Tafuta

Bwana anatualika sisi sote wadhambi kuzungumza na Yeye kwa sababu dhambi inatufunga sisi binafsi.Lazima kumweleza Bwana dhambi zetu aliye na uwezo wa kubadili kila kitu.  Bwana anatualika sisi sote wadhambi kuzungumza na Yeye kwa sababu dhambi inatufunga sisi binafsi.Lazima kumweleza Bwana dhambi zetu aliye na uwezo wa kubadili kila kitu.   (VaticanMedia)

Papa Francisko:makuhani pelekeni Ekaristi kwa wagonjwa wa corona

Misa ya pili ya Papa Francisko ya moja kwa moja kupitia Kanisa la Mtakatifu Marta mjini Vatica nia yake ni kuwatia moyo wahudumu wa afya ambao wanapambana dhidi ya COVID-19 na sala kwa ajili ya wagonjwa.Katika sala ya leo pia ameongeza nia nyingine kwa makuhani ili waweze kutoka na kupeleka Ekaristi kwa wale ambao hawawezi kutoka nje.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Papa Francisko hata  Jumanne tarehe 10 Machi 2020 wakati wa kuanza misa Takatifu katika Kanisa la Mtakatifu Marta mjini Vatican amekumbusha jinsi Jumatatu wavyosali kwa nia ya  wale wanaoteseka kwa sababu ya  Vurusi vya COVID-19 , kwa ajili ya wale wanao wahudumia na kwa kuwasindikiza kwa matashi mema. Kwa mujibu wa misa ya Jumanne asubuhi Papa Francisko ameongeza nia ya kusali kwa ajili ya “makuhani, ili waweze kuwa na ujasiri wa kutoka na kwenda kwa wagonjwa, kuwapelekea Neno la Mungu na Ekaristi na kuwasindikiza wahudumu wa afya, watu wa kujitolea katika kazi yao ambayo wanaendelea kufanya”. Katika mahubiri yake kwa kuongozwa Injili ya Siku kutoka  Mt 23,1-12, ambayo inaelezea juu ya waandishi na mafarisayo wakati wa kipindi chao cha uongozi wa kinafiki, wa kujidai mbele ya watu huku wakitaka waitwe walimu wakati huo huo wakikataa kuwa waadilifu katika mienendo yao.

Papa Francisko amesema, “jana Mungu alikuwa anatufundisha kutambua dhambi zetu na kutubu, lakini si katika akili tu bali kutoka undani wa moyo na kwa roho ya aibu; Aibu ni kama tabia njema mbele ya Mungu kwa ajili ya dhambi zetu. Leo hii Bwana anatualika sisi sote wadhambi kuzungumza na Yeye kwa sababu dhambi inatufunga sisi binafsi,  inatufanya kuficha ukweli wetu na ikiwa unahisi aibu, lakini kishawish kinakufanya ufiche ukweli huo wa ndani. Jambo hili ndilo liliwatokea Adamu na Eva baada ya kutenda dhambi walijificha kwa sababu walikuwa na aibu na maana walikuwa uchi.

Mdhambi anahisi kuwa na dhambi, anaona aibu lakini ana kishawishi cha kutaka kujificha na kwa maana hiyo  Bwana anatuita  akisema:“Haya, njoni, tusemezane yaani tuzungumze juu ya  dhambi zako, tuzungumzie hali yako . “Usiwe na hofu anaongeza, “Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji; zijapokuwa nyekundu kama bendera zitakuwa kama sufu (Is. 1:18).”. “ Njooni kwa sababu mimi nina uwezo wa kubadili kila kitu asema Bwana “ msiwe na hofu ya kuja kuzungumza, kuweni jasiri hata kwa dhambi zenu hizo”. Papa anasema.  

Papa Francisko aidha amekumbuka mfano wa mtakatifu mmoja ambaye amesema  alikuwa ni muungama na alikuwa anasali sana. Yesu alikuwa anajaribu kumpatia Bwana kile ambacho Bwana alikuwa anamwomba atende. Licha ya hayo yote Bwana hakufurahia juu ya ke.  Ndipo siku moja huyo mtakatifu alikuwa kidogo amekasirika dhidi ya Bwana, kwa maana alikuwa na tabia kidogo ngumu.  Alimwambia Bwana: “Lakini Bwana mimi sikuelewi. Mimi ninakupatia kila kitu, lakini wewe daima huridhiki kama vile unakosa jambo fulani. Je ni kitu gani unakosa?" Na Bwana  alijibu na kusema: “Nipe dhambi zako, ndicho kitu ninachokosa.”.

Kwa maana hiyo Papa ameongeza kusema ni kuwa na ujasiri wa kwenda kwa Bwana na dhambi ulizo nazo na kumsimulia yote kwa  maana yeye anarudia kusema:“Njoo tusemezane. Usiwe na hofu. Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji; zijapokuwa nyekundu kama bendera zitakuwa kama sufu”. Huo ndiyo mwaliko wa Bwana . Lakini daima kuna ulaghai  ambao badala ya kwenda kuzungumza na Bwana, ni kujifanya huna dhambi, amesisitiza Papa.  Ndiyo jambo ambalo Bwana anakemea kwa waandishi wa sheria. Watu hao wanafanya matendo yao ili waweze kutazamwa na watu…wao hunena lakini hawatendi. Wao hufunga mizigo mizito na kuwatwika watu mabegani mwao; wasitake wenyewe kuigusa kwa kidole chao; kwa kuwa hupanua hirizi zao, huongeza matamvua yao; hupenda viti vya mbele katika karamu, na kuketi mbele katika masinagogi, na kusalimiwa masokoni, na kuitwa na watu, Rabi.

Uwazi na ukweli unafichwa kwa maana ya kufunika ukweli wa moyo na ubatili mtupu. Ubatili hauponi kamwe, anasema Papa.  Hata sumu inaingia na kuendelea mbele kwa kuufanya moyo uugue na kuupelekea ugumu wa moyo na ambao nakuvuta “usiende kwa Bwana bali ubaki tu. Ubatili ndiyo nafasi ya kujifunga binafsi bila kusikiliza wito wa Bwana. Kinyume chake, mwaliko wa Bwana mi ule wa Baba, wa ndugu, usemao njooni tusemezane. Hatimaye mimi nina uwezo wa kukubadili maisha yako kutoka katika wekundu na kuwa mweupe. Papa Francisko amehitimisha kwa kuomba Bwana atupe ujasiri na kwamba sala zetu ziwe sala za kweli. Hali halisi yetu, ya dhambi zetu, maana yetu. Kuzungunza wazi  na Bwana kwa maana yeye anajua sisi ni nani. Sisi tunajua lakini ukweli huo tunaufunika na kwenda mbele. Bwana anatusaidie.

MAHUBIRI-PAPA
10 March 2020, 13:28
Soma yote >