Tafuta

Vatican News
PAPA FRANCISKO PAPA FRANCISKO 

Papa Francisko amesali kwa ajili ya Ulaya ili iwe ya umoja na udugu!

Katika Misa ya asubuhi Jumatano tarehe 29 Aprili 2020,katika kikanisa cha Mtakatifu Marta,Vatican Papa Francisko amekumbusha Siku kuu ya Mtakatifu Katarina wa Siena,Msimamizi wa Ulaya na kusali kwa ajili ya umoja na muungano wa Ulaya ili kwa pamoja tuweze kutembea kwenda mbele kama ndugu.Katika mahubiri Papa anawaalika waamini kuomba Bwana neema ya kuwa rahisi na unyenyekevu wa kuungama kwa dhati dhambi binafsiili kuweza kupata msamaha wa Mungu.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican

Papa Francisko kama kawaida ameadhimisha Misa Takatifu ya asubuhi, tarehe 29 Aprili 2020 wakati Mama Kanisa anakumbusha Siku kuu ya Mtakatifu Catarina wa Siena, Bikira na Mwalimu wa Kanisa  ambaye ni msimamizi wa Italia na Ulaya. Katika utangulizi wake, mawazo yake ni kwa  Bara la Ulaya na vile vile kukumbusha hali halisi ya kipindi cha janga la Covid-19: Leo hii ni Siku kuu ya Mtakatifu Caterina wa Siena. Mwalimu wa Kanisa na msimamizi wa Ulaya. Tusali ili wote tuweze kwenda mbele pamoja kama ndugu”.

Yohane anaonya tusidanganye

Akianza tafakari yake kwenye mahubiri yamejikita katika somo la Barua ya Kwanza ya Mtakatifu Yohane (1Yh 1,5-2,2), Mtume ambaye anathibitisha kuwa Mungu ni nuru, tukiwa tunasema ya kwamba twashirikiana naye, tunaungana na wengine, damu ya Yesu itatutakasa na kila dhambi. Lakini anaonya kuwa, tukisema kwamba hatuna dhambi, twajidanganya wenyewe, wala kweli haimo ndani mwetu. Papa Francisko anasema katika somo hili kuna mambo ambayo yanakwenda kinyume, kati ya mwanga na giza, uongo na ukweli, dhambi na kutokuwa na hatia. Lakini daima mtume anahimiza uthabiti na katika ukweli na kusema kuwa hatuwezi kuwa katika muungano na Yesu na kutembea katika giza, kwani ukungu ni hatari zaidi, kwa sababiu ukungu huo unakufanya uamini kuwa wewe unatembea katika  mwanga, ukungu ni msaliti mkubwa sana, amesisitiza Papa.

Sisi ni wadhambi

Mtume anaendelea mbele kusema kuwa sisi ni wadhambi. Papa Francisko amebainisha kuwa, hapa kuna jambo ambalo linaweza kudanganya wote, kwani mara nyingi wote husema sisi ni wadhambi na ni jambo la kawaida na kijamii, lakini kwa kufanya hivyo hatuna dhamiri ya kweli ya dhambi, yaani uwazi. “Ukweli daima ni wa dhati”. Papa Francisko aidha amesema kuwa, “wewe huwezi kwenda kuungama dhambi zako kwa namna ya kijuu juu tu, inabidi uzingatie hali halisi ya dhambi, amerudia kusisitiza Papa. Udhabiti  ni ule wa kunifanya nihisi uzito wa kuwa mimi ni mwenye dhambi. Kwa kutoa mifano halisi amebainisha kuwa “Ni vizuri kuwasikiliza watoto wadogo wanapokuja kuungama, wanasema vitu halisi. Wao wana ule urahisi”.

Urahisi wa kitoto anasema ukweli wote

Kwa kutoa mfano Papa amekumbuka mtoto mmoja ambaye alikwenda kuungama na akamweleza kuwa alikuwa na huzuni kwa sababu alikuwa amegombana na shangazi yake. Alimuuliza ni nini alikuwa amemfanyia. Mtoto alisimulia kwamba, alikuwa nyumbani na wakati huo alikuwa anataka kwenda kucheza mpira, japokuwa shangazi yake alimkataza kwa sababu alitaka kwanza afanye mazoezi aliyopewa shuleni. Kufautia na hilo, alimtukana shangazi yake hata kusema hilo tukano alilolisema. Hii yote, Papa amefafanua kwa  kurudi juu ya maneno ya  somo la Yohane anaposema “Ikiwa tunasema hatuna dhambi tunajidanganua wenyewe. Na hivyo anasema inabidi ndani ya dhamiri uhisi kusema kuwa  “Sitaki kuifanya tena, inaniumiza, ni muhimu na pia isi wenyewe tunatakiwa kuyapa majina dhambi zetu” Papa Francisko ameshauri.

Uthabiti unahitajika

Kadhalika Papa Francisko akiendelea kuelezea umuhimu wa uthabiti amekumbusha kuwa jana alipokea barua moja kutoka kwa mtoto mmoja aitwaye Andrea ambaye anadai kuwa anamsikiliza Papa kwenye televisheni wakati wa misa yake na kwamba alimkaripia kwa sababu, Papa wakati wa muda w kutakiana amani anatamka kuwa takianeni amani,  wakati huo huo wao hawawezi kufanya hivyo kwa sababu katika  kipindi cha janga ni katazo.  Kwa maana hiyo Papa amesema, ni lazima kuwa na hekima ya uthabiti, kwa sababu ibilisi anataka sisi tuishi katika ukungu na uvuguvugu. Haya ni maisha ambayo Bwana hapendi, amesisitiza Papa. Kwa kuhitimisha, amewaalika waamini wote kuomba Bwana neema ya kuwa watu rahisi, ile anayowapaita walio rahisi kama watoto na vijana ambao hawafichi lolote ambalo wanahisi ndani mwao.

29 April 2020, 13:37
Soma yote >