Vatican News
Tuombe  neema ya  habari zote za machungu  ya wanadamu ambayo tunayo, iweze kushuka ndani ya mioyo na  kutuchochea kufanya jambo fulani kwa wengine. Tuombe neema ya habari zote za machungu ya wanadamu ambayo tunayo, iweze kushuka ndani ya mioyo na kutuchochea kufanya jambo fulani kwa wengine.  (Vatican Media)

Papa Francisko amesali kwa ajili viongozi bila kusahau maskini!

Katika Misa ya Papa Francisko kwa nia ya kuombea waathirika na wahudumu wa virusi vya Corona ameomba pia kusali kwa ajili ya wenye mamlaka ya kuchukua maamuzi mbele ya janga la Virusi vya Corona.Katika kipinid hiki pia emeshauri wasihau watu ambao wanahitaji,watoto wenye njaa na wale wanaokimbia vita kwa maana ni wengi ambao wanazuiwa na kuta za na waya zenye miiba mikali.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Papa Francisko tarehe 12 Machi ameendelea kutusindikiza katika kipindi hiki kigumu kwa Misa Takatifu katika Kanisa la Mtakatifu Marta Vatican. Ni maadhimisho ya Ekaristi ya Nne kusikika mubashara. Mwanzoni mwa utangulizi Papa Francisko amewaalika waamini kusali kwa namna ya pekee ajili ya wenye mamlaka: “Tuendelee kusali  kwa pamoja katika kipindi hiki cha janga, kwa ajili ya wagonjwa, familia zao, kwa anjili ya wazazi na watoto wao nyumbani… na zaidi leo hii ninaomba tusali kwa ajili ya wenye mamlaka. Wao wanatakiwa kuamua na mara nyingi hutoa maamuzi ya hatua ambazo watu hawapendi. Lakini ni kwa ajili ya wema wetu. Mara nyinyi wenye mamlaka uhisi kuwa pekee yao kwa njia hiyo Papa amesisitiza kuwa “Tusali kwa kwa ajili ya viongozi watawala ambao wanapaswa watoa maamuzi juu ya hatua hizi na ili wahisi wanasindikizwa na maombi ya watu”.

Papa Francisko akianza kutafakari Injili ya Siku inayohusu Tajiri na Maskini Lazaro (Lk 16,19-31),ameshauri kuacha tabia ya kuwa na sintofahamu mbele ya  janga hasa ka kwa watoto;  mbele ya watu wale wanaokimbia vita na kukutana mbele yao hata kuta. Papa Francisko anasema simulizi ya Yesu ina utajiri mkubwa sana hata kama unaweza kufikiria ni hisotria ya watoto wadogo lakini ni rahisi sana. Yesu anataka kutuelekeza kuwa kwamba si katika historia, lakini hata uwezekano wa ubinadamu hai kwa maana hata leoho hii sisi sote tunaishi uzoefu huo. Watu wawili, mmoja aliyetosheka aliyekuwa anavaa vizuri na labada alikuwa anatafuta mshonaji marufu  wa mavazi ya nyakati zile: “alikuwa akivaa nguo za rangi ya zambarau na kitani safi, na kula sikuzote kwa anasa”.  Papa anasema, Yeye alikuwa na furaha ya namna hii. Hakuwa na wasi wasi wowote, alikuwa anafanya taadhari labda hata kutafuta  dawa ya kupunguza mafuta mwilini kutokana na ulazi wake na kwa maana maisha yake yalikuwa namna hiyo na alikuwa na utulivu.

Katika mlango wake alikuwapo  maskini mmoja, jina lake Lazaro. Yeye alikuwa anajua kama yupo maskini huo pale . Lakini ilionekana jambo la kawaida. Papa anaongeza  “Ninafanya vizuri na hii ... lakini, ndivyo pia maisha, ajijue”. Labda hata kama Injili haisemi hili, wakati mwingine inawezekana alikuwa kimtumia chochote labda makombo. Na ndivyo maisha yanaendelea mbele kwa watu hawa wawili. Wote wawili walipitia Sheria ya sisi sote, yaani ya  kufa. Tajiri alikufa na Lazaro akafa. Injili inasema kwamba “Lazaro alipelekwa Mbinguni, karibu na Ibrahimu”... kwa upande wa tajiri Injili inasema kuwa “alizikwa basi na kuisha”. Hapa kuna mambo mawili yanayoshangaza;  na hili ni jambo ambalo tajiri alikuwa anajua kwamba yupo masikini na kwamba alikuwa anatambua jina lake kuwa ni  Lazaro. Lakini hakujali na ilikuwa kama kitu cha kawaida. Tajiri labda pia alifanya biashara yake ambayo hatimaye ilikwenda dhidi ya maskini. Alikuwa anajua wazi na alikuwa amepewa habari ya hali halisi hii. Na jambo la pili ambalo Papa Francisko linamgusa sana ni neno la “kuzimu” ambalo Ibrahimu anamweleza tajiri na kusema kuwa:  “Na zaidi ya hayo, kati yetu sisi na ninyi kumewekwa shimo kubwa”, Papa anaongeza kuseam  kwa maana hatuwezi kuwasiliana, hatuwezi kuvuka sehemu moja kwenda sehemu nyingine. Na hili ndilo shimo kubwa ambalo katika maisha yao ilikuwa kati ya tajiri na Lazaro. Shimo kubwa kumbe halikuanzia kule kuzimu bali lilianzia hapa hapa. Papa Francisko  amefafanua.

Papa Francisko amefikiria ni kwa jinsi gani huyo mtu alipitia janga hili, janga la kuwa na mengi, japkuwa yeye moyo wake ulikuwa umefungwa. Habari za tajiri huyo zilikuwa hazifiki katika moyo wake. Hakuwa na mshtuko wa ndani  na wala hata kuguswa majanga ya wengine. Hakuweza kumwita mmoja wa watumishi wake ambao walikuwa wanamtumikia mezani ili kuweza kumepelea masikini Lazaro chochote. Alipata taarifa laki taarifa hizo hazikuweza kupenya ndani ya moyo wake na jambo ni jambo ambalo linagusa hata maisha yetu sisi amesema Papa. Sisi sote tunajua kwa sababu tumesikia kupitia katika luninga au tumsona kupitia katika magazeti, watoto ambao wanateseka na njaa leo hii ulimwenguni; watoto wangapi ambao hawana madawa muhimu; watoto wangapi ambao hawawezi kwenda shule.  Mara nyingi janga hili tunalisikia katika mabara na tunajua lakini tubakia kuishi na kuendelea mbele bila kufanya chochote. Hatuguswi na lolote. Habari hizi hazishuka katika moyo kwa kina, wengi wetu, makundi ya wanaume na wanawake ambao amesema wanaishi mbali kabisa kati ya kile ambacho wanafikiria, kile ambacho wanajua na kile ambacho wanasikia. Kwa maana moyo umetengana na akili, hawajali  ni kama yule tajiri ambaye hakujali uchungu wa Lazaro. Papa Francisko amebainisha kuwa, kutokana na jambo hili ni wazi kwamba kuna umbali kama wa kuzimu wa kutojali. Akitolea mfano Papa Francisko amekumbusha alivyokwenda Lampedusa kwa mara ya kwanza na  aliijiwa na neno akilini mwake kuhusu utandawazi wa sintofahamu. Labda leo hii jiji Roma amesema , “tunaangaika kwa sababu maduka yamefungwa na wakati huo mmoja anafikiria “ninapaswa kwenda kununua hiki na kile, na wala sitoweza kufanya matembezi ya kila siku, mahangaiko ya mambo yangu tu”.

Tunasahau lakini watoto wenye njaa, tunasahamu maaskini, watu wale ambao wako mipaka ya nchi wakitafuta uhuru, wahamiaji wa kulazimishwa ambao wanakimbia njaa na vita na wanakutana na kuta tu; kuta ma waya zenye miiba mikali, na ni kuta ambazo zinawazuia wasiweze kupita. Tunatambua jinsi mambo hayo jinsi yalivyo na yapo lakini hayaingii ndani ya mioyo…tunaishi katika sintofahamu. Sintofahamu ni janga la kuwa na taarifa vizuri, lakini bila kujali hali halisi ya wengine.  Hilo ndilo shimo kuu, shimo  kuu la sintofahamu. Papa Francisko akendelea na muktadha huo pia amebanisha suala jingine linaloshangaza. “ Hapa tunatambua jina la masikini kuwa Lazaro. Hata Tajiri alikuwa anajua kwa maana alipokuwa kuzimu alimwomba Ibrahimu atume Lazaro, alikuwa anamfahamu vizuri! Lakini “ umtume huyo”…  Sisi hatutambui jina la tajiri.

Papa Francisko akiendelea na ufafanuzi wake huo mesema katika Injili haitaji jina la Bwana huyo  alikuwa anaitwa nani. Hana jina. Alikuwa amepoteza jina. Alikuwa ametumbukia ndani ya vitu vya maisha yake. Tajiri na mwenye mali…alikuwa anajulikana kwa vitu tu. Jambo hilo ndilo linatufanya kuwa na ubinafsi ndani mwetu na kupoteza utambulisho halisi, jina lako kukupelekea  kuthamanishwa kwa vitu tu na viambishi.  Mambo ya kidunia yanatusaidia katika muitadha huo,yaani “Sisi tumeangukia katika utamaduni wa mambo ya vitu, mahali ambamo thamani yako inageuka kuwa kile ulicho nacho na kile ambacho unaweza… Lakini je unaitwa nani? Umepoteza jina. Sintofahamu zinakupelekea katika hali hiyo. Kupoteza jina na kubaki na jina la matajiri, maana ya kuwa na viambishi. Leo tumwombe  Bwana neema ili tusidumbukie katika sintofahamu, tuombe neema ya kuwa na habari zote za machungu ya wanadamu ambayo tunayo, na yaweze kushuka ndani ya mioyo na kutuchochea kufanya jambo fulani kwa wengine.

PAPA:MAHUBIRI

 

12 March 2020, 10:52
Soma yote >