Tafuta

Vatican News
Misa ya Papa Francisko katika kikanisa cha Mtakatifu Marta. Misa ya Papa Francisko katika kikanisa cha Mtakatifu Marta.  (Vatican Media)

Papa amesali kwa ajili ya wazee wenye hofu kwa sababu ya janga!

Katika misa ya asubuhi kwenye kikanisa cha Mtakatifu Marta mjini Vatican Papa Francisko amesali kwa Bwana ili awe karibu na wazee walio pekee yao au kwenye vituo vya kuwatunza katika kipindi hiki kigumu.Katika mahubiri Papa Francisko amekumbusha uaminifu wa Mungu ambao unaendelea katika mchakato wa safari ya watu wake kama mwokozi.Uaminifu huu ni furaha kwetu sisi na unapasha joto mioyo.

Sr. Angela Rwezaula- Vatican

Katika Misa ya Papa Francisko katika Kikanisa cha Mtakatifu Marta mjini Vaticana siku ya Jumatano tarehe 15 Aprili tukia bado katika kipindi cha Pasaka, Papa Francisko  mawazo yake yamewaendea wazee na kusema, “tusali kwa ajili ya wazee hasa wale ambao wanaishi peke yao au katika nyumba  za utunzaji. Wao wana hofu; hasa  hofu ya kufa wakiwa peke yao. Wanahisi janga hili kama jambo la kuwasonga wao. Wao ni mizizi yetu, historia yetu. Wao wameotuonesha imani, utamaduni, maana ya kuwa wazalendo. Tusali kwa ajili yao ili Bwana aweze kuwa nao karibu katika wakati huu”. Papa Francisko akianza mahubiri yake kwa kutafakari masomo ya siku kutoka Matendo ya mitume 3, 1-10, mahali ambapo  kiwete tangu kuzaliwa, aliponyeshwa kwa njia ya maombi ya Petro akisema:“kwa jina la Yesu Kristo”, vile vile  na Injili ya siku kutoka Luka 24, 13-35, mahali ambapo Yesu Mfufuka anatembea na wafuasi  njiani huko Emau huku  akiwaelezea wao juu ya fumbo la kifo chake. Mitume wawili walimkaribisha katika nyumba na ndipo walipoweza kumtambua tu mezani wakati wa kuumega mkate, japokuwa alitoweka machoni pao.

Papa Francisko amethibitisha kuwa  Mungu ni mwaminifu katika ahadi zake, yeye yuko karibu na watu wake, anafanya wahisi kama mwokozi wa watu. Uaminifu wa Mungu ni  sikukuu na furaha kwa sisi sote, kama alivyomfanyia kiwete; ni uaminifu mvumilivu na hupasha  joto moyo kama  ilivyo watokea wafuasi  huko Emau. Uwepo wetu mwaminifu ni jibu katika uaminifu huu. Hata hivyo mahubiri ya Papa Francisko ameanza kwa kukumbuka siku ya Jumanne walivyotafakari kuhusu Maria Magdala  kwamba ni kama picha ya uaminifu, umanifu kwa Mungu. Lakini uaminifu huu wa Mungu ukoje? Ni mungu yupi?  Natoa jibu kwamba “Ni Mungu mwaminifu. Uaminifu wetu siyo mwingine zaidi ya kuwa ni jibu la uaminifu kwa Mungu. Mungu ni mwaminifu katika maneno yake ambayo ni ahadi yake na kwamba anatembea na watu wake  huku akipeleka mbele ahadi hiyo na watu wake.

Mwaminifu katika ahadi zake: Papa Francisko amesema ni Mungu ambaye mara nyingi anaendelea kufanya asikike kama mwokozi wa watu wake kwa sababu yeye ni mwaminifu. Mungu anauweza kufanya upya mambo na kuumba, kama alivyofanyia kiwete tangu kuzaliwa , aliumba miguu na kumfanya apone. Mungu anaponyesha; ni Mungu ambaye daima analeta faraja kwa watu wake. Mungu anaumba kwa upya. Uumbaji wake ni mpya, ndiyo uaminifu wake kwetu. Uumbaji mpya ni wa kushangaza sana. Ni Mungu ambaye anakwenda mbele na wala hachoki kufanya kazi, “instar laborantis”, kama wasemavyo wataalimungu  ili kupeleka mbele watu na wala hana hofu ya kuchoka… Kama yule mchungaji anapoingia nyumbani anatambua kuwa hakuna kondoo wake, anarudi nyuma kutafuta kondoo aliyepotea. Mchungaji anafanya jambo maalum, lakini kwa ajili ya upendo na kwa ajili ya uamanifu.

Mungu wetu ni Mungu anayefanya mambo maalum, lakini bila kulipwa, yeye anatenda bure. Ni mwaminifu wa utoaji wake na kwa wingi. Mwaminifu ni yule baba mwenye uwezo wa kuchungulia mara nyingi nje ili kutazama kama mwanaye mpotevu anarudi; yeye kamwe hachoki kupanda ngazi na kutazama mbali. Anasubiri ili afanye sikukuu. Uaminifu wa Mungu kwa maana hiyo ni sikukuu na furaha;  furaha kama hiyo ni kama ile aliyoifanya kwa kiwete kwa maana aliingia katika hekalu akiwa anatembea, anaruka ruka na kusifu Mungu. Uaminifu wa Mungu ni sikukuu na sikukuu ya bure na kwa ajili ya wote.

Uaminifu wa Mungu ni uaminifu mvumilivu. Mungu ana uvumilivu na watu wake, anawasikiliza, anawaongoza, anawaeleza kwa taratibu na kuwawasha moyo kama alivyo wafanya mitume wale wawili ambao walikuwa wanakwenda mbali kutoka Yerusalem. Anawasha mioyo yao  ili waweze kurudi nyumbani. Uaminifu wa Mungu ni ule ambao hatujuhi nini kilitokea katika mazungumzo yao, lakini ni Mungu mkarimu ambaye alimtafuta Petro, ambaye alikuwa amemkana. Tunachojua tu ni kwamba Bwana alifufuka na akamtokea Simon. Ni kitu gani lilitokea katika mazunguzo yao hatujuhi. Tunachotambua tu ni kwamba Mungu alikuwa mwaminifu na alimtafuta Petro. Uaminifu wa Mungu daima unatangulia mbele na  uaminifu wetu daima ni kama jibu la uaminifu ule ambao unatutangulia. Mungu anatutangulia daima. Yeye ni kama ua la mti  wa (mandorlo),au (almond ni mti ambao huchanua katikasehemu za joto) huchanua  maua katika mti huo ukiwa wa kwanza  Kuwa mwaminifu ni kusifu uaminifu huo; kuwa mwaminifu kwa uaminifu huo, ndiyo jibu la uaminifu huo amehitimisha Papa Francisko mahubiri yake. Kama kawaida ya misa zake maalum katika kipindi hiki cha chanja, anahitimisha kwa kuabudu ekaristo na kutoa baraka ya huku akiwaalika waamini ambao hawawezi kwenda kanisani kushiriki komunio ya tamaa.

15 April 2020, 10:32
Soma yote >