Katika Misa ya Papa Tarehe 27 Machi 2020 amesema mbele ya kukabiliwa na roho ya ghadhabu, inabidi kuwa na ukimya tu hakuna kuhesabiwa haki kamwe! Katika Misa ya Papa Tarehe 27 Machi 2020 amesema mbele ya kukabiliwa na roho ya ghadhabu, inabidi kuwa na ukimya tu hakuna kuhesabiwa haki kamwe!  (ANSA)

Papa Francisko amewashukuru watoa huduma kwa wahitaji!

Katika Misa ya asubuhi,kwenye kikanisa cha Mtakatifu Marta Vatican,mawazo ya Papa Francisko kwa upya ni kwa ajili ya wagonjwa,wazee walio na upweke,familia ambazo hazijuhi zifanye nini pia akatoa shukrani kwa wale ambao wanajishughulia kutoa msaada kwa watu hawa.Katika mahuburi amesisitiza juu ya ghadhabu kutokana na ibilisi anayeharibu.Ameshauri jibu ni ujasiri wa kunyamaza.Yesu alifanya hivyo na inatakiwa kukabiliana vizuizi hivyo vidogo kama vile domo.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Katika Misa iliyotangazwa moja kwa moja na vyombo vya habari Vatican  katika Kanisa la Mtakatifu Marta, Papa Francisko tarehe 27 Machi 2020 ameweza kuonesha shukrani kubwa kwa wale ambao wanafikiria wengine katika wakati huu mgumu wa maambukizi ya virusi vya corona- covid-19. Katika utangulizi wa maadhimisho  Papa Francisko amesema: “Siku hizi zinafika habari za watu wengi ambao wameanza kuwa na wasi wasi kwa ujumla  na kushughulikia  wengine, kama vile na wanafamilia ambao hawajuhi namna ya kuish,i wazee walio peke yao, wagonjwa katika mahospitali na hivyo hawa, wanaomba na kutafuta namba ya kuweza kuwafikishia msaada… Hii ni ishara nzuri. Tumshukuru Bwana ili aweze kuongeza hisia hizi ndani ya mioyo ya waamini”.

Wakati wa mahubiri yake, Papa ametafakari masomo ya siku kutoka Kitabu cha Hekima  (Hekima 2, 1. 12-22) na Injili ya Yohane (Yh 7, 1-2. 10. 25-30),  kwa kelezeaa juu ya ghadhabu kwa wale ambao walikuwa wanataka kumuua Yesu na kwamba ilikuwa inatokana na shetani, kwa sababu nyuma ya kila ghadhabu ya kuharibu, kuna ibilisi. Huwezi kujadiliana na mwenye ghadhabu, bali unaweza kunyama tu, kama alivyo fanya Yesu ambaye alichagua ukimya na Mateso. Ndiyo mtindo wa kufuata hata kwa ghadhabu ndogo ndogo za kila siku na midomo. Papa Francisko amesema : Somo la kwanza ni karibia  ya taarifa (iliyotangulia) kwa kile ambacho kitamtokea Yesu. Ni taarifa iliyo mbele ni unabii. Utafikiri inaelezea historia ya kile  kitakachotokea baadaye!

Je wasio msadiki Mungu walisema nini?  Anajibu kwa kusoma somo la siku kwamba: Na tumhakikishe kwa jeuri na maumivu, huku wakimfikiri yasiyo kweli, Zaidi ya hayo na tumwotee mtu wa haki, maana hatuna haja naye, naye yu kinyume cha matendo yetu; atukaripia ya kama tumeiasi torati, na kutushitaki ya kama tumekosa adabu. Asema ya kwamba anamjua Mungu, na kujiita mtumishi wa Bwana. Ametuwia magombezi ya fikira zetu. Hata kumtazama twaona ni kugumu; maan amaisha yake si sawasawa na masiha ya wengine, na mwenendo wake ni wa kigeni. Tunahesabiwa naye kuwa kama madini hafifu; anajitenga na njia zetu kama na uchafu. Wenye haki asema kuwa mwisho wao ni heri; hujivuna ya kwamba Mungu ndiye baba yake. Na kama kweli ni mwana wa Mungu atakuja kumsaida na kumwondoa katika mikono ya maaduia zake. Tufikirie yale ambayo walikuwa wanamweliza Yesu juu ya msalaba.

Papa ameendelea kufafanua: Wewe kana ni mwana wa Mungu telemka na Yeye atakuja kukuokoa. Na baadaye ni hatua za utekelezaji. “Haya tumweke katika majaribu na  tuone kama maneno yake ni kweli; tufanye kujaribu yatakayompata wakati wa mwisho wake; mradi mwenye haki akiwa ni mwana wa Mungu, Yeye atamtegemeza na kumwokoa mikononi mwa adui zake. Na tumhakikishe kwa jeuri na maumivu, ili tujifunze upole wake na kuithibitisha saburi yake akidhulumiwa. Hata tumhukumu auawe mauti ya aibu, maana ataangaliwa sawasawa na maneno yake”.

Papa Francisko mesema : “Haya maneno ni unabii wa kile ambacho kilitokea, Wayahudi walitafuta namna ya kumuua, Injili inasema. “Walitafuta namna ya kumkamata; lakini hakuna mtu aliyeunyosha mkono wake ili kumshika, kwa sababu saa yake ilikuwa haijatimia bado”. Unabii huo umeelezewa vizuri sana amesema Papa, mipango ya watu hawa wakatili ndiyo mipango hasa juu yake, haijali lolole, tumweke katika majaribu!. Hii ndiyo inaitwa ghadhabu hasa shetani ambaye yuko nyuma daima kwa kila ghadhabu anatafuta kuharibubila kujali lolote. Tufikie mwanzo wa Kitabu cha Ayubu, ambacho ni unabii wa jambo hili. Mungu alikuwa amependezwa na namna yake ya kuishi na shetani akasema: kwa kuwa ana kila kitu,  hana majaribu na tumjaribu tuone!

Kwanza shetani alimwondolea mali yake na kumwondolea afya yake, lakini Ayubu hakumwacha Mungu. Lakini ndizo njia za shetani ambazo anatumia na kuwa na ghadhabu daima. Nyuma ya ghadhabu kuna shetani ambaye anataka kuharibu kazi ya Mungu. Nyuma ya malumbano au uadui inawezekana akawepo shetani, japokuwa kwa mbali na kujificha huku akitumia vishawishi vya kawaida. Ghadhabu hizi ni finyu sana. Tufikirie jinsi ambavyo shetani alikasirikia si tu, dhidi ya Yesu, lakini hata kwa mateso ya wakristo. Ni jinsi gani alitafuta vyombo zaidi vilivyojificha ili kumkana Mungu, yaani kwenda mbali na Mungu. Hayo ni kama tunavyosema kwa lugha ya kawaida kwamba ndiyo akili ya ushetani. Akitolea mfano mmoja, Papa Francisko amesema, kuna baadhi ya maaskofu katika nchi ambazo zilikumbwa na udikteta wa kumkana Mungu na ambao walifikia hatua ya kutesa watu,lakini kwa namna finyu ya kutafuta wakristo. Kwa mfano Jumatatu baada ya Pasaka, walimu waliweza kutumia njia ya kuwauliza watoto kwa ujanja kuwa: “je ni mlikula nini jana?

Watoto walisema kile ambacho walikula. Baadhi walisema “Mayai”, na wale waliokuwa wamesema mayai, walipata kuteswa kwa maana wakristo katika nchi hizo walitumia utamadunu wa kula mayai wakati wa siku ya Dominika ya Pasaka.Kwa maana hiyo Papa Fancisko ameongeza kusema “Hadi kufikia hatua hii, kufanya , udadisi na kudakua, mahali ambapo kuna Mkristo na kumuua. Hii ni ghadhabu katika mateso na huyo ndiye Ibilisi! Je ni jinsi gani ya kufanya wakati huo wa ghadhabu? Papa anajibu: inawezekana kufanya mambo mawili tu kwanza kuadiliana na watu kama hao siyo rahisi kwa sababu wanayo mawazo yao ambayo ibilisi amepanda ndani ya mioyo yao. Tumesikia mipango yao ya utekelezaji. Je nini kifanyike? Kile ambacho alifanya Yesu. Kunyamza. Inashangaza tunapsoma katika Injili kwamba mbele ya ya mambo hayo yote hata mashtaka hayo Yesu alibaki kimya.  Kwa maana hiyo mbele ya kukabiliwa na roho ya ghadhabu, inahitajika kuwa na ukimya tu, hakuna kuhesabiwa haki kamwe! Yesu alipotambua kuwa hakuna maneno, alikaa kimya tu. Na kwa ukimya Yesu aliteseka.

Ni ukimya wa mwenye haki mbele ya ghadhabu. Na hii pia ni sahihi hata kama tuiite maneno madogo ya kila siku,  Papa Francisko amesisitiza n ahata wakati mwingine watu wanahisi kuwa kuna domo juu yao na wanasemwa vitu na kisha hakuna kitu kinachotokea …lazima  kukaa kimya. Na kuteseka na kuvumilia ghadhabu ya domo. Domo pia ni ghadhabu na ghadhabu ya kijamii. Katika jamii, kitongoji,  mahali pa kazi, lakini daima dhidi yao. Ni gadhabu isiyo na nguvu,  japokuwa  ni ghadhabu kwa ajili ya kuharibu mwingine kwa sababu mwingine anamwona kuwa anamsumbua,na pia wivu. Kwa kuhitimisha mahubiri yake Papa Francisko amesema: “tuombe Bwana neema ya kupambana dhidi ya roho mbaya na  kujadili wakati tunapaswa kujadili; lakini mbele ya roho ya ghadhabu ni kuwa na ujasiri wa kukaa kimya na kuacha wengine wazungumze. Hiyo ni sawasawa, hata mbele ya ghadhabu ndogondogo za kila siku ambazo ni domo, tuache wazungumze. Tubaki kwa ukimya mbele ya Mungu! Na mwisho Papa Francisko amehitimisha kwa kuabudu sakramenti na kutoa baraka huku akiwaalika waamini washiriki komunia ya tamaa. Kabla ya kuacha Kanisa Papa ameshiriki wimbo wa Maria kwa lugha ya kilatini Regina Caelorum “Ave Regina dei Cieli”...

PAPA-MISA

 

 

 

27 March 2020, 10:59
Soma yote >