Karika Misa ya Papa Francisko amesistizia juu ya amani itokayo kwa Yesu na ile ya ulimwengu isiyozaa matunda. Karika Misa ya Papa Francisko amesistizia juu ya amani itokayo kwa Yesu na ile ya ulimwengu isiyozaa matunda. 

Papa amesali kwa ajili ya wauguzi mfano wa ushujaa.Amani ya Yesu inatufungua kwa wengine!

Katika Ibada ya Misa ya asubuhi kwenye kikanisa cha Mtakatifu Marta,Papa Francisko ameomba Mungu abariki wauguzi ambao katika kipindi hiki cha janga wamekuwa mfano wa kishujaa na baadhi wamepoteza maisha yao.Katika mahubiri amesisitiza kuwa amani ya Yesu ni zawadi ya bure ambayo inafungulia kwa wengine daima na kutoa matumaini ya Mbingu ambayo ni amani ya mwisho na wakati amani ya ulimwengu ni ya ubinafsi,isiyozaa matunda na ya kitambo.

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Jumanne asubuhi, tarehe 12 Mei 2020, Papa Francisko ameadhimisha Ibada ya Misa katika Kikanisa cha Mtakatifu Marta mjini Vatican ikiwa ni Wiki ya tano ya Pasaka. Katika utangulizi wa misa hiyo mawazo yake yamewaendea wauguzi katika siku ambayo ni kilele kumbukumbu ya kimataifa ya wauguzi. Papa Fransiko amesema “Leo ni Siku ya Wauguzi. Jana nimetuma ujumbe. Tuombe leo hii kwa ajili ya wauguzi wote, wanaume na wanawake, vijana wa kike na kiume, wenye taaluma hii ambayo ni zaidi ya taaluma; ni wito ni kujitoa. Na Bwana awabariki. Katika kipindi hiki cha janga wameonesha mfano wa kishujaa na baadhi wamepoteza maisha yao. Tuwaombee wauguzi wa kike na wa kiume”.

Amani ya dunia inakutengenisha na wengine

Katika mahubiri ya Papa Francisko ametafakari Injili ya siku kutoka Yohane 14,27-31 ambapo Yesu anawambia wafuasi wake kuwa “ Amani nawaachieni, Amani yangu Niwapavyo sivyo kama ulimwengu utoavyo”. Ameongeza, “Bwana kabla ya kuondoka zake aliwapatia zawadi ya amani. Hii siyo kama amani ya ulimwengu, amani bila vita ambavyo tunatamani, bali ni amani ya moyo. Bwana anatoa amani na sivyo kama ulimwengu utoavyo”. Hii ni amani tofauti. Ulimwengu unatoa amani ya kiundani kama ile ya kutaka kumiliki, kama vile ya jambo ni la kwako ambalo linakutengenisha na wengine; ni kama vile umeinunua na unajifungia ndani ya amani hiyo. Ni amani ya kwako binafsi inayokufanya utulie na kuwa na furaha, lakini inakufanya usinzie kama mwenye ngazi. Papa ameongeza kusema, ni kama kidogo ya  ubinafsi. Ni amani inayokugharimu kwa maana inahitaji ubadilishe kila wakati zana za amani, inabidi kila wakati utafute zana za kuinunua; haizai matunda na ya kitambo tu.

Amani ya Yesu inakuweka katika mwendo na haikubagui

Amani ya Yesu inakuweka katika mwendo, haikubagu, inakufanya uende kwa wengine, inakufanya uwasiliane. Amani ya Yesu ni ya bure ni zawadi  ni matunda, inakupeleka mbele daima. Hata hivyo Papa Francisko kwa kusisitizia juu ya hilo amekumbusha kuwa “Amani ya ulimwengu imeelezwa hata katika sehemu ya Injili, mahali ambapo inazungumzia yule mtu aliyekusanya mazao katika ghara lake la ngano na kuamini kuwa mwenye furaha na hatimaye mwenye nguvu na kupumzika, lakini usiku ule ule Mungu akamwambia mjinga wewe, leo hii utakufa”. Amani ya ulimwengu  ni amani ya kitambo ambayo haikufungulii mlango wa upeo, kinyume chake amani ya Yesu iko wazi imefungua Mbingu kwa ajili yake na kwa ajili ya wengine.

Mwaliko wa kujitazama ndani binafsi kuhusu amani

Papa Francisko amewalika waamini kujitazama ndani binafsi  juu ya amani na kutoa maswali ya kujiuliza: “je ninapata amani kutoka wapi? Katika mambo, katika ustawi, katika umiliki au ninapata amani kama zawadi ya Bwana? Ninatakiwa nilipe kwa ajili ya amani au niipokee bure kutoka kwa Bwana? Ikiwa ninakasirika ninapokosa kitu, hii ni udhihirisho kuwa sina amani ya Bwana. Je nina amani na ninataka kuwatangazia wengine na kupeleka mbele jambo lolote? Na hiyo ndiyo amani ya Bwana, Papa amesisitiza. Anaongeza, hata katika wakati mbaya sana  na mgumu, amani inabaki ndani mwangu? Ni amani ya Bwana. Na amani ya Bwana inaleta matunda hata kwa ajili yangu na imejaa matumaini, kwa kutazama Mbingu.

Papa Francisko akiendelea kueleza amani amesimulia jinsi alivyopokea barua jana kutoka kwa Padre mmoja mwema ambaye alimwambia kuwa yeye anazungumza kidogo kuhusu Mbingu na wakati anatakiwa azungumzie sana. Kwa kuongeza Papa amesema “Anayo sababu na ndiyo maana leo hii nimependelea kusisistizia hili, kwamba amani hii tunayopewa na Yesu ni amani kwa ajili ya sasa na kwa wakati ujao”. Ushauri wa Papa amesema, “Ni kuanza kuishi Mbingu sasa na matunda ya Mbingu. Siyo kugandishwa. Amani nyingine ndiyo, kwa maana inakugandisha na mambo ya ulimwengu na ikiwa dozi ya mgandisho huo inakwisha, unachukua nyingine na nyingine  na nyingine…  Lakini Amani ya Yesu ni ya mwisho, yenye kuwa na matunda na inayoambukiza. Haina ubinafsi kwa sababu inatazama Bwana.

Bwana atupatie neema iliyojaa matumaini

Amani nyingine inakutazama wewe na ni ya kibinafsi,Papa amesema. “Bwana atupatie neema iliyojaa matumaini na ambayo inazaa matunda na kutufanya tuwasiliane na wengine,na ambayo inaunda jumuiya na ambayo inatazama daima amani ya mwisho Mbinguni”. Kwa kuhitimisha Papa Francisko maadhimisho ya misa hii kwa kuabudu na kutoa baraka ya Ekaristi. Kabla ya kuacha kikanisa cha Mtakatifu Marta, wimbo wa Malkia wa Mbingu umeimbwa kwa lugha ya kilatino:Regína caeli laetáre, allelúia.

Quia quem merúisti portáre, allelúia.

Resurréxit, sicut dixit, allelúia.

Ora pro nobis Deum, allelúia.

12 May 2020, 09:18
Soma yote >