Papa amesali kwa ajili ya watu wanaozika wafu katika kipindi cha janga!

Katika misa ya Papa Francisko kwenye kikanisa cha Mtakatifu Marta amesali kwa ajili ya wenye jukumu la kuzika wafu katika kipindi hiki cha janga,wanahatarisha maisha yao.Katika mahubiri amejikita kuelezea juu ya roho ya ulimwengu,tasaufi ya ulimwengu ambayo ni utamaduni wa usiojua uaminifu,hauna uvumilivu wa msalaba na unataka kuharibu Kanisa.Ni kwa njia ya imani katika Kristo aliyekufa na kufufuka inawezekana kushinda ulimwengu.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican

Papa Francisko kama kawaida ya kila siku ikiwa ni wiki ya tano ya Kipindi cha Pasaka Jumamosi tarehe 16 Mei 2020, ameadhimisha misa yake katika kikanisa cha Mtakatifu Marta Vatican. Mawazo yake wakati wa utangulizi yamewaendea watu wanaojikita  katika huduma ya kuzika wafu katika janga hili. “Tusali kwa ajili ya watu ambao wanajikita na shughuli ya kuzika wafu katika janga hili. Kuzika wafu ni moja ya matendo ya huruma  na ndiyo jambo linalopendekezwa kwa asili yake. Tusali kwa ajili ya maisha kwa maana wanayo hatari ya kuambukizwa”.

Ulimwengu ulimchukia Yesu

Katika mahubiri yake Papa Francisko ametafakari Injili ya Siku ( Yh 15, 18-21) mahali ambapo Yusu anawambia mitume wake kuwa “Iwapo ulimwengu ukiwachukia, mwajua ya kuwa umenichukia mimi kabla ya kuwachukia ninyi. Kama mngekuwa wa ulimwengu, ulimwengu ungewapenda walio wake; lakini kwa kuwa ninyi si wa ulimwengu, bali mimi naliwachagua katika ulimwengu, kwa sababu hiyo ulimwengu huwachukia”.

Ulimwengu ni tamaduni ya kitambo leo ndiyo kesho hapana

Papa Francisko amebainisha kuwa"Yesu alisema mara nyingi kuhusu ulimwengu, anazungumzia chuki dhidi yake na wafuasi wake na kumwomba Baba hasiwaondoe katika ulimwenguni bali awalinde na roho ya ulimwengu". Kufuatana na hilo Papa anajiuliza: "Je Roho ya umwengu ni ipi?  Ni ulimwengu upi wenye uwezo wa kuchukia, wa kuharibu wafuasi wake zaidi na kuharibu Kanisa? “Ni pendekezo la maisha,  ulimwengu ni tamaduni; ni tamaduni ya kitambo, utamaduni wa kuonekana, ni utamaduni wa leo ndiyo na kesho hapana, kesho ndiyo na leo hapana” Papa amefanua. 

Ulimwengu ni kama kinyonga hujibadili 

Ulimwengu, Papa Francisko amebanisha, siyo wa juu juu tu, lakini una mizizi ya kina na ni mabadiliko, au ni kama kinyonga kulingana na mahali anapokuwa lakini ndiye huyo huyo, ni pendekezo la maisha ambalo huingia kila mahali, hata katika Kanisa. Ulimwengu, wafuasi wa kidunia, kujitengeneza wa kijuu juu tu, kila kitu kinafanywa ili kiwe hivyo”.Na Yesu anaomba kwa Baba atulinde dhidi ya utamaduni huu wa ulimwengu. Ni tabia ya kutumia na kutupa, kwa mujibu wa hali halisi na urahisi. Ni tamaduni isiyo na uaminifu na ni njia ya kuishi maisha pia kwa wengi wanaojiita Wakristo. Ni Wakristo lakini wao ni wa ulimwengu".

Ulimwengu wa kiroho ni tabia ya maisha

Yesu amesema mbegu inayoanguka katika ardhi yenye mahangaiko ya  Dunia yaani ya ulimwengu unasonga Neno la Mungu, hauachi neno likue. Kwa kusitiza zaidi Papa ametaja kitabu cha Padre de Lubac, mahali ambapo anazungumzia ulimwengu wa kiroho na ambao  amebainisha ni mbaya zaidi ya maovu yanayoweza kutokea katika Kanisa; na yeye haizidishi kiasi  kwa kuelezea 'maovu kadhaa ambayo ni mabaya', Papa amesema. “Ulimwengu wa kiroho ni tabia ya maisha, ni njia ya maisha; pia njia ya  kuishi ukristo. Na katika  kuishi mbele ya kuhubiriwa Injili, huchukia, na kuua ”. Papa Francisko amekumbuka juu ya wafiadini,  waliouawa kwa  sababu ya chuki ya imani, lakini ameongeza kusema siyo hao tu. Walio wengi wanauawa na ulimwengu ambao unachukia imani”.

Ulimwengu hauvumilii msalaba

Papa Francisko amekumbusha hata haotuba ya Paulo huko Atene, alipotoa ule umakini kuhusu Mungu hasiyejulikana na kuanza kuhubiri Injili, lakini alipofika sehemu ya Msalaba na Ufufuko, wote walikashfu na kuondoka zao. Malimwengu yapo na hawana uvumilivu, Papa amesema.  Ulimwengu una jambo moja ambalo haulikubali ambalo ni  kashfa ya Msalaba. Hauwezi kuvumilia Papa amesisitiza. Na dawa pekee dhidi ya roho ya ulimwengu ni Kristo aliyekufa na kufufuka kwa ajili yetu sisi, kashfa na upumbavu

Ushidi wa pekee ni imani katika Yesu Kristo

Mtume Yohana anasema kwamba “ushindi dhidi ya ulimwengu ni imani yetu”. Ushindi wa pekee ni “imani katika Yesu Kristo, aliyekufa na kufufuka. Na hii haimaanishi kuwa mdanganyifu, ”,kuacha kuzungumza na watu wote, lakini ni kujua kuwa ushindi dhidi ya roho ya ulimwengu ni imani yetu, kashfa ya Msalaba.

Kwa kuhitimisha Papa Francisko amesema:“Tuombe Roho Mtakatifu katika siku hizi za mwisho, wakati wa Pasaka, neema ya kung’amua  ni nini mwalimwengu nanì ni nini maana ya  Injili na siyo kudanganywa, kwa sababu ulimwengu unatuchukia, ulimwengu ulimchukia Yesu na Yesu aliomba kwamba Baba atulinde dhidi ya roho ya ulimwengu ”. Mara baadaya Misa imefuata kuabudu na kubariki kwa Ekaristi. Wimbo wa Malkia wa Mbingu ulikuwa wa Mwisho.

Regína caeli laetáre, allelúia.

Quia quem merúisti portáre, allelúia.

Resurréxit, sicut dixit, allelúia.

Ora pro nobis Deum, allelúia

16 May 2020, 09:16
Soma yote >