo hayajikiti juu ya nguvu ya utashi, bali kwa njia ya kukaribisha wokovu na kuachwa upendwe kama vile  Wasraeli kabla ya kuvuka  Bahari ya Shamu na baadaye chini ya Mlima wa Sinai. Kwanza ni wokovu ambao Mungu anawaokoa watu wake kupitia Bahari ya Shamu na baadaye katika mlima wa Sinai anawaelekeza nini cha kufanya. Watu hao wanatambua kuwa mambo anayo yanafanyika kwasababu wamekombolewa na Baba anayewapenda.

Baba Mtakatifu anasema kuwa, shukrani ni  tabia ya moyo uliotembelewa na Roho Mtakatifu; na ili kutii Mungu lazima hawali ya yote kukumbuka mema yake aliyokutendea. Mtakatifu Basilio anasema: Asiye anguka katika majaribu ya kusahau mema ya Mungu, anao mwelekeo wa fadhila njema na kujikita kwa  kila kazi ya haki (rej. Kanuni fupi, 56). Je, inatupeleka wapi ? inatupeleka kufanya mazoezi ya kumbukumbu, kama vile: ni mambo mangapi Bwana ametenda kwa kila mmoja wetu! Jinsi gani Baba wa Mbinguni  ni mkarimu!

Mara baada ya kutoa mifano hiyo, Baba Mtakatifu amewataka wafanya zoezi dogo, hasa la kukaa kimya wote na kujiuliza mioyoni mwao juu ya mambo gani mema ambayo Mungu ametenda, na kwa kimya kila mmoja ajibu kimoyo moyo…. Huo ndiyo uhuru wa Mungu, kwa maana Mungu anafanya mambo mengi mazuri na kuokoa. Lakini wakati mwingine Baba Mtakatifu amebainisha kuwa  unaweza usihisi kufanya uzoefu wa kweli wa huru wa Mungu na hiyo kwa kawaida inatokea na sababu ni nyingi kama vile,inawezakana kwamba mara baada ya kutazama dhamiri, unakuta kuna nafasi ya kuwajibika tu, tasaufi ya utumwa na siyo ya wana! Je, kutokana na hili inabidi kufanya nini? Baba Mtakatifu Francisko ametao jimbu kwamba ni lazima kufanya kama walivyofanya wana wateule. Kitabu cha Kutoka kinasema: “Wana wa Israeli wakaugua kwa sababu ya ule utumwa, wakalia; kilio chao kikafika juu kwa Mungu kwa sababu ya ule utumwa. Mungu akasikia malalamiko, Mungu akakumbuka agano lake alilolifanya na Ibrahimu na Isaka na Yakobo. Mungu akawaangalia  hali za wana wa Israeli na kufikiria (Kut 2,23-25). Kwa maana hiyo Mungu anafikiria hata mimi! 

Tendo la kukombolewa na Mungu, alilotoa mwanzo wa Amri kumi , ndiyo jibu dhidhi maombolezo.  Sisi hatuwezi kujikomboa sisi wenyewe, lakini kwa kuanzia katika kilio kinasaidia na kusema: Bwana niokoe, nifundishe njia zako, Bwana nipe faraja, Bwana nipe furaha kidogo. Baba Mtakatifu anathibitisha ndicho kilio ambacho kinasaidia.  Hivyo inategemea na sisi kuomba neema hiyo ya kuondokana na ubinafsi, dhambi na  minyororo ya utumwa. 
Hicho ndiyo kilio muhimu, ni maombi na utambazi ambao unahitajika ili kuweza kukombolewa ndani mwetu. Kuna mambo mengi ndani ya roho zetu  ambayo yahitajika kukombolewa, kwa maana hiyo ni kuomba. 

Akihitimisha Baba Mtakatifu Francisko  amesema: niokoe, nisaidie na nipe uhuru” ndiyo sala ya Bwana. Mungu anasubiri kilio kile kwa maana anaweza na anataka kuvunja vunja minyororo: Mungu hakutuita katika maisha haya  ili tubaki tumeelemewa, badala yake ili tuwe huru na kuishi kwa shukrani, kwa kumtii, kwa furaha yake  Yeye ambaye ametupatia mengi yasiyo pimika na ambayo hatuwezi kamwe kumrudishia. Ni vizuri jambo hili na hivyo Mungu aweze daima kutukuzwa kwa kile ambacho alitenda na atatenda kwa ajili yetu.

 

27 June 2018, 08:36