Tafuta

Misa ya Papa Francisko katika kikanisa cha Mtakatifu Marta Misa ya Papa Francisko katika kikanisa cha Mtakatifu Marta 

Papa Francisko amesali kwa ajili ya waathirika wa janga wasiojulikana!

Katika Misa ya asubuhi ya Papa Francisko tarehe 30 Aprili 2020,mawazo yake yamewaendea watu waliokufa kwa sababu ya Covid-19.Amesali kwa namna ya pekee wale ambao wamekufa bila kujulikana majina yao na kuzikwa katika kaburi la pamoja.Kwenye mahubiri amekumbusha kuwa kumhubiri Yesu siyo kufanya propaganda,bali ni ushuhuda wa imani kwa maisha binafsi na kusali kwa Baba ili avutie watu kwa mwanaye Yesu.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Papa Francisko ameadhimisha misa yake katika kikanisa cha Mtakatifu Marta Vatican Alhamisi, tarehe 30 Aprili 2020 katika wiki ya tatu ya Pasaka. Akianza na utangulizi wake mawazo yake yamewaendea waathirika wa virusi vya corona au covid-19: "Tusali leo hii kwa ajili ya marehemu, wale wote ambao wamekufa kwa sababu ya janga; hata kwa namna ya pekee marehemu ambao hawana majina na ambao tumewaona katika picha za kuzikwa katika kaburi la pamoja. Ni wengi…"

Katika mahuburi Papa Francisko ametafakari somo la kwanza la Matendo ya Mitume (Mdo 8, 26-40) inayosimulia Filipo aliyekutana na Mkushi aliyekuwa juu ya hazina yote ambaye alikuwa anatafuta kujua ni nani aliyekuwa ameandikwa na Nabii Isaya kwa maana fungu la Maandiko alilokuwa akilisoma lilikuwa likisema: “Aliongozwa kwenda machinjoni kama kondoo, Na kama vile mwana-kondoo alivyo kimya mbele yake amkataye manyoya, Vivyo hivyo yeye naye hafunui kinywa chake. Ndipo Filipo alipomweleza kuwa alikuwa na Yesu, na Mkushi akaomba kubatizwa.

Wasi wasi aliokuwa kuwa nao huyo mkushi katika somo la Isaya ulikuwa ni Baba mwenyewe ambaye alikuwa anamvutia kuelekea kwa Yesu (Yh 6,44): Alikuwa amemwandaa huyo mkushi wa Ethiopia kwenda Yerusalemu ili kuabudu Mungu na baadaye katika somo alikuwa anamwandaa huyo ili kumfunulia Yesu hadi kufikia  kuona maji na kusema ninaweza kubatizwa, kwa maana yeye aliamini.

Papa Francisko katika Injili ya siku kutoka (Yh 6, 44-51) ambayo inavutia utambuzi wa Mwana wa Mungu anasema, bila tukio kama hilo siyo rahisi kujua fumbo la Kristo. Hakuna ambaye anaweza kuja nyuma yangu ikiwa hajavutiwa na Baba na hakuna ambaye anaweza kumjua Yesu bila Yesu kumvutia kwake na  ndiyo thamani ya utume wetu wa kutenda kiutume na kama wakristo a,emesisitza Papa na kufikiria  shughuli za utume wetu… Papa amesema kwamba "ili jyweza kwenda katika utume bila kuwa na hushuhuda, haiwezekani kufanya lolote".

Bila ushuhuda, wa kikristo, kazi yetu haitakuwa kazi ya ushuhuda, bali ni kama kazi ya chama chochote cha kihisani, ikiwa na mambo mengi lakini yasiyo kuwa na cha zaidi mbele ya Mungu. Ikiwa ninataka kwenda katika utume, ikiwa mimi nataka kwenda kufanya hutume ni lazima niende kwa uwajibikaji ambao Baba anavutia watu kwa Yesu na ndiyo unafanya ushuhuda Papa amethibitisha, na kwamba Yesu mwenyewe alimwambia Petro. "Baba anavutia watu hata kwa njia ya ushuhuda wetu, bila kufanya hivyo tututenda mambo mema lakini siyo tangazo la Injili".

Papa Francisko akiendelea na mahubiri amesema ni lazima kusali ili Baba  Mungu aweze kuwavutia watu wake kwa maana bila ushuhuda huwezi kuhubiri kitume na huwezi kumtangaza na kufanya  mahubiri labda ya adili, utafanya mambo mengi lakini Baba Mungu haweza kuvutiwa na watu wake na hiki ndicho kitovu ha utume wetu. Amekazia Papa Francisko.

Tutoe ushuhuda na kusali ndiyo njia mwafaka kwa ajili ya utume pia hata kufanya kazi kama wakristo, ameshauri Papa. Tujiulize, je ninatoa ushuhdua kwa mtindo wangu wa maisha, ninasali ili Baba Mungu aweze kuvutia watu kwa Yesu, ni maswali Papa ametoa. "Sisi hatuwezi kufanya mtu yoyote awe na uongofu kwa maana ni Mungu anayegusa mioyo wa watu, amesema hayo pia kwa kutoa mfano mmoja wa mwanamke aliyemletea mbele watoto wawili akijisifia kuwa aliwarudisha katika imani.  "Tuombe Mungu neema ya kuishi kazi yetu, tumwombe Bwana ili aweze kuwavutia watu wake kwa Yesu".

30 April 2020, 10:20
Soma yote >