Tume kwa Mtakatifu Yosefu ili wafanyakazi wote wawe na hadhi ya kazi na mshahara wa haki. Tume kwa Mtakatifu Yosefu ili wafanyakazi wote wawe na hadhi ya kazi na mshahara wa haki. 

Sala ya Papa:Pasikosekane kazi,hadhi kazini na haki ya malipo!

Katika Misa ya Asubuhi Mei Mosi,katika kikanisa cha Mtakatifu Marta Mjini Vatican wakati mama Kanisa anakumbuka sikukuu ya Mtakatifu Yosefu Mfanyakazi,Papa amesali kwa ajili ya wafanyakazi na wasikose kulipwa kwa haki na waweze kuwa na kazi yenye hadhi hatimaye katika kufurahia uzuri wa mapumziko.

Na Sr. Angeka Rwezaula – Vatican

Katika sikukuu ya Mtakatifu Yosefu sambamba na Siku ya Wafanyakazi duniani, Mei Mosi, 2020, Papa Francisko amesisitiza kwa nguvu zote kuwa “kila ukosefu wa haki juu ya mtu anayefanya kazi ni kukanyaga hadhi ya kibinadamu, hata hadhi ya anayefanya haki. Ni kumshusha ngazi yake na kuishia katika mvutano kati ya dikteta na mtumwa”. Kwa maana hiyo katika mtazamo huo wa sikukuu ya Mtakatifu Yosefu Mfanyakazi, sambamba na siku ya kimataifa ya wafanyakazi amesema katika utangulizi wa misa: “Leo ni sikukuu ya Mtakatifu Yosefu Mfanyakazi na sambamba na Siku ya wafanyakazi. Tusali kwa wajili ya wafanyakazi wote. Kwa sababu  hasiwepo mtu hata mmoja akose kazi na wote kulipwa kwa haki na kila mmoja  aaweze kufurahia hadhi ya kazi na uzuri wa mapaumziko”.

Mungu anamkabidhi kazi mwanadamu ili kuifanya naye

Akiongozwa na masomo ya siku ya kumbu kumbu ya Mtakatifu Yosefu ambapo kati ya mambo mengine mwaka huu inaangukia katika kuadhimisha miaka 150 tangu kutangazwa Mtakatifu Yosefu kuwa Msimamizi wa Kanisa na Papa Pio IX kwa Hati ya “Quemadmodum Deus”, hivyo Papa Francisko ameanzia na sehemu ya somo la kwanza kutoka kitabu cha Mwanzo ambapo linazungumzia juu ya kazi ya uumbaji. “ Neno kazi  ni lile linalotumiwa katika Biblia ili kuelezea shughuli hii ya Mungu. Inapelekea ukamilifu wa kazi ambayo alikuwa amefanya na kuacha siku ya saba kupimzika kwa kila kazi na kumkabidhi shughuli mwanadamu ambaye anapaswa aendelea kufanye kazi kwa kuunda na yeye ulimwengu huu” amefafanua Papa Francisko.

Katika kazi mwanadamu ni muumbaji

Katika kazi, Papa aneendelea kusema, “kwa maana hiyo mwanadamu ni muumbaji na hivyo katika kazi ndani yake kuna wema, anaunda umoja na maelewano ya kila kitu na kumuunganisha mtu kwa kila kitu katika mawazo, kusikia na kutenda”. Papa Francisko aidha amebainisha kwamba katika kazi ndiyo wito wa kwanza wa mwanadamu na kwa maana hiyo kazi inampatia mwanadamu hadhi na kumfanya awe sawa na Mungu.

Hata leo hii hadhi imekanyagwa

Lakini hasa kazi hii mara nyingi sana imekanyagwa, amebainisha Papa. Kufuataia na hili pia amekumbuka zile meli zilizokuwa zinawapekeka watumwa kwenda Amerika, na watumwa, lakini pia amesisitiza kuwa kuna  utumwa hata leo hii, kwa wanaume na wanawake ambao wanalazimika kufanya kazi ili waweze kuishi. Kazi za suruba, zisizo za hadhi, kulipwa vibaya na ambazo zinampelekea mwanadamu kuishi hadhi iliyokanyagwa, amethibitisha. Hilo siyo matukio yanayoteka mbali anasema Papa, kwa sababu hata karibu yetu kuna kazi ambazo zinalipwa vibaya, bila usalama na bila pensheni.  Hii yote siyo hadhi ya leo hii na kwa maana hiyo “ kila ukosefu wa haki ambayo unafanyika juu ya mtu ambaye anafanya kazi ni kumkanyaga hadhi yake ya kibinadamu”. Lakini hata hivyo  Papa Francisko amesisitiza kuwa, “inawezekana kufanya kazi katika hali ya haki na yenye kuheshimu hadhi ya mtu”.

Kuwaombea hata wajasiriamali wema

Katika Siku yaWafanyakazi, wote inayoadhimishwa na waamini na wasio waamini, Papa Francisko anawaalika kwa maana hiyo kuungana na wale wote ambao wanapambana ili kuweza kupata haki ya kazi na hata wajasiriamali wema ambao wanapeleka mbele kazi kwa haki, hata kama wao wanapoteza. Hapa ametoa mfano mmoja wa Mjasiriamali ambaye amemfahamisha kuwa licha ya matatizo yaliyopo hataweza kuwasimamisha kazi wanafanyakazi wake.”Akitolea  mfano wa maneno ya mjasiriamali alisema: “ kwa sababu kumwachisha kazi mmoja wao ni kama kuachishwa kazi mimi”.  Kwa maana hiyo Papa Francisko ameongeza “hii ndiyo dhamiri ya wajasiriamali wema ambao wanalinda wafanyakazi wao kama vile ni watoto wao. Tuwaombee hata wao”. Na tuombe kwa Mtakatifu Yosefu, akitazama sanamu nzuri iliyokuwa katika Kikanisa ikiwa imeshikilia zana ya kazi mikononi na kwamba “atusaidie kupampania hadhi ya kazi ili kazi iweze kuwapo kwa watu na iwe kazi yenye hadhi. Na isiwe kazi ya utumwa. Leo hii iwe ndiyo sala, Papa amehitimisha.

Komunio ya tamaa,baraka na sala ya Malkia wa Mbingu

Mara baada ya Komunio yake, ameomba waamnini wote nao wapokee komuniuo ya tamaa na baadaye kufuata kuabudu na kuhitimisha kwa baraka ya ekaristi na wimbo wa mwisho wa Malkia wa Mbingu: Regína caeli laetáre, allelúia. Quia quem merúisti portáre, allelúia. Resurréxit, sicut dixit, allelúia. Ora pro nobis Deum, allelúia.

Malkia wa mbingu, furahi, aleluya. Kwani uliyestahili kumchukua, Aleluya. Amefufuka alivyosema, Aleluya. Utuombee kwa Mungu, Aleluya. Furahi shangilia, ee Bikira Maria, Alaluya. Kwani hakika Bwana amefufuka Aleluya.

 

01 May 2020, 10:49
Soma yote >