Cerca

Vatican News
2018.06.27 Udienza Generale Baba Mtakatifu Francisko wakati wa katekesi yake Siku ya Jumatano  (Vatican Media)

Papa Francisko aanza mzunguko mpya wa katekesi: Amri za Mungu!

Amri za Mungu ni muhtasari na mwongozo wa maisha adili ambayo mwamini anapaswa kuufuata ili aweze kujipatia maisha ya uzima wa milele. Hii ni zawadi ya Agano kati ya Mungu na taifa lake na ni katika Agano la Kale Amri za Mungu zinapata maana yake ya kweli ndani na kwa njia ya agano hilo. Yesu amekazia umuhimu wa kumwilisha Amri hizi katika matendo!

Na Sr. Angela Rwezaula. - Vatican

“Hata alipokuwa akitoka kwenda njiani, mtu mmoja akaja mbio, akampigia magoti, akamwuliza, Mwalimu mwema, nifanye nini nipate kuurithi uzima wa milele? Yesu akamwambia, Kwa nini kuniita mwema? Hakuna aliye mwema ila mmoja, ndiye Mungu. Wazijua amri, Usiue, Usizini, Usiibe, Usishuhudie uongo, Usidanganye, Waheshimu baba yako na mama yako. Akamwambia, Mwalimu, haya yote nimeyashika tangu utoto wangu. Yesu akamkazia macho, akampenda, akamwambia, Umepungukiwa na neno moja. Enenda, ukauze ulivyo navyo vyote, uwape maskini, nawe utakuwa na hazina mbinguni; kisha njoo unifuate” (taz. Mk 10,17-21)

Ndugu wapendwa habari za asubuhi, … Ni sikukuu ya Mtakatifu Anthoni wa Padua. Kuna yoyote anayeitwa Anthoni?.... , kwa wote wanaoitwa Anthoni tuwapigie makofi…  leo hii tunaanza safari mpya ya Katekesi. Itakuwa inahusu mada ya amri za Mungu. Katika utangulizi tutumie neno la Mungu lilisomwa: mkutano kati ya Yesu una mtu aliyepiga  magoti akiomba kufahamu ni jinsi  gani ya kufanya ili  apate kuurithi ufalme wa Mungu (taz. Mk 10,17-21). Katika swali hilo, kuna changamoto za kila maisha yaani shauku ya maisha kamili na yasiyo na mwisho. Je ni kufanya nini ili kuweza kufikia? Ni kuingia kiukweli na maisha yenye heshima kubwa. Je ni vijana wangapi wanatafuta kuishi na wanajiharibu kwa kufuata mambo yanayopita tu kwa siku moja.

Ni utangaulizi wa tafakari ya Katekesi ya Baba Mtakatifu Francisko, tarehe 13 Juni 2018, kwa mahujaji na waamini kutoka pande zote za dunia waliounganika kwa pamoja kumsikiliza katika viwanja vya Kanisa kuu la Mtakatifu Petro Mjini Vatican ambapo ametoa utangulizi wa Mada nyingine mpya kuhusu Amri za Mungu. Katekesi hii imeongozwa na Neno la Mungu Kutoka Injili ya Mtakatifu Marko 10,17-21, inayoeleza mtu mmoja aliyekuja mbio na kumpigia magoti, akiuliza afanye nini ili apate kuurithi uzima wa milele.

Baba Mtakatifu akiendelea na fafanuzi yake amesema, wengi wanafikifiria ni bora kuzima hakika hamu hiyo kwasababu ni  hatari. Amethibitisha, hasa akilenga vijana kwamba kwamba adui mbaya zaidi siyo matatizo ya kweli, pamoja na majanga yake yaliyopo. Hatari kubwa zaidi ni ile ya kuwa na  roho mbaya na kuridhika tu , wakati huo siyo kwa si kwasabu ya  upole au unyenyekevu, badala yake ni kiasi, uhafifu na unyonge.  Kijana mnyonge ni kijana asiye kuwa na wakati endelevu, anakaa anajisahau na hakui, pia kamwe hatakuwa na mafanikio.  Vijana kama hao wanayo hofu ya kila kitu, kwani wanajisema sisi tuko namna hiyo.Na hivyi  inahitaji kweli kuwa na moyo wa nguvu na siyo uhafifu na kiasi.

Mwenye heri Pier Giorgio Frassati alikuwa ni kijana ambaye alikuwa akisema kwamba, lazima kuishi na siyo kujizeesha kwa maana watu wafifu wanazeeka, kwa maana hiyo ni kuishi kwa nguvu ya maisha. Ni lazima kuomba Baba wa mbinguni kwa ajili ya vijana leo hii  ili wapate zawadi kamili ya shauku, na uwezo wa kutokuridhika tu na maisha bila uzuri na bila rangi. Iwapo vijana hawatakuwa na njaa ya maisha ya kweli, ubinadamu utakwenda wapi? Anauliza Baba Mtakatifu Francisko. Je ubinadamu huu na vijana wenye mashaka na mahangaiko wataishia wapi?

Swali la mtu yule katika Injili, liko ndani ya kila mmoja: Je maisha kamili yanapatika namna gani?,  Yesu anajibu “wewe wazijua amri”, na alitaja sehemu ya amri za Mungu.  Ni mchakato wa mafunzo ambayo Yesu anataka kumwongoza  mahali pa dhati,  hiyo ni wazi kutokana na swali la mtu huyo, ambaye hana maisha kamili. Je ni jambo gani kwa hakika napaswa kutambua? Mara baada ya kujibu: Mwalimu, haya yote nimeyashika tangu utoto wangu, (Mk 10,20).
Ni jinsi gani ya kutoka katika  hatua za ujana kuekekea  katika ukomavu? Baba Mtakatifu anajibu kwamba, unapoanza kukubali vizingiti vyako. Unakomaa unapokuwa na utambuzi na uelewa wa kile ambacho unakosa, maana Yesu alimkazia  macho, akampenda, akamwambia, umepungukiwa na neno moja (Mk 10,21)…. Mtu huyo sasa amelazimika kutambua kila kitu ambacho anapaswa kufanya , na Baba Mtakatifu anatoa mfano kuwa hakizidi paa la nyumba na wala kwenda  ukingoni. Lakini ni jinsi gani ilivyo vema kuwa wanaume na wanawake; jinsi gani ilivyo na thamani kuu ya maisha! Pamoja na hayo kuna ukweli kwamba katika historia ya karne za mwisho, mtu daima amekataa na matokeo yake mabaya katika ukweli wa vizingiti vyake.

Yesu katika Injili anataja jambo ambalo linaweza kutusaidia;   Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua torati au manabii; la, sikuja kutangua, bali kutimiliza. (Mt 5,17). Bwana Yesu anatoa zawadi ya ukamilifu na ndiyo maana alikuja. Mtu yule alikuwa anatakiwa afike katika upeo, mahali ambapo panafungua uwezekano wa kuacha kuishi kibinafsi kama vile shughuli zake, mali zake na ndiyo maana alikuwa anapungukiwa maisha timilifu, hakuna na pendekezo la kujali maskini, badala yake  alipendelea utajiri wa kweli. Yesu akamwambia, Umepungukiwa na neno moja. Enenda, ukauze ulivyo navyo vyote, uwape maskini, nawe utakuwa na hazina mbinguni; kisha njoo unifuate (taz. Mk 10,21).

Ni nani anaweza kuchagua kati ya asili na kopi?, baba Mtakatifu anaongeza,  tazama ndiyo changamoto ya kutafuta kitu asili na siyo kopi. Yesu hatoi mfano na kopi, Yeye  anatoa ukweli wa maisha, upendo wa kweli na utajiri wa kweli!  Ni jinsi gani vijana wanaweza kufuata imani iwapo hawaoni mfano halisi wa kuchagua, iwapo hawaoni vipimo vya kutosha?  Ni mbaya sana kukutana na wakristo wenye vipimo, Baba Mtakatifu ameomba samahani kutumia mfano wa watu wafupi sana ambao wanakua kiasi fulani na kuishia hapo, lakini  akiwa maana ya kuelezea juu ya ukiristo ambao hautakiwi kuishi na mioyo mifinyu .iliyofungwa, badala yake anasema ni mbaya sana kukutana na wakristo wa namna hiyo. Inahitaji mifano ya mtu ambaye anawaalika kwenda zaidi ya. Mtakatifu Ignatius alikuwa akiita moto wa kuchochea shauku ya  kufanya matendo ambayo ni wazi na yanakwenda sambamba na maisha kamili ya mkristo.

Njia inayokosekana, inapitika na kile kichopo.Yesu hakuja kutengua torati  au manabii, bali kuikamilisha. Tunapaswa kuanzia katika hali halisi ili kuruka kile kinachoksekana. Tunalazimika kuchanganua yanayotakiwa  na kujifungulia yale ya kawaida.  Katika katekesi hizi,  Baba Mtakatifu amesema, atajikita kuelezea amri alizopewa  Musa na kuwapatia wakristo. Na ili kwa kushikana mikono na Yesu kupitia maisha ya muda kama yale ya ujana hadi kufikia tunu iliyoko  mbinguni wote wakiwa nyuma yake. Watagundua kila aina ya amri ya zamani, hekima na  mlango uliofunguliwa na Baba ambaye yupo mbinguni kwa sababu Bwana Yesu alipitia, na ambaye anatupatia maisha ya kweli na ni maisha ya watoto wa Mungu.13 June 2018, 09:00