Tafuta

Vatican News
17-04-2020 Misa ya Papa Francisko katika kikanisa cha Mtakatifu Marta Vatican. 17-04-2020 Misa ya Papa Francisko katika kikanisa cha Mtakatifu Marta Vatican.  (ANSA)

Papa Francisko asali kwa ajili ya mama wajawazito na kuonya hatari ya imani katika mitandao!

Katika misa ya asubuhi tarehe 17 Aprili 2020 mawazo ya sala ya Papa ni kwa ajili ya mama wajawazito katika kipidni hiki kisicho na usalama.Katika mahubiri yake amezungumzia juu ya hatari na kuweka tahadhari juu ya kuwa na imani dhaifu, isiyo kuwa na kijumuiya na mawasiliano halisi ya kibinadamu katika kuishi sakramenti ya kiroho kwa njia ya mitandao ya kijamii.

Na Sr. Angela Rwezaula Vatican

Kama kawaida ya kipindi hiki Papa Francisko, Ijumaa ya Pasaka  tarehe 17 Aprili 2020 katika kikanisa cha Mtakatifu Marta Vatican, kwenye utangulizi wake mawazo yamewaendea wanawake wajawazito: “Ninapenda leo hii kusali kwa ajili ya wanawake wajawazito, ambao watakuwa mama na wana wasiwasi. Wakijiuliza swali: ni dunia gani ataishi mwanangu? Tuwaombee ili Bwana aweze kuwapa ujasiri wa kwenda mbele na watoto hawa kwa tumaini kwamba kwa hakika dunia itakuwa tofauti, lakini daima itakuwa dunia ambayo Bwana ataipenda sana. Katika mahubiri yake, Papa Francisko ametafakari Injili ya Siku kutoka  Yahane 21 1-14) mahali ambapo mara baada ya Yesu kufufuka aliendelea kuwatokea mitume ambao walikuwa wamerudi fukweni kuvua samaki, lakini bila kupata hata mmoja katika bahari ya Tiberiade. Hii ilikuwa ni kwa mara ya tatu Yesu anawatokea baada ya kufufuka.

Papa Francisko akiendelea amesema, Bwana aliwaagiza watupe nyavu zao na  wakajaza nyavu hizo.  Jambo hili linajitokea katika hali ya kawaida, kwa sababu mitume walikuwa wamekwisha komaa katika uzoefu wa kawaida wa kifamilia na Yesu. Kama wakristo, tunatakiwa kukua katika hali hii ya kifamilia na ambayo ni tabia binafsi, lakini ni ya kijumuiya.  Hali ya kifamilia bila jumuiya, bila Kanisa, bila Sakramenti ni hatari, inaweza kugeuka hali ya kawaida ya kifamilia iliyo mbali na kujitenga kutoka kwa Watu wa Mungu. Katika janga hili, amebainisha Papa, mawasiliano ni kwa njia ya vyombo vya habari, lakini watu hawakai pamoja kama ilivyokuwa inajitokeza kwenye misa hiyo. Ni hali ngumu ambayo kwa waamini hawawezi kuudhuria maadhimisho na wanaweza kufanya Komunio ya tamaa tu. Kwa maana hiyo  Papa Francisko anasema tunapaswa kuondokana na handaki hizi ili kuweza kurudia kuwa pamoja kwa maana hilo siyo Kanisa, bali ni Kanisa ambalo liko katika hatari ya kimintandao. “Bwana atufundisha kuishi uzoefu wa kifamilia wa dhati, familia ya kina na Yeye, lakini katika Kanisa na Sakramenti zake na watu watakatifu wa Mungu.”

Papa Francisko akiendelea na tafakari ya kina ya Injili ya siku anasema: Mitume walikuwa ni wavuvi na Yesu alikuwa amewaita kutoka katika kazi yao. Andrea na  Petro walikuwa wanafanyakazi na nyavu. Waliacha nyavu na kumfuata Yesu. Yohane na Yakobo pia waliacha baba yao na vijana wengine waliokuwa wanafanya kazi nao na kumfuata Yesu”. Wito ulikuwa huo ni wa kuvua. Katika sehemu hii ya Injili, miujiza hii ya uvuvi, amappngeza kusema- inatufanya tufikirie hata muujiza mwingine wa uvuvi ambao unasimuliwa katika Injili ya Luka 5. Hata pale ilitokea miujiza sawa na hiyo. Hawa walipata samaki wakati wamekwisha fikiria hawatapata. Baada ya kuhubiri Yesu aliwambia tupeni jarife. Nao wakajibu sisi tumefanya kazi usiku kucha na hatukupata kitu”, Lakini Yesu akasema enendeni na ndiyo  Petro kwa imani  alijibu kuwa “kwa neno lako nitatupa jarife”. “Hapo kulikuwa na samaki wengi, inasema Injili na wakabaki na mshangao wa miujiza hiyo”

Papa Francisko akidadavua anasema: “Leo hii katika uvuvi mwingine hawazungumzi juu ya mshangao. Inaonesha uhakika wa kuwa kawaida, hii ni kuonesha maendeleo, yaani mchakato wa safari katika utambuzi wa Bwana, kuelewa kwa kina Bwana. Kwa njia hiyo Papa amesema “mimi nitasema neno linalostahili ni “uzoefu wa kifamilia na Bwana” Yohane alipoona hivyo akamwambia Petro. “Ndiye Bwana! naye Petro aliposikia ya kwamba ni Bwana, akajifunga vazi lake, (maana alikuwa uchi), akajitupa baharini kumfuata Bwana. Ikumbukwe kwa mara ya kwanza alipiga magoti mbele yake na kumwambia “nenda mbali nami kwa maana mimi ni mdhambi”,  lakini kwa mara hii hasemi lolote kwa maana imekuwa kawaida. Hakuna aliyeuliza :“ je wewe ni nani?” Walikuwa wote wanajua ni Bwana, jibu lao lilikuwa la asili, yaani kukutana na Bwana. Uzoefu wa mitume wa kukutana na Bwana unaonekana kuwa ulikuwa umekua.

Sisi Wakristo pia, katika safari yetu ya maisha, tuko katika hali kama hii ya kutembea kwenda mbele katika kufahamiana na Bwana. Papa ameongeza “ninaweza  kusema- ni kidogo wa kumpatia mikono kwa sababu Yeye anatembea nasi, na tunamtambua kuwa ni Yeye. Aidha  katika kufahamiana kwa kila kitu na Bwana Papa Francisko anathibitisha, ndiyo ule wa kikristo.  Kwa hakika waliweza kupata kifungua kinywa kwa samaki na mkate; kwa hakika waliweza kuzungumza mambo mengi ya asili.  Huo ndiyo ufamilia na Bwana, kwa kikristo ambao daima ni wa kijumuiya. Ndiyo ni wa kina na ni wa kibinafsi, lakini ni wa kijumuiya. Amesisitiza Papa! Uzoefu wa kifamilia  bila kuwa na jumuiya, uzoefu wa kifamilia bila  kuwa na Kanisa, bila kuwa na watu, bila kuwa na sakramenti ni hatari sana Papa ameonya.

Unaweza kugeuka uzoefu wa kifamilia mbali yaani ufamilia wa umimi tu ambao unaondoa ukaribu na watu wa Mungu. Uzoefu wa  mitume na Bwana ulikuwa wa kawaida kila wakati, ulikuwa wa kila wakati mezani, na ishara ya jamuiya, ulikuwa kila wakati na sakramenti na mkate. Papa Francisko amethibitisha kwamba: Ninasema hivyo kwa sababu kuna mtu alinifanya nitafakari juu ya hatari ambayo sasa tunaishi, janga hili ambalo limefanya kila mtu aweze kuwasiliana hata kidini kupitia mitandao ya kijamii, kupitia vyombo vya habari, hata katika Misa hii, sisi sote tunawasiliana, lakini siyo pamoja,  bali kiroho pamoja. Watu ni wachache lakini kuwa watu wengi: “sisi tuko pamoja hapa, lakini siyo pamoja. Hata sakramenti: leo hii mnayo ninyi, Ekaristi, lakini watu ambao wameunganishwa na sisi, wanashiriki kiroho tu. Na hii siyo Kanisa: Hili ni Kanisa katika hali ngumu, ambayo Bwana ameruhusu, lakini wazo zaidi la Kanisa daima ni la kuwa pamoja na watu na sakramenti kila wakati”.

Ushuhuda wa Papa Francisko amesema, “Kabla ya Pasaka, wakati zilitolewa habari kwamba nitaadhimisha Pasaka katika kanisa Kuu la Mtakatifu Petro likiwa tupu, Askofu mmoja aliniandikia, ni  Askofu mzuri na  akanikosoa. “Lakini kwa nini Kanisa la Mtakatifu Petro ni kubwa sana, usiweke watu wasiopungua 30, ili angalau waweze kuonekana watu? Hakutakuwa na hatari ... Mimi nilifikiri: Hivi huyo ana nini katika kichwa chake kuniambia hayo?  Sikuelewa kwa wakati huo. Lakini kwa kuwa yeye ni Askofu mwema, aliye karibu sana na watu, alikuwa na kitu cha kutaka kuniambia. Niliwaza kwamba nikikutana naye nitamwuliza. Baadaye nikaelewa. Yeye alitaka kuniambia kuwa “Uwe mwangalifu ili usiweze kueneza Kanisa katika mitandao, sakramenti isiwe ya mitandao na watu wa Mungu wasiwe ni wa mitandao. Kanisa, Sakramenti, Watu wa Mungu ni halisi. Ni kweli kwamba kwa wakati huu lazima tufanye hivi kwa kuwa na uzoefu wa Bwana kwa njia hii, lakini iwe ni kwa njia ya kutoka kwenye handaki na siyo kukaa humo.

Na huu ndiyo uzoefu wa kifamilia wa mitume:siyo ule wa kuwa mbali na wala wa mitandao na siyo wa ubinafsi kwa kila mmoja wao, lakini ni uzoefu kamili wa watu. Kuwa na uzoefu wa uhusiano wa kawaida na Bwana katika maisha ya kila siku, uzoefu wa kifamilia  na Bwana katika sakramenti, katikati ya watu wa Mungu. Wao walifanya  mchakato wa safari ya ukomavu katika kufahamiana na Bwana. Kwa njia hiyo tujifunze kufanya hivyo pia. Kuanzia mwanzo, walielewa kuwa uzoefu huo ulikuwa tofauti na vile walivyokuwa wanafikiria na hatimaye walifikia jibu hilo. Walijua ni Bwana, walishirikishana kila kitu: jumuiya, sakramenti, Bwana, amani, na  sikukuu. Bwana aweze kutufundisha kukaa naye kwa kina, kufahamiana kifamilia na Yeye lakini katika Kanisa,na Bwana na watu waaminifu wa Mungu. Papa amehitmisha maadhimisho kwa kuabudu na kubariki kwa Baraka ya ekaristi akiwaalika waamini kupokea komunia ya tamaa.

MAHUBIRI YA PAPA 17 APRILI
17 April 2020, 10:56
Soma yote >