20-04-26 Papa Francisko katika Misa ya Dominika ya III ya kipindi cha Pasaka amewaombea watu wote wenye kuteseka kwa huzuni sababu ya madhara ya janga la virusi vya corona. 20-04-26 Papa Francisko katika Misa ya Dominika ya III ya kipindi cha Pasaka amewaombea watu wote wenye kuteseka kwa huzuni sababu ya madhara ya janga la virusi vya corona. 

Papa Francisko asali kwa ajili ya wenye huzuni katika janga!

Katika misa ya Papa Francisko,Jumapili tarehe 26,Aprili,amewakumbuka na kuwaombea watu wote wenye huzuni na uchungu kwa maana wako peke yao au bila kazi na hawajuhi namna ya kutunza familia kwa sababu ya matokeo ya janga la virusi vya corona.Katika mahubiri amekumbusha Yesu anayetembea daima karibu nasi hata wakati wa kipindi cha giza.

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Papa Francesco wakati wa kuadhimisha Misa katika Kikanisa cha Mtakatifu Marta mjini Vatican, tarehe 26 Aprili 2020 ambapo ni Dominika ya III ya kipindi cha Pasaka, katika utangulizi wake mawazo yamewandea wale wote wenye huzuni na uchungu mkubwa katika kipindi  hiki kigumu cha janga la virusi vya corona. “Tuombe katika misa hii leo hii kwa ajili ya watu wanaoteseka kwa uchungu, kwa sababu wako peke yao au kwa sababu hawajuhi ni kitu gani kinawasubiri baadaye au kwa sababu hawajuhi namna gani ya kupelekea mbele familia kwani hawana fedha na hawana kazi. Watu wengi wanateseka kwa huzuni. Tuwaombee leo hii”.

Papa Francisko akianza mahubiri yake kwa kuongozwa na Injili ya siku  kutoka Mtakatifu Luka 24, 13-35,  ambayo inasimulia juu ya Yesu Mfufuka aliyekutana na mitume wa Emau na jinsi walivyomtambua wakati wa kuumega mkate. Papa Fancisko amesema kuwa mara nyingi tumesikia kuwa ukristo siyo mafundisho, bali ni namna ya kuishi, na siyo utamaduni. Yote hayo yanaweza kuwa sawa, lakini jambo muhimu la kwanza ni kukutana. “Mtu ni mkristo kwa sababu alikutana na Yesu Kristo na kuacha akutane Naye”.

Katika sehemu hii ya Injili ya Luka, inasimuli kwa namna ya kutambua vema jinsi Bwana anavyotenda na jinsi gani sisi tunapaswa kutenda.  Papa Francisko amebainisha kuwa: “Sisi tulizaliwa na uzao wa kutokuwa na utulivu. Mungu alitaka hivi: kutokuwa na utulivu wa kutafuta utimilifu, kutokuwa na utulivu wa kumpata Mungu, mara nyingi hata bila kujua kama tunayo hali kama hii ya kutokwa na utulivu. Mioyo yetu haina utulivu, mioyo yetu ina kiu: kiu ya kukutana na Mungu. Anamtafuta, na mara nyingi kwenye njia mbaya: anapotea na  baadaye anarudi, anamtafuta ... Kwa upande mwingine, Mungu ana kiu ya kukutana, kiasi kwamba alimtuma Yesu kukutana na sisi, ili kukabiliana na wasiwasi huu”.

Papa Francisko ameendelea na mahubiri yake na kuuliza swali: “Je Yesu anatenda namna gani? Katika sehemu hii ya Injili, Lk 24,13-35  inaonesha ni kwa jinsi gani Yeye anaheshimu, anaheshimu hali yetu halisi na wala ahendi mbele. Ni kwa wakati mwingine tu kuwa mkaidi, hasa tunapofikiria Paulo alipomwangusha chini kutoka juu ya farasi wake. Lakini kawaida Yeye  huenda pole pole, kwa heshima  nyakati zetu. Yeye ndiye Bwana wa uvumilivu. Ni kiasi gani cha uvumilivu alio nao Bwana na kila mmoja wetu! Bwana anatembea kandoni mwetu”. Hali kadhalika Papa Francisko amesisitiza kuwa kama inavyosikika kwa mitume hawa wawili, anasikiliza wasiwasi wetu, anautambua na wakati huo huo  analo jambo la kueleza. Kwa upande wa Bwana anapenda kusikia jinsi tunavyozungumza, kuelewana vyema na kutoa jibu sahihi kwa ajili ya wasiwasi huo. Bwana hana mwendo kasi , yeye huendana na  hatua zetu, mara nyingi polepole, lakini kwa uvumilivu wake ni kama huo”.

Papa Fracisko amekumbusha hata kanuni ya kizamani ya mahujaji ambayo inasema kuwa “mhujaji wa kweli lazima aende hatua kwa hatua na mtu anayetembea polepole. Yesu anao uwezo huo,yeye hana mwendo kasi bali anatusubiri ili sisi tutimize hatua ya kwanza. Na wakati unafika, yeye huuliza swali. Katika kesi hii ni wazi: “Unazungumza nini?” (Rej Lk 24,17), anakuwa mjinga ili kutufanya tuzungumze. Yeye anapenda sisi kwamba tuzungumze. Yeye anapenda kusikia hili, anapenda kuwa tuzungumze namna hiyo. Ili kutusikiliza na kutujibu anatufanya tuzungumze kama vile kujifanya mjinga, lakini kwa heshima kubwa. Na baadaye anajibu, anaelezea, kwa hatua muhimu. Hapa anatuambia kuwa: “Je! Kristo hakulazimika kupata mateso haya ili aingie katika utukufu wake?  Na, akianza na Musa na manabii wote, aliwaelezea katika Maandiko yote yale yaliyomhusu (Rej Lk 24, 26). Anafafanua, na kuweka bayana”.

Papa Francisko hali kadhalika amesema: “Ninakiri kwamba nina udadisi wa kujua jinsi Yesu alivyoelezea ili nami ni weze  kufanya vivyo hivyo. Ilikuwa ni katekesi nzuri. Na baadaye Yesu yule yule ambaye alitusindikiza na ambaye alitukaribia na kujifanya anatangulia kwenda mbele zaidi kuona ni kiwango gani cha wasiwasi wetu. Na kusikia mitume wanamwambia kuwa, “Hapana, njoo, njoo, kaa nasi kwa muda” (Rej 24, 29). Kwa njia hiyo mkutano hulifanyika, Papa amesisitiza.  Kwa kuongezea anasema “Lakini mkutano siyo wa wakati huo wa kuumega mkate huo tu, bali ni safari nzima. Tunakutana na Yesu katika gizani la mashaka yetu. Hata katika shaka baya la dhambi zetu, Yeye yupo kwa ajili ya kutusaidia, katika wasiwasi wetu ... Yeye yupo pamoja nasi kila wakati”.

Bwana anatusindikiza kwa sababu anataka kukutana na sisi. Hii ndiyo sababu tunasema kwamba msingi wa Ukristo ni tukio, ni kukutana na Yesu. Kwanini wewe ni Mkristo? Na watu wengi hawajuhi kusema hilo kwa sababu hawakugundua kuwa ni kukutana na Yesu. Yesu hututafuta kila wakati. Na tuna wasiwasi wetu. Wakati ambapo wasiwasi wetu  hukutana  na Yesu, hapo ndipo tunaanza maisha ya neema, maisha ya utimilifu, maisha ya safari ya Kikristo. Bwana atupe neema yote  hayo ili kukutana na Yesu kila siku, kujua, hakika kuwa anatembea na sisi katika wakati wetu wote. Yeye ni msindikizaji wa hija yetu”. Amehitimisha.

Papa Francisko kabla ya kumaliza maadhimisho ya misa takatifu imfuatia  kuabudu na baraka ya ekaristi akiwaalika waamini nyumbani washiriki ekaristi ya tamaa katika roho ….. Na wakati huo huo kala ya kuondoka katika kikanisa cha Mtakatifu Marta,wimbo wa Maria kwa lugha ya kilatino “Regina caeli”, unaoimbwa kipindi chote cha Pasaka umeimbwa: Regína caeli laetáre, allelúia.

Quia quem merúisti portáre, allelúia.

Resurréxit, sicut dixit, allelúia.

Ora pro nobis Deum, allelúia.

Malkia wa Mbingu furahi Aleluya,kwani uliyestahili kumchukua Aleluya.

Amefufuka alivyosema aleluya,utuombee kwa Mungu aleluya.

Furahi shangilia ee Bikira Maria aleluya,kwani hakika Bwana amefufuka aleluya.

Queen of heaven be happy hallelujah, for whom you deserve to take hallelujah. He has risen and said hallelujah, pray for us to God hallelujah. Rejoice, O Virgin Mary Hallelujah, for the Lord has risen, for surely the Lord has risen hallelujah.

26 April 2020, 12:29
Soma yote >