Papa anasema Nabii Yeremia kiukweli alikuwa anatabiri juu ya Mateso ya Bwana.Je maadui  hao wanasema nini? Njoni na tumpige kwa ndimi zetu,wala tusiyaangalie maneno yake yoyote. Papa anasema Nabii Yeremia kiukweli alikuwa anatabiri juu ya Mateso ya Bwana.Je maadui hao wanasema nini? Njoni na tumpige kwa ndimi zetu,wala tusiyaangalie maneno yake yoyote.  (Vatican Media)

Papa Francisko amesali kwa ajili ya wafungwa katika wakati mgumu

Katika misa ya ya asubuhi Jumatano tarehe 11 Machi 2020,Papa Francisko ameendelea kuombea wagonjwa wa virusi vya Corona na wazo pia limewaendea kwa namna ya pekee wafungwa.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Katika Misa Papa Franciko kwa siku ya tatu ikiwa mubashara katika Kikanisa cha Mtakatifu Marta mjini Vatican ameendelea kuwaombea wagonjwa wa Virusi vya Corona na wazo pia limwaendeea wafungwa katika magereza. Papa akianza mahubiri amesema “Tunaendelea kuwaombea wagonjwa wa janga hili. Na leo, kwa namna ya pekee, ninapenda kuwaombea wafungwa, kaka  na dada zetu waliofungwa. Wanateseka na lazima tuwe karibu nao kwa maombi ili Bwana awasaidie, awafariji katika wakati huu mgumu”. Papa Francisko amesoma sala mwanzoni mwa liturujia kwa kusema:“Wewe, Bwana, usiniache, Mungu wangu, usijitenge nami. Ufanye haraka kunisaidia, Ee Bwana, wokovu wangu”. (Zab 38,22-23).

Kwa kuongozwa na  masomo ya siku Papa Francisko amezungumza juu ya mateso ya Yesu kwa kubainisha ni kwa jinsi gani ibilisi ndiye  anaye haribu kwa kutumia mtindo wake maalum gadhabu. Kuna ulaghai ambao ibilisi anautumia ili kufanya uende mbali na Msalaba kwa kukuelekeza katika roho ya kidunia kama vile ya kutaka nguvu, ubatili, lakini pia kuwa na ghadhabu. Papa amewakumbuka juu ya Wakristo wengi waliotesa kwa maana hiyo amemtaja hata Asia Bibi.  Katika somo la Kwanza, Nabii Yeremia kiukweli alikuwa anatabiri juu ya Mateso ya Bwana. Je maadui  hao wanasema nini?Njoni, na tumpige kwa ndimi zetu, wala tusiyaangalie maneno yake yoyote. Kwa maana hiyo tumwekee vizingiti. Hawasemi “tumshinde na kumtoa nje hapa Papa anasema na kuongeza kuwa:“Wanasema kumtendea ili awe na maisha magumu na kumtesa. Ni mateso ya nabii, japokuwa hapo ndipo kuna unabii juu ya Yesu. Katika Injili pia Yesu anazungumza hilo: “Angalieni, tunapanda kwenda Yerusalemu; na Mwana wa Adamu atatiwa mikononi mwa wakuu wa makuhani na waandishi nao watamhukumu afe; kisha watampeleka kwa Mataifa wapate kumdhihaki, na kumpiga mijeledi na kumsulibisha; na siku ya tatu atafufuka”.

Kuna kunyenyekeza, kuna ghadhabu. Siyo hukumu ya kifo tu Papa anasema, bali kuna jambo jingine zaidi. Kuna kufedhehewshwa na gadhabu.  Na ikiwa  kuna ghadhabu katika mateso ya Mkristo, ya mtu, hapo kuna Ibilisi. Shetani ana mitindo miwili, awali ya yote ni  ujanja na ahadi za ulimwengu, kama alivyotaka kumfanyia Yesu kule jangwani, kumlaghai kwa ujanja ili amfanye  abadilishe mpango wa ukombozi, na ikiwa hiyo haitakwenda basi ni gadhabu. Pepo hana maneno ya kukosolewa kwa maana kiburi chake ni kikubwa sana, kiasi kwamba anajaribu kwa njia zozote kutaka  kuharibu na kuharibu huku akifurahia uharibifu huo kwa ghadhabu.

Katika kuendelea na tafakari hiyo Papa Francisko amewaalikwa waamini tufikirie mateso ya watakatifu wengi na wakristo wengi wanaouwawa, lakini pia hata wanaoteswa na wakutafutiwa kila njia ya kuwadhalilisha hadi kufikia kifo chao. Usichanganye manyanyaso rahisi ya kijamii, kisiasa, kidini na gadhabu ya shetani. Shetani anaendelea kuwa na gadhabu ya kuharibu. Fikirieni katika historia ya Mwisho wa dunia anapotaka kumla mtoto wa yule ambaye yuko karibu kuzaliwa na mwanamke. Majambazi wawili waliokuwa wamesulibishwa na Yesu, walihukumiwa na kusulilibiwa na kuwaachwa wafe kwa amani pale. Hakuna hata mmoja aliyekuwa akiwasuta na wala kuwajali. Papa Francisko amefafanua  lakini matusi yalikuwa yameelekezwa kwa Yesu tu, dhidi ya Yesu.

Yesu aliwaambia mitume kwamba atahukumiwa  na kuuawa, lakini pia atadhihakiwa, atakashambuliwa, atasulibiwa ... wao wakamdhihaki. Na njia ya kuondokana na ghadhabu ya ibilisi, kutoka katika  uharibifu huu, ni roho wa ulimwengu ni kama ya mama anayeombea watoto, yaani watoto wa Zebedayo katika Injili ya Siku. Yesu aliziungumza  juu ya kufedheheshwa, ambayo ni hatma yake mwenyewe na huku mama na watoto wake wanamuomba yale ya muonekana wa kijuu juu, yaani madaraka na nguvu. Ubatili na roho ya ulimwengu ni njia halisi ambayo shetani utumia ili uweze kuondoka na Msalaba wa Kristo. Utimilifu wa kibinafsi, taaluma kibinafsi, mafanikio ya kidunia vyote hivyo ni barabara zisizo za Ukristo, zote ni njia za kufunika Msalaba wa Yesu, Papa amesisitiza.

Kadhalika Papa akiendelea kufafanua mesema: “Bwana atupe neema ya kuweza kutambua na kung’amua wakati ambao kuna roho inayotaka kutuangamiza kwa hasira na gadhabu na wakati huo huo, kutambua hata roho inayotaka kututuliza na kuonekana kijuu  juu katika ulimwengu na kwa ubatili. Kwa maana hiyo  Papa anaonya kuwa“tusisahau kuwa wakati kuna ghadhabu, kuna chuki, kulipiza kisasi jua kwamba shetani ameshindwa! Ni hivyo mpaka leo, hii  katika  Kanisani. Tufikirie Wakristo wengi, jinsi wanavyoteswa kikatili. Siku hizi, magazeti yamezungumzia juu ya Asia Bibi. Yeye kwa miaka tisa alibaki gerezani na kuteseka. Ni hasira na gadhabu ya shetani. Bwana atupatie  neema ya kutambua njia ya Bwana, ambayo ni Msalaba na kutoka njia ya ulimwengu, ambayo ni ubatili, muonekano wa wa nje tu  na  kujitengeneza.

MAHUBIRI PAPA

 

11 March 2020, 13:32
Soma yote >