Tafuta

Tusali kwa ajili ya familia ili wasipoteze amani katika kipindi hiki kigumu na waweza kumudu katika  kupeleka mbele familia nzima kwa nguvu na hata furaha. Tusali kwa ajili ya familia ili wasipoteze amani katika kipindi hiki kigumu na waweza kumudu katika kupeleka mbele familia nzima kwa nguvu na hata furaha.  

Papa Francisko:Tuombe amani ndani ya familia katika kipindi kigumu!

Katika Kanisa la Mtakatifu Marta mjini Vatican,Papa Francisko amesali kwa ajili ya familia ili katika kipindi hiki kigumu amani na furaha na nguvu viweze kutawala.Amewakumbuka watu walemavu na katika Injili ameongozwa na sura ya mwana mpotevu.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Katika misa takatifu ya sita, mubashara katika Kanisa la Mtakatifu Marta mjini Vatican, tarehe 14 Machi 2020 Papa Francisko ameendelea kusali kwa ajili ya wagonjwa wa COVID-19 mawao yake yakiwaendea kwa namna ya pekee familia na watu walemavu. Katika utangulizi wa misa Papa amesema: “tuendele kusali kwa ajili ya watu waliokumbwa na janga. Leo hii ninaomba kwa namna ya pekee kusali kwa ajili ya familia ambazo siku hadi siku wanajikuta na watoto nyumbani, kwa sababu shule zimefungwa kwa ajili ya usalama na wanapaswa kukabiliana na hali halisi ngumu kwa kuikabili vizuri kwa amani hata kwa furaha. Kwa namna nyingine ninafikiria hata familia ambazo kuna walemavu. Vituo vya kuwapokea watu walemavu vimefungwa na watu hao wanabaki nyumbani. Tusali kwa ajili ya familia ili wasipoteze amani katika kipindi hiki na waweza kumudu katika  kupeleka mbele familia nzima kwa nguvu na furaha”.

Injili ya mwana mpotevu

Papa Francisko katika mahubiri ametafakari Injili ya mwana mpotevu na baba mwenye huruma kwa mujibu wa pendekezo la siku  (Lk 15, 1-3. 11-32). Papa amesema, mara nyingi tumesikia sehemu hiyo ya Injili. Mfano huo Yesu anasema katika muktadha maalum maana  “Walimkaribia Watoza ushuru wote na wenye dhambi kumiskiliza Yesu” . Mafarisayo na waandishi wakanung’unika, wakisema, “Mtu huyu huwakaribisha wenye dhambi, tena hula nao”. Yesu akawajibu kwa kutumia mfano. Papa amesema,  Je walikuwa wanamwambia nini? Watu watoza ushuru na wadhambi walikaa kimya, hawakuwa na lolote la kusema lakini uwepo unaonesha  mambo mengi, kwa maana walikuwa wanataka kusikiliza. Waandishi wa sheria  je wanasema nini ? wao walikuwa wakinung’unika kwa mujibu wa Injili kwa maana walikuta wanatafuta kufuta mamlaka ya Yesu aliyokuwa nayo juu ya watu. Hii ndiyo hukumu kubwa ya kwamba “ anawakaribisha na anakula na wadhambi, na hivyo ni najisi”.

Wadhambi walihisi kumba msaada

Katika mfano  huo unaelezea janga hili ambao ni tatizo Papa amesema. Je hawa walihisi nini? Hawa alihisi mahitaji ya wokovu. Watu hawa walikuwa ahajuhi kutengenisja mema na mazuri akilini. Kwa maana hiyo “ mimi ninahitaji kutafuta Bwana wangu ambaye awajaze, wanahitaji kiongozi na mchungaji”. Watu walikuwa wanamkaribia Yesu kwa kuwa walikuwa wanamwona ni Mchangaji na walikuwa wanataka kusaidiwa kutembea katika maisha. Watu hawa walihisi mahitaji hayo. Walimu wa sheria na  wengine wote wanahisi kujitosheleza  kwa maana ya kusema “ “Sisi tumekwenda chuo Kikuu, tumepata shahada”.  “Mimi niko vizuri na sheria inasema na zaidi ninatambua kila kitu, maelezo yote, kesi zote na tabia zozote za kisheria”. Papa anaongeza, “hawa walikuwa wanahisi kijitosheleza na kudharau watu, walikuwa wanadharau wadhambi na ndiyo dharau kwa wadhambi”. Katika mfano huo wao wanasemaje?  Papa bado anauliza swali. Yule mwana alimwambia babaye, “Baba, nipe sehemu ya mali inayoniangukia niondoke zangu” na Baba akampatia na hakusema kitu kwa sababu ni Baba labda alikuwa na kumbu kumbu ya mpenzi enzi za ujana wake , na kwa maana hiyo hasemi kitu. Baba anajua kuteseka kwa ukimya. Baba anasubiri wakati. Anaacha kipite kipindi kibaya. Wakati mwingine tabia ya baba ni kujifanya kama mpumbavu, mbele ya makosa ya watoto wao, Papa amefafanua. Mwana wake mkubwa  anamkaripia baba yake kwa kusema  “ hujatenda haki”. Je hawa walihisi nini katika mfano huo? Kijana mdogo alihisi mahitaji ya kushibishwa na  ulimwengu na kwenda mbali kutoka ndani ya nyumba, labda pale alihisi na kuishi kama mtumwa na hata kujiamini kumwamba Baba yake nipe sehemu ya mali inayoniangukia. Alihisi ujasiri na nguvu. Je baba yake?  Kinyume chake Papa anasema “ Baba yake alihisi uchungu, huruma na upendo mwingi.  Baadaye mtoto aliposema neno jingine kwamba “Alipozingatia moyoni mwake, alisema, nitaondoka, nitakwenda kwa baba yangu na alimkuta baba yake akimsubiri kwa maana alimwona kwa mbali. Baba anajua kusubiri nyakazi za watoto wao.

Mtoto mkubwa alikasirika na kudharau

Je  yule mtoto wake  mkubwa alisema nini? Injili inasema alikasirika na kuhisi kudharau. Mara nyingi kukasirika  ndiyo mtindo wa hisia za watu wale  . Lakini hayo ndiyo yanayoelezwa katika Injili  na mambo ambayo wanasikia.  Lakini je tatizo liko wapi? Tatizo linaanzia na mtoto mkubwa, kwa maana Yeye alikuwa anaishi nyumbani, lakini hakuwahi kutambua  nini maana ya kuishi nyumbani. Alikuwa anafanya wajibu wale, kazi yake, lakini hakuwa na utambuzi wa uhusiano wa upendo uliopo na baba yake.  Mwanae mkubwa alikasikirika na hakutaka kuingia ndani.  Alikuwa anafikiri hii siyo nyumba yangu tena?...  Mawazo yake yalikuwa kama ya walimu wa sheria.  Kwa kusema “hakuna utaratibu na sasa amefika mdhambi na kufanyiwa sherehe, je mimi? Katika Injili inafafanua wazi kwani baba yake anasema “Mwanangu, wewe u pamoja nami siku zote, na vyote nilivyo navyo ni vyako. Mtoto huyo hakuwa ametambua hilo mapema, alikuwa anaishi katika nyumba yake kama vile yuko kwenye nyumba ya kulala na hakuhisiubaba … Nyumba zipo nyingi za kulala katika nyumba ya Kanisa ambazo inaamini ni bwana. Inashangaza, kwani baba yake  hasemi neno kwa mwanaye ambaye amerudi kutoka dhambini, anafanya tendo la kumbusu tu, kumkumbatia na kumfanyia sherehe; kinyume chake mwingine lazima amfafanulie ili aweze kuingia ndani ya moyoni mwake. Alikuwa na moyo ulifungwa sana kuhusiana na mantiki ya baba yake ya kuwa mwana na kwa namna ya kuishi.

Mdhambi na mnyenyekevu anahisi kuomba msamaha

Papa Francisko kufuatia na fafanuzi hiyo amekumbuka kuwa kulikuwa na padre mmoja mzee mwenye busara, na alikuwa ni muungamishi mkubwa ambaye alikuwa ni mmisionari, mwanaume aliyekuwa anapenda Kanisa sana na ambaye  akizungumza na padre mmoja kijana mwenye kujiamini sana na mwaamini sana, … ambaye alikuwa wa thamani sana na ambaye alikuwa na mamlaka fulani katika Kanisa alisema lakini “ mimi ninasali kwa ajili hiyo ili Bwana aweze kuweka ganda la ndizi na kumfanya ateleze  kwa kile ambacho kimtamtende mema”. Jambo hili Papa Francisko amesema utafikiri alikuwa anakashifu yaani kufanya atende dhambi ndipo atakuwa na haja ya kuomba msamaha na kumjua Baba yake. Mambo mengi yanaoneshwa katika mfano wa Bwana na ambapo ni jibu kwa wale ambao wananung’unika na kukejeli Bwana kwamba alikuwa anakaa na wadhambi. Hata hivyo Papa Francisko amesema  leo hii wananung’unikia watu wa Kanisa ambao wanakaribia wenye kuhitaji msaada, watu wanyenyekevu watu ambao wanafanya kazi na ambao wanafanya kazi kwa ajili yetu.  Akihitimisha Papa Francisko amesema “Bwana tupatie neema ya kutambua matatizo yako wapi. Matatizo ni kuishi katika nyumba lakini bila kuhisi nyumbani, kwa sababu hakuna ule uhusiano wa ubaba, wa udugu, bali kuna uhusiano wa kusindikizana kikazi tu.

MAHUBIRI-PAPA
14 March 2020, 10:28
Soma yote >