Tafuta

2020-04-19 Misa ya Papa Francisko katika kikanisa cha Mtakatifu Marta, Vatican 2020-04-19 Misa ya Papa Francisko katika kikanisa cha Mtakatifu Marta, Vatican  

Papa amesali kwa ajili ya wahudumu wa walemavu wenye covid-19!

Katika misa ya Papa katika kikanisa cha Mtakatifu Marta Vatican,wazo lake limewaendea walemavu waliokumbwa na virusi vya corona,madaktari na wauguzi wanaoshughulikia wao.Katika mahubiri Papa Francisko amebainisha kuwa mkristo anatambua kuzungumza kwa uwazi na ujasiri wa kusema ukweli na uhuru utokao kwa Roho Mtakatifu.

Na Sr. Angela Rwezaula -Vatican

Papa Francisko ameongoza misa ya asubuhi kama kawaida ya siku hizi maalum katika janga la virusi vya corona katika kikanisa cha Mtakatifu Marta Vatican, Jumamosi ya Pasaka tarehe 18 Aprili 2020 ikiwa ni tayari ni mkesha wa Dominika ya Huruma ya Mungu. Mawazo ya maombi yake katika Misa hii yamewaendea wahudumu wote wa afya, hasa madaktari na wauguzi wanaojikita kusaidia walemavu waliokumbwa na janga hili la corona. Papa Francisko akianza mahubiri yake, ameeleza kuwa alipokea barua kutoka kwa mtawa mmoja anayefanya kazi ya kutafsiri kwa lugha ya viziwi na ambaye alimweleza ilivyo ngumu kazi walio nayo wahudumu wa afya, wauguzi na madaktari wanaoshughulikia wagonjwa walemavu ambao wameambukizwa virusi vya covid-19. Hivyo amesema “tuombe kwa ajili yao ambao daima wanajikita katika huduma yao kwa ajili ya watu hawa ambao wana kila uwezo, japokuwa hawana kama ule tulio nao sisi”.

Katika sehemu ya kwanza ya mahubiri ya Papa Francisko ametafakari sehemu ya somo la Matendo ya Mitume (Mdo 4,13-21) mahali ambapo makuhani na akida wa hekalu walipoona ujasiri wa Petro na Yohane, na kuwajua ya kuwa ni watu wasio na elimu na maarifa, wakastaajabu, wakawatambua ya kwamba walikuwa pamoja na Yesu. Kwa maana hiyo  wakimwona yule aliyeponywa akisimama pamoja nao hawakuwa na neno la kujibu. Wakawaamuru kutoka katika baraza, wakafanya shauri wao kwa wao, wakisema tuwatishe wasiseme tena na mtu awaye yote kwa jina hili. Wakawaita, wakawaamuru wasiseme kabisa wala kufundisha kwa jina la Yesu.

Lakini hawa wawili Petro na Yohane wakawajibu kwa ujasiri na uwazi kabisa  wakawaambia, Kwamba ni haki mbele za Mungu kuwasikiliza ninyi kuliko Mungu, hukumuni ninyi wenyewe; maana sisi hatuwezi kuacha kuyanena mambo tuliyoyaona na kuyasikia. Uwazi kabisa Papa Francisko amesema ni neno muhimu, ni tabia ya wahubiri. Ni ujasiri wa mkristo unaomsukuma kuzungumza kwa uhuru.  Mioyo ya viongozi wa kidini hao ilikuwa imefungwa mbele ya uwazi huo, ilikuwa imeharibika. Roho Mtakatifu hawezi kuingia katika mioyo hiyo. Petro ambaye alikuwa ni kigeugeu mbele ya tishio la viongozi, anajibu kwa ujasiri. Je amepata kutoka wapi ujasiri huo? ni ule ujasiri utokanao na Roho. Mkristo anasema ukweli wote kwa sababu ni wa dhati amesisitiza Papa Francisko..

“Kuna sehemu ambayo naipenda sana katika barua ya Wahebrania:kuna kitu fulani ambacho katika jumuiya kinawasumbua, wakristo hawa walikuwa wamegeuka kuwa na vuguvugu.W Hawa wanakumbusha zile siku za kwanza, ya kwamba mmeweza kupambana sana na kwa ugumu na hivyo  msitupilie mbali ule uwazi na ujasiri wenu” Amebainisha Papa Francisko. Aidha ameongeza“ haiwezekani Mkristo hasiwe na ule uwazi kabisa. Kwa kutoa mfano amesema “Ikiwa unataka kueleza nafasi uliyo nayo unateleza katika itikadi za mawazo, lakini unakosa uhuru wa kuzungumza. Ni kama wazee hao viongozi na waandishi ambao ni waathirika wa uwazi huo. Badala ya kukubali ukweli waliokuwa wanauona lakini mioyo yao ilifungwa na  ambayo inatafuta njia nyingine zisizo halali. Wameweka uwazi pembeni na mioyo yao imeharibika”.

Aidha Papa Francisko ameendelea na tafakari kuhusu Injili ya siku(Mk16, 9-15)mahali ambapo Yesu kwa mara ya kwanza aliwakaripia mitume kutokana na mioyo yao kuwa migumu, kwa sababu hawakuamini kile kilichosemwa kuwa wamemwona mfufuka na baadaye anawashauri waende Dunia kote kutangaza kwa ujasiri Injili kwa kila kiumbe. Papa amesema utume unazaliwa kwa njia ya Roho Mtakatifu. Na sala ya mwisho ni ile ya kuomba Bwana atusaidie daima kuwa na ujasiri. Hii haina maana ya kukosa busara, bali ujasiri amebainisha Papa. Ni ujasiri wa kikristo ambao daima ni wenye burasa lakini pia ni ujasiri. Katika kitabu cha Matendo ya Mitume kimejaa habari za ujasiri huuo na ambao ulikuwa unaeleza  wayahudi kwa uwazi kuhusu fumbo la Yesu.

Kama kawaida ya kuhitimisha misa kwa kubudu ekaristi na kutoa baraka, wakati huohuo ni kuwaalika waamini wapokee ekaristi ya tamaa. Wakati wa kuondoka amesema kuwa misa ya Dominika itafanyikia katika Kanisa la Roho Mtakatifu saa 5.00, (majira ya Ulaya) na misa ya kawaida katika kikanisa cha Mtaatifu Marta  itakuwa Jumatatu saa moja.

18 April 2020, 10:19
Soma yote >